How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Saturday, 5 October 2019

HAKI ZA BINADAMU ZIHESHIMU HAKI ZA WENGINE-KUDOS MAGUFULI


Hakuna shaka. Nchi za kiafrika zimekuwa zikipwakia kila uchafu kutoka ulaya bila kufikiri. Mojawapo ya jambo tulilopokea kijinga tena bila kufikiri sawa sawa ni kama kuzuia kuwaadhibu watoto wetu eti kwa vile tunavunja haki za binadamu. Je tulijiuliza ni kwanini wazungu walianzisha hizi haki za kutowaadhibu watoto?
 Waliowahi kuishi ulaya wanajua fika namna ambavyo kizazi chake cha sasa ni migogoro mitupu. Sababu mojawapo ya kuanzisha marufuku dhidi ya kuadhibu watoto ni ile hali kuwa wazungu walifikia kuua watoto katika kuwaadhibu. Afrika hatujafikia hapa. Mila za kiafrika ziko wazi kuhusiana na kuwaadhibu watoto. Kuna haja ya kutafakari kwa makini mambo mengi tunayoletewa bila kufikiri. Mfano, kuna clip inatembea kwenye mtandao inayoonyesha mzungu mmoja akikiri kuwa walieneza ukimwi barani Afrika kwa makusudi. Mbali na hilo, haiwezekani watu waliotutawala, kutuuza kwenye utumwa na kuendelea kutunyonya chini ya mifumo yao ya kisasa wawe na uchungu nasi. Hivyo, kuna haja ya kujisimamia kama alivyofanya rais John Magufuli kusema wazi wazi kuwa adhabu ya viboko mashuleni ilejeshwe ili kujenga taifa lenye maadili ya kiafrika kwa ajili ya kesho.

No comments: