How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Sunday, 1 September 2019
KUZUILIWA NDEGE YETU KWANINI WATANZANIA TUSHINGISHANE KILA MMOJA SH 100 NA KUIREJESHA AU KUWEKA BOND IKAACHIWA?
Kitendo cha ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania kushikiliwa nchini Afrika Kusini tokana na madai ya mkulima mmoja, kinalitia hasara shirika ukiachia mbali kuchafua jina la taifa letu. Kuepuka hasara, nashauri watanzania tuitishe mchango wa kila mtanzania huku wenye uwezo wakiwachangia maskini ili kupata pesa ya kuweka poni mahamani ili ndege yetu iachiwe wakati kesi ikiendelea. Sidhani kama taifa lenye watu zaidi ya milioni 50 tukiamua kila mmoja achangie shilingi lau mia tutashindwa kurejesha ndege yetu ili iendelee kuchapa kazi wakati kesi ikiendelea nasi tukitafakari namana ya kuepuka kurudiwa kwa kadhia hii.
Pia wakati tukichangishana, tungewasaka waliosababisha hujuma hii ya uchumi kuanzia aliyetoa hukumu ya awali hadi walioingia mkataba na mdai na namna alivyokuwa amewekeza ili tujiridhishe kuwa hakuna rushwa au kama kuna makosa kuhakikisha hayatarudiwa kwenye uwekezaji mwengine na kama kuna waliopatiwa chao kiwatokee puani.
Kwa leo ni haya tu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment