The Chant of Savant

Sunday 2 August 2015

Who’s using whom in UKAUA shotgun marriage?






















He kept them guessing. He kept other wishing. Others were hunting
He himself was scheming. At last, there came breaking news
Luwasha had made a hard decision. Will this marriage live long? Who’s using whom?
After the former Big Minister (BM) Eddie Luwasha officially uprooted himself from Cham cha Mizengwes (CcM), boozers have a lot of questions vis-à-vis the whole hustle and bustle. Some fully endorse the move saying it is nice save that Luwasha and UKAUA have a lot to explain.  However, some oppose the move as they want to know when and how Luwasha saw the light so as to become one of those they used to believe are on the other side of the river aspiring to emancipate them from corruption Luwasha is accused of partaking? They think both Luwasha and the opposition have proved beyond doubts to be opportunists who’d not be trusted. What logic can one apply to crack the brainteaser whereby three doctors abandoned their positions to stand against CcM’s flag bearer to an immigrant in opposition circles?  Many’d want to know how Luwasha and opposition will reconcile their incompatible interests as far as ulaji is concerned. Again, politics has full of miracles, miracles, and miracles ad infinitum. Indeed UKAUA has killed our hearts and minds.
Everything in politics is possible. No permanent enemy or permanent friend in the business of looking for eating free and getting richer and richer fast. Boozers expected that they’d choose their chief eater between CcM’s and UAUA’s candidates.  Now that –if Luwasha is seconded by the opposition to vie –all candidates are from CcM boozers seem not to get it. They even don’t know if this pact results from love, patriotism or even business. I heard some boozers allegedly saying that with dosh in Bongolalaland you can buy even presidency. They reminded me of EPA and 2005 presidency in which the same dude was player.
 When the news of Luwasha’s defection broke, one boozer said that you can trust all but not a politician and a prostitute. Unfortunately, he gave no reasons.
Now that Luwasha is one the other side, we’ll he get his dear power that he’s sought by all means even? Boozers think that if he wants to succeed, he must link Jake Kiquette with Richmond and show how he’s receiving order from above. So, too, he must tell the whole truth and seek forgiveness from the boozers. This way, maybe, he can make sense of his move failure to which he may end up being like Mlema. It is too early to tell however in politics anything is possible. It seems that UKAUA is good at preaching water and drink wine. They’re turning boozers into chapatti they can turn any way they like. Boozers want to know. Why’s Luwasha now clean like snow while the same opposition used to tell them the guy was stinky? Were they lying to them?  It seems that after being defeated for many times they’d no choice even if it requires them to have a devil to win the coming elections, they’ll succumb before it. Sad for CcM, they took everything for granted little knowing that politicians are unpredictable especially when their interests are sabotaged or foiled. Is Luwasha going to fulfill his journey of hope? Will his move mark the beginning of the end or the end of the beginning after the said journey ends hopelessly? Will the arrival of Luwasha in the opposition bring blessings or bad blood? Who knows?
I thought Tanzanians would like to have a third and alternative force in that they ditch CCM and UKAUA due to the fact that they all have proved to be the same crap and corrupt. Again, where’s this third force? I can see the wisdom that the type of politicians you find in a certain country represents the type of the people that country has. I don't like to generalize. However, I can comfortably argue that CCM and UKAUA look alike and also look like Bongolalalanders.  That’s why change will always be history in Danganyika.
If UKAUA want to carry the day, Luwasha must not run for president or being picked as running mate. He’d play behind the curtain to make sure that they win first then they’ll know how to divide ulaji. Again, when the hyena dances with the goat, what do you expect what comes next? I don’t know if UKAUA still remember the list of shame that Dr. Willy Silaha flung to the world on 15 September, 2007. Is it a time for someone licking his vomits or speaking in tongue? Will CcM keep mum as one of their cadres start turning tables against them? Will they take him with  all force to see to it he’s not spoiling their broth or just cool off and find another way to see to it they’re carrying the day? Will this shotgun marriage live longer especially after the elections? Is truly the couple in love or love business? Who is using whom in this marriage of convenience? “Earth provides enough to satisfy every man's needs, but not every man's greed.” Mahatma Gandhi once said.
Source: Guardian Aug., 2, 2016.

7 comments:

Anonymous said...

Salaamu Mwalimu Mhango.
Nimekua mwenye kukusoma katika kipindi chote ambacho ulichokuwa unamuongelea Lowassa akiwa CCM kuhusu mabovu,machafu na mapungufu yake yote,na pia unapomuongelea hivi sasa baada ya kuondoka CCM.Japo unamuongelea kwa hadhari kwamba uwenda akawa rais wa nchi, lakini bado unamuongelea katika sifa zile zile ambazo alizokuwa nazo akiwa ndani ya CCM.

Mwalimu Mhango,mimi nakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja kwa yote uliyo na unayo muongelea Lowassa isipokuwa hofu yangu tu kwamba kwa mtu ambaye asieijua Kaya yetu na anaeyasoma maandishi yako kuhusu mwanasiasa huyu anaweza kudhani na kuamini kwamba Kaya yetu ina wanasiasa wengi wazuri na wasafi ambao wanastahiki zaidi nafasi ya kutwalia urais kuliko mwanasiasa huyu mchafu wa kuitwa Lowassa.Kwa maoni yangu Mwalimu Mhango,tangu iingie awamu ya pili mpaka hii ya nne madarakani kwa muda wa miaka 30 mimi sioni hata kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa CCM ambaye aliekuwa safi au msafi ambae alikuwa anastahiki kuwatumikia wananchi wa Kaya yetu kwa maadili ya uongozi na kuwajibika kwa manufaa ya nchi na wananchi.Naam,Mwalimu Mhango Lowassa ni fisadi kama walivyokuwa mafisadi viongozi wengine wa CCM,naam,Lowaza ana utajiri ambao hatujui chazo chake kimeanzia wapi kama walivyokuwa Viongozi wengine wa CCm ambao ni matajiri na hatujui utajiri wao umeanzia wapi,naam,Lowassa ni mwizi na jambazi kwa wananchi wa Kaya yetu kama walivyokuwa viongozi wengine wa CCM.Kwa hiyo CCM kimekua ni chama cha ujambazi na ufisadi na hakuna msafi hata mmoja zaidi ya kutaka kutuibia na kuigeuza nchi kama shamba la bibi kwa wao,waramba viatu wao na familia zao.

Mwalimu Muhango,udhani kwamba labda Mungu anataka kuwakomboa watanzania kutoka katika mikono ya CCM.Kwani CCM wamejitungika wao wenyewe kitanzi cha kifo cha kisiasa pale walipoingiza ubinafsi,chuki,majungu fitina na husda dhidi ya Lowassa na kukiuka maadili ya kwao wenyewe ya jinsi gani ya kumtafuta na kumpata mgombea urais katika chama chao, kana kwamba nchi inatawaliwa na chama kimoja badala ya kumkumbatia na kumpitisha mtu ambae anaetakiwa na wengi ndani ya chama na wananchi mtu ambaye angewafanya waendelee kubaki madarakani wakaendelea kutunyanyasa,kutuibia na kuundeleza ufisadi wao wa hali ya juu, kisha wangekaa kitako na kujaribu kutatua matatizo yao ndani ya chama wakiwa madarakani.Hili ni kosa ambalo wapi walipojiamini na kutoona nini kitachotokea baada ya maamuzi yao hayo ya watu wachache kumweka mtu waliemtaka wao.Je dhamana gani ambayo waliyokuwa nayo kwamba watashinda tu uchaguzi? (maandishi yanaendelea)

Anonymous said...



Salaamu Mwalimu Muhango,kwa kupiga makelele eti Lowassa ni fisadi na mroho wa madaraka ni kama vile hatuelewi nini siasa au siasa ni nini.Kama inavyojulikana kwamba siasa ni mchezo machafu wenye rafu za kila aina na mwanasiasa yoyote yule duniani ni lazima asifike na sifa ya uroho wa madaraka kwani hilo ndio lengo la mwanasiasa yoyote yule duniani,na kama mwanasiasa huyo hana uroho wa madaraka huyo anakuwa sio mwana siasa bali unakuwa ni amateur katika siasa na hakuna moderate temperature kwa uroho huo.Na kwa mwanasiasa mzoefu atatumia njia zote kwa kila njia za halali na zisizokuwa za halali na atatumia rafu zote ili afike madarakani,Je CCM walikuwa wanaamini kabisa kwa kukatwa jina la Lowassa,Lowasa huyo atasema nimesikia,nimetii na nimekubali?Ebu tukumbuke nini alivyobainisha Niccolo Machiavelli katika kitabu chake kinachojulikana kwa jina la The Prince jinsi mwanasiasa atakavyopigania (kwa kutaka kuyapata madaraka) aliandika "Principality which may be acquired by several methods: by one's own power, by the power of others, by criminal acts or extreme cruelty, or by the will of the people.
Na ana msemo wake mwingine maarufu katika kitabu chake hicho ambao ni moja ya muhimili mkubwa wa wanasiasa wote duniani wanautumia wakiwa madarakani au wakiwa katika harakati za maisha ya kisiasa ambao""The ends justify the means"!Kwa hiyo Lowassa tunamuona hapa akiufuata maagizo ya Niccolo Machiavelli katika kitabu cha The Prince!

Naam,Mwalimu Muhango, Lowassa ni mwanasiasa mzoefu na ni mzoefu pia kiutendaji na anapendwa na sehemu kubwa ya wananchi je kwa nini watanzania tusuitume nafasi hii alietuletea Mungu kuing'oa CCM madarakani?ENOUGH IS ENOUGH kutawaliwa na CCM.Na kusema kwamba Lowassa ni FISADI ni sawa na watanzani kutumia ufumbuzi wa mbuni wa kuzamisha kichwa chini ya mchanga na kutoona tatizo kwamba CCM ni chama cha mafisadi,mimi nauliza Mwalimu Muhango,ebu na tukubaliane kwa hoja ya mjadala kwamba Lowassa ni fisadi Lowassa mwizi lakini na tumuungalie upande wa pili wa sura ya Lowassa ambae anazingatiwa ni mzoefu na mchapa kazi na ni mmoja wa matajiri wa Tanzania je ni bora kumuweka mtu tajiri madarakani ambae akatuuma na kutupuzia au kumleta mtu ambae ni masikini na akaanza kutung'ata bila ya kutuonea huruma yeye,wafuasi wake na familia yake?Watanzania wakumbuke kwamba nchi zote zilizoendelea bila ya kuwa tajiri uwezi kuukwaa urais au uwaziri mkuu.Kudai kwamba Mwalimu Nyerere alimkataa Lowassa kwa hoja ya ufisadi,ni kweli kabisa tunalijua hilo lakini kwa wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere kwa vile tulikuwa na siasa ya chama kimoja na siasa ya ujamaa ambayo viongozi wake walikuwa chini ya darubini kwa mapato yao,lakini sasa Tanzania sio nchi ya ujamaa tena na haina hata maadili ya ujamaa ambayo aliyoyajenga Mwalimu Nyerere,Tanzania sasa ni nchi ya kibepari na tunataka viongozi watakaekuja madarakani wawe matajiri ili wasituibie sana kiongozi ambae ataipigania katiba ya wananchi na sio katiba ya mafisadi,kiongozi mwenye maadili ya utawala bora mwenye kuwajibika na kuwajibisha.Mwalimu Muhango,tumekuwa watumwa wa CCM kwa miaka 30 sasa na umeshafika wakati wa kujikomboa katika utumwa huo ni sisi wenyewe watanzania ndio waamuzi wa kumuweka tumtakae kwa kupitia sanduku la kura,na tuwe na hamasa ya kujikomboa na hata mtu ambaye anaetaka kutukomboa amejitenga na waliokuwa wanatufanya watumwa kwa miaka mingi tusimuulize ni wapi na vipi atatukomboa,wache atukukomboe kwanza kisha katika miaka mitano ya awali ya kuwa kwetu huru ndipo tutajua alikuwa na nia gani.Mwalimu Muhango,Nimeyandika haya si kwamba namkubali sana Lowassa bali nauongelea ukweli uliopo ardhini nao ni kwamba umeshafika wakati wa kuing'oa CCM madarakani na kuitia katika kapu la historia ya kiza na kusaulika na watanzania kuwa huru BY ANY MEANS NECCESSARY NA LOWASSA NDIO NJIA!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon shukrani kwa kurejea na hoja zenye ushawishi ingawa sikubaliani nazo. Ni kweli watanzania japo si wote wangependa kuona anguko la CCM. Hasa kwa wale wapenzi wa vyama kila mtu anatetea chama chake. Kwa akina sie tusio na chama tunaotetea maslahi ya taifa, hatuna upande zaidi ya kutaka haki itendeke kwa watu wetu. Tunao ushahidi wa kutosha kuwa hatupiganii maslahi binafsi. Kwa mtu kama mimi niliyetoka wakati wa Mkapa itakuwa jambo la ajabu kuwa na maslahi binafsi. Hivyo, kusema wote tuwe Machiavellian ili kuiondoa CCM bila kujua hawa tunaowatumia wakishapata madaraka watatuenza vipi si jambo jema. Kwetu sisi iondoke isiondoke CCM tunachotaka ni mabadiliko yenye kujali maslahi ya umma na si mabadiliko ya vyama au sura. Kama Lowassa ni fisadi ni fisadi tu hata kama ataiondoa CCM. Unategemea afanye nini baada ya kuiondoa CCM zaidi ya kufanya unyani ule ule?
Nadhani tunapoteza kipaumbele kama walivyoonyesha wapinzani kwa kudhani adui wa Tanzania ni CCM na si mfumo. Tunachopaswa kupambana nacho si CCM wala Lowassa wala Magufuli bali mfumo fisadi uliowatengeneza na kuwalisha akina Lowassa na wengine. Nilikuwa nikiangalia matokeo ya kura za maoni na wafanyabiashara tena wabaguzi wa kihindi wanavyoshinda. Hii nayo ni hatari hasa ikizingatiwa kuwa watu hawa tangu waletwe na mkolono wamekuwa wakijitenga nasi kijamii na sasa wanajifanya kuwa wenzetu kisiasa ili waendelee kuhujumu uchumi wetu wakisaidiana na wahindi weusi. Leo hili si hoja. Nimalizie kutokana na kutokuwa na fursa ya kutosha kwa kusema kuwa sina ugomvi na CCM CHADEMA wala Lowassa. Nina ugomvi na injustices na kwangu the end doesn't justify the means or the means to justify the end only justice justifies everything. Naomba uniwie radhi siwezi kujibu hoja zako moja baada ya nyingine zaidi ya kutoa jibu la jumla.

Anonymous said...

Salaamu Mwalimu Mhango,
Kwanza kabisa ningependa kukupongeza kwa kuchukua wakati wako ambao umebanika sana na kuwapa umuhimu wasomaji wako kwa kujibu maoni yao.Hili linatia moyo sana kwa sisi wasomaji wako kuendelea kuchangia maoni yetu kila inapolazimika kufanya hivyo,Japo umesema kwamba umejibu jibu la jumla lakini umegusa sehemu kubwa ya maoni yangu,

Mwalimu Mhango umenjibu kwa kuandika ".......Nadhani tunapoteza kipaumbele kama walivyoonyesha wapinzani kwa kudhani adui wa Tanzania ni CCM na si mfumo.Tunachopaswa kupambana nacho si CCM wala Lowassa wala Magufuli bali mfumo fisadi uliowatengeneza na kuwalisha akina Lowassa na wengine" kwa hoja yako hii kunaleta swali ambalo linajiuliza lenyewe kwa nguvu sana,JE NI NANI MWENYE JUKUMU LA KUWAJIBIKA KUPAMBANA NA MFUMO FISADI NA KUUNDOA NDANI YA CCM KAMA ITASHINDA UCHAGUZI AU IKISHINDA UKAWA?NA JE TANGU CCM IMEKAA MADARAKANI KWA MIAKA YOTE HIYO 30 YA AWAMU HIZI TATU KUMESIKIKA SAUTI YOYOTE ILE YA KIONGOZI AIDHA ALIEKUWA MADARAKANI KAMA NI RAIS AU KIONGOZI WA NGAZI ZA JUU AMBAYE AMEBEBA BANGO LA KUPAMBANA NA MFUMO FISADI NDANI YA CHAMA NA KUONGELEA INJUSTICE YA WANANCHI?

Mwalimu Nyerere alisema kwamba "endapo watanzania hawatopata mabadiliko ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM"natujiulize je ni mabadiliko gani hayo ambayo Mwalimu Nyerere aliyoyakusudia?Kama si kuuondoa na kupambana na MFUMO FISADI NDANI YA CCM na ili kuwepo na haki,uadilifu na uhuru kwa wananchi na kwa nchi?CCM imekaa madarakani kwa miaka mingi na wameshaamini kwamba wanaweza kufanya chochote kile dhidi ya nchi na wananchi na hakuna kitachotokea na dio mana mfumo wa ufisadi umekuwa ni kama gonjwa la saratani ndani ya CCM.Kwa hiyo na kuwepo na njia ya kuondolewa CCM madarakani hata kama njia hiyo inaongozwa na Shetani na uwenda kwa mabadiliko hayo vyama vyote vitakuwa na utambuzi kwamba wananchi wanaweza kukiondoa chama chochote kile madarakani endapo hawatopata madiliko waliyoyatarajia.Lakini kusema kwamba kupambana na MFUMO FISADI bila ya wananchi kufanya wimbi la mapinduzi kwa kukiondoa chama cha CCM madaraka itakuwa ni sawa na WISHFUL THINKING kuliko UKWELI WA ARDHINI ULIVYO.
Kuna msemo usemao kwamba" endapo wananchi hawatokuwa tayari kubadilika na kuleta mabadiliko katika jamii yao au nchi yao wasitegemee kwamba mabadiliko yanaweza yakaja kutoka mbiguni.

Mwalimu Mhango,tunajuwa wazi kwamba swala la wahindi kuanzia Afrika kusini,Tanzania,Kenya na Uganda wamepandikizwa na wakoloni wa kiingereza kwa kulinda masilahi ya wakoloni hao kwa kumiliki njia zote za uchumi za nchi hizo kama tulivyofikia sasa na kuwa ni sehemu ya kuimarisha mfumo wa ufisadi uendelee kwa masilahi yao na mabwana zao(wakoloni).Iddi Amini alipowachukulia hatua za kizalendo wahindi hao hawakurudi kwao India bali walikimbila UK na Canada wakiwa na uraia za nchi hizo na wahindi hao japo ni raia wa Tanzania lakini mioyo yao na imani zao hazipo Tanzania bali ni UK na Canada.Kwa maoni yangu hawa ni wasaliti tu vyovyote vile watakavyojifanya na usaliti huo wanashirikiana na viongozi wetu ambao nao wanaukubali usaliti huo kwa masilahi yao binafsi.Na tusisahau kwamba wengine wameshauona udhaifu wetu huo wa kuiona Tanzania ni chuma ulete, angalia wimbi la wachina,waturuki na wengineo wanavyoanza kujizatiti katka nchi yetu kwa hoja ya uwekezaji wakiwa wananlindwa na viongozi wetu wasaliti wa nchi na wananchi wake.

Swali lilobaki ni hil, je nini tufanye ili tuweze kupambana na wasali hawa?Je tumechelewa kuwachukulia hatua zinazostahiki kama wengine wanavyodai au kutakuja wakati wakakapatina viongozi wenye uzalendo kama Idi Amini?

Nasema tena ahsante kwa kujibu maoni yangu pamoja ya kwamba wakati wako kuwa finyo.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon, usemayo yana msingi sema mimi siku zote ni mtu wa machele. Nisingependa tuangalie upande mmoja kwa kutaka kupata au kusikia tunachotaka kupata au kusikia. Hivi ikitokea UKAWA wakabwagwa nini plan B? Nadhani kupambana na mfumo si kuondoa CCM wala kutochagua upinzani bali ni kwa watanzania wote kugeuka na kuchukua jukumu hili kuwa la kila mtu. Hata wakiingia wapinzani hali inaweza kuwa hivyo hivyo kama tulivyoshuhudia kule Zambia baada ya kuangusha UNIP au Malawi baada ya kufutilia mbali MCP. Hivyo, bado naamini kuwa dawa isiwe kuondoa CCM bali mfumo. Atauondosha nani? Watanzania wenyewe watakapokubali kubadilika ili wawabadilishe wanasiasa wao.
Kuhusu hili la wahindi na ndoa ya kisiasa kweli linakera nalo pia linapaswa kushughulikiwa na watanzania wenyewe wakaacha kuwaabudia. Huwa napiga picha kama magari na starehe wanazoishi nchini ingekuwa waswahili kwao mbona wangewachoma moto. Niliwahi kuandika kuwapo kwa jamii ya waafrika iitwayo Jarawa kwenye visiwa vya Andaman ambao wamegeuzwa kama nyani wa kufanyia utalii baada ya kutelekezwa na serikali ya India. Pamoja na ukatili na unyama huu bado hata waafrika hatukuchukia. Hata makala yenyewe nilipoiandika haikupata wa kuchangia au kusoma. Google kwenye blog hii kwa kuweka neno Jarawa hapo kwenye nafasi ya kupekua utaiona na kuisoma.
Kujibu swali lako la muhimu ni kwamba tubadilike tuanze kuchukia uoza, ubaguzi, ufisadi na kila takataka badala ya kushi kwa matumaini na kukata tamaa hadi kutegemea mafisadi waliotuuza eti ndiyo waje kutukomboa. Sana sana watatutumia na wakishapata wanchotaka wanatubwaga kama nepi au kondomu.

Anonymous said...

Salaamu Mwalimu Mhango,
Naona hatukutofautiana kimsingi kwamba ni nani ambaye anajukumu la kubadilisha MFUMO FISADI kwa chama chochote kile ambacho kitachokaa madarakani,ya kwamba jukumu hilo ni la wananchi wenyewe wa Tanzania ulipoandika "...... Watanzania wenyewe watakapokubali kubadilika ili wawabadilishe wanasiasa wao."Sasa kama tumeliona hilo inabidi tuuilize ni wakati gani ambao wananchi hao watakubali kubadilika ili wawabadilishe wanasiasa wao?Wakati ni huu na kama watanzania watasita au watafeli kwa hali hii iliyotokea ya kisiasa nchini hatutoweza kufanya mabadiliko yoyote yale.Nitasisitiza tu zaidi kwamba tuivunje hali ya kisaikolojia ya wanasiasa wetu ya kujiamini kwamba wao ni ma-ELITE ambao wanamiliki nchi na wananchi na kutuweka katika saikolojia ya akili ya kundi la nyati au mbogo(CATTLE MENTALITY).Wachunguzi wa kisiasa za kiafrika wanadai kwamba vyama tawala vinashinda na kubaki sana madarakani kutokana na ujinga,ujinga wa wananchi wao hususa wa vijijini ambao hawaelewi chochote kile kinachoendelea zaidi ya kile ambacho chama tawala kinachoona au kuimbisha.Mwamko wa kisiasa wa wananchi ndio muhimu hapa kwa hiyo vyama pinzani vina jukumu la kutilia mkazo kampeni zao vijijini vya kuwaelimisha wananchi hao nini faida ya kuwepo kwa siasa ya vyama vingi nchini na ni nini maana yake,maana yake ni kwamba wananchi ndio wenye msemo wa mwisho wa nani akae madarakani kwa ajili yao na kwa ajili ya nchi na wanasiasa wetu hawataki tufikie huko lakini inawezekana ukawa huu ndio wakati muwafaka.

Naam,Mwalimu Mhango,nimeisoma makala ya "JARAWA" hakika ni ukweli tupu na ukweli mchungu sana ni vigumu kuumeza kwa kila mwenye hisia ya uzalendo na fikra za kimapinduzi naweza kusema tu ya kwamba wakaoloni na vibaraka vyao wamefanikiwa kutukinaisha kwamba sisi waafrika hatupendezi,hatupendezi rangi yetu,hatupendezi maumbile yetu,akili zetu hazijakomaa na hazitokomaa na hatuwezi kujitawala na kujiletea maendelea ya nchi zetu na jamii zetu.Hatimae tumefikia kuaamini hayo tumekuwa wenye kujihisi upungufu kwa kila upande tunapokabiliana na wakoloni hao na vibaraka vyao,na kibaya zaidi kwama kuna baadhi ya viongozi wetu wamekuwa cloned ili wawe kama wakoloni wenyewe na ndio waotutawala kutuumiza na kutudhalilisha.Je kizazi kijacho kitatuelewa vipi endapo tumeshindwa kujikomboa kiakili na tumebaki na uhuru wa bendera tu?Naweza kuuona na kuelewa uchungu wako na hasira zako kwamba makala yako ya JARAWA imepuuzwa kama kwamba hukuwaandikia waliopaswa kuandikiwa na kusomwa na kui comment!Niliiona documentary hiyo ya community ya JAWARA kwa miaka mingi iliyopita ambayo iliniacha speechless.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon, tukubaliane kimsingi kuwa sisi wananchi ndiyo wenye dhima na dhamana ya kuleta mageuzi tunayotaka na yanayotufaa kwa kujenga tabia ya kutowaachia wanasiasa wajifanyie watakavyo kana kwamba hatuna stake kwenye wanachofanya. Mfano mzuri ni mapokezi ya Lowassa na kuteuliwa kupeperusha bendera ya UKAWA. Sijui wananchi tumeshirikishwa au kutoshirikishwa kiasi gani. Nadhani, kwa ufupi, tuanzie kwenye hili kuelekea huko tunakotaka na kulenga kuelekea.