–––muda mfupi kabla ya kupiga kura–––kuwa wapinzani wangeshindwa vibaya, wapo walioniona kama mtu anayejipendekeza kwa chama tawala wasijue ukweli utasimama tena si baada ya kitambo kirefu. Sasa matokeo yametoka, na ukweli umejulikana. Uyakubali hata uyakatae, waliodhani nilikuwa nakipendelea chama tawala hawana la kusema bali kushangaa ilikuwaje japo ilikuwa rahisi kutabiri kipigo kilichotokea. Hata kama hupendi kitu, kusema ukweli ni sehemu mojawapo ya kukusaidia kufikisha kile unachoamini au kutaka kuwasilisha. Pia kuukubali ukweli husaidi kimkakati kupambana na kile unachotaka kupambana nacho kisayansi na si kwa kujilisha pepo au kutegemea miujiza.
Pili, mwanakijiji ambaye tangu tupate uhuru ameishi kwa kibatari halafu ghafla, ndani ya miaka mitano, akapata umeme huwezi kumwambia kitu. Kama kuna siri ya wapinzani kuangusha vibaya, si nyingine bali hii. Wapo waliokejeli kuwa watanzania sasa wanasifia, barabara, flyover, kusambazwa umeme, mabwawa ya kuzalisha umeme, madaraja, meli, ndege, reli, umeme na mengine mengi. Je walitaka wasifie nini wakati hizi ni nyenzo za maendeleo?
Tatu, mama aliyekuwa akijifungulia nyumbani au kwenye zahanati inayotegemea kibatari asingeweza kuchagua yeyote zaidi ya yule aliyewezesha kupatikana huduma ya uhakika. Mamantilie aliyekuwa akimwagiwa chakula chake na migambo au machinga akifukuzwa na kukamatwa hovyo hovyo asingemchagua yoyote zaidi ya aliyekomesha kadhia hizi. Mwananchi mchukia rushwa asingeweza kumchagua mwingine zaidi ya yule aliyeikomesha.aliyekuwa akisafari kupitia nchi jirani kwenda Dar asingemchagua yeyote zaidi ya aliyetatua tatizo lake.
Nne, mwananchi aliyekuwa amekosa kazi tokana na ajira nyingi kuchukuliwa na walioghushi au kutolewa kikabila, asingeacha kuchagua aliyekomesha kadhia hizi. Hapa hatujaongelea usalama kwa ujumla. Mikoa iliyozoea kutekwa kwa magari usiku na kushamiri kwa vitendo vya ujambazi asingechagua wapinzani hata wangemwimbia mashairi mazuri kiasi gani.
Tano, ukizingatia ukweli hapo juu, utagundua kuwa hata malalamiko juu ya matokeo ya uchaguzi uliokwisha na kukipa chama tawala ushind mnono, yatahitaji Ushahidi wa nguvu kweli kweli kusimamisha kesi ya msingi. Kwani, madai yanayotolewa kwa sasa, kimahesabu ya kura na matokeo, yanakosa uzito japo hatupingi kulikuwa na matukio yaliyoripotiwa bila kutolewa Ushahidi shahidi. Hii ni kazi ya mahakama; si kazi ya uchambuzi. Tunaambiwa kura za urais rais Magufuli ameshindwa kwa kura zaidi ya 12,000,000 dhidi ya mpinzani wake wa karibu aliyepata kura takriban 2,000,000. Hii maana yake nini? Je mshindi alipewa kura ngapi feki au tuseme mshindwa aliibiwa kura ngapi? Wangepishana kura kama elfu kadhaa, madai ya wizi wa kura yangeweza kujenga ushawishi hata kama yangekuwa ya kuzua. Kwa hali ilivyo, tukubali, upinzani umeshindwa vibaya ikilinganishwa na uchaguzi wa kabla.
No comments:
Post a Comment