The Curse for Salvation

The Curse for Salvation

Wednesday, 9 September 2026

Chunga Wafyatuaji wa mafyatu wanapofyatuana!

Juzi, nilishuhudia maajabu yasiyo ya kawaida tena ya kifyatu. Sikujua kuwa kumbe hata wafyatuaji wawafyatuwao mafyatu wanaweza kujigeuza mafyatu wakawafyatua mafyatu wasio na hatia na baadae wakafyatuana wao kwao. Nikiwa nimeenda kichakani kuchegama na kupiga lisiragara kubwa si nikakuta majembuzi sorry wafyatuzi wakubwa wawili wawafyatuao mafyatu wakifyatuana! Hakuna kilichonishangaza kama fyatuzi kubwa kulifyatua saidizi eti kwa kukataa kwenda kufanikisha dili la kufyatua ujambazi sehemu sehemu.
            Baada ya mafyatuzi haya mawili makatili na mafisi yaliyojaa unyaninyani na ungedele kuwafyatua mafyatu waliogoma kufyatuka na kuyafyatua kwa muda mrefu si yaligeukana na kufyatuana huku kubwa lao likifyatua dogo lake kuepuka kufyatuliwa au kuwafyatua mafyatu wakafyatuka na kulifyatua likafyatukia mbali. 
            Nasikia, sijui liligundua au vifyatuzi vidogo vililetea umbea dhidi ya lile saidizi hadi yakakosana kiasi cha kufukuzana kwenye genge lao kimtindo hadi kuwafyatua mafyatu waliobaki wakihaha kutafuta sababu za kufyatuana huku ambao si chochote wala lolote bali bonge la sanaa na zengwe. Kumbe mchezo huu auhitaji huruma wala kumbukumbu! Ukigundua fyatu mwenzio mnayefyatua mafyatu pamoja anataka kukufyatua, unamfyatua kabla ya kukufyatua au kuwafyatua mafyatu wakakufyatua na ukasahaulika au hata kuishi lupango.
            Nani angeamini kuwa hata mafyatuzi yanayo matambiko? Kabla ya fyatuzi kubwa kulifyatua dogo, lilifyatua vigagula wake vikavyatuka na kumfyatua hasimu wake ili kuweka mazingira ya kufyatuana kirahisi na kisanii. Na kweli, haiwi haiwi, si huwa. Si Fyatu kuu lilifyatuka na kumfyatua dogo hadharani tena bila kueleza sababu za ufyatuaji na ufyatuzi huu kiasi cha kuwazuga mafyatu wasifyatuke na kutaka kujua kunani! Fyatu kuu lilijifyatua na kufyatua mambo kana kwamba kaya ya Fyatuland ni mali yake binafsi linayoweza kuifyatua litakavyo bila kufyatuliwa.
         Kwa vile Fyatuland ina mafyatu wasiofyatuka na kuwafyatua wawafyatuao, nao si walifyatuliwa mkenge tena wakauingia kirahisi na dili likapita wakati kimakwelini walipaswa kufyatuka na kuwafyatua wawafyatuao. Mie nilidhani wangefyatuka na kufyatua mafyatuzi yote mawili lakini wapi. Hawakufyatuka bali kuufyata wakaishia kufyatuliwa kizwazwa kwa ufyatu wao uchwara usiofyatuka au kuwafyatua wakawafyatua wawafyatuwao ilhali wakiangalia!
            Kwa vile na ujembuzi unahitaji sanaa ya ufyatuaji, aliyefyatuka akafyatua na aliyefyatuliwa wote wawili wameufyata baada ya kufyatuana ukiachia mafyatu waliofyatuliwa nao wakaufyata wasifyatuke wakafyatua bali kufyatuliwa mkenge. Uzoefu wangu wa kifyatu unaonyesha kuwa hakuna haramu isiyo na vikwazo. Leo, wanafyatuana wao kwa wao. Kesho, nani ajua kuwa na mafyatu watafyatuka na kuwafyatua ili waache kufyauliwa tena kisanaa na kizwazwa? Unapopanda mbigili usitegemee kuvuna matunda. Utafyatuliwa iwe leo au kesho. Utafyatuliwa tu iwe uko ulajini ukiwafyatua wenzao au utokapo. Lazima ipo siku utafyatuliwa tu, taka usitake.
            Katika kutumia ujuzi na weledi wangu kama profesa wa ufyatuzi, naweza kutabiri ufyatuzi zaidi hasa mafyatu watakapofyatuliwa hadi wakachoka nao wakafyatuka na kuwafyatua wawafyatuao. Ni suala la muda. Huwezi kuuficha moto kwa kuufunika blanketi uvunguni ukajifyatua kuwa hautakua na kukufyatua. Kuna kipindi ufyatu ukimzidia fyatu hujifyatua na kuwaona mafyatu wengine kama hamnazo na wasioweza kufyatuka wakamfyatua akafyatukia mbali. Dunia hii we acha. Unaweza kujifyatua ukawafyatua wengine ukiamini unawadanganya wakati unajidanganya. Uwadanganyao wanaweza kukudanganya wakakaa kimya wakipanga kufyatuka na kukufyatua wakakuaminisha kuwa hawatafyatuka baadaye kukufyatulia mbali kudadeki.
            Japo kufyatuana baina ya majambazi ni jambo la kawaida, kuna haja ya kutumia lau akili japo kidogo. Wahenga wanasema kuwa ukiishi kwa upanga, utakufa kwa upanga. Ukiwafyatua wenzako, kuna siku watakufyatua tu. Ni suala la muda. Wanaweza kufyatuana na kuficha na mafyatu wakafyatuliwa na kuzugika na kuacha kufyatuka wakidhani kuwa ni vita ya panzi wasijue kuwa wakati mwingine yanaweza kuwa machezo au matezo kwa sie mafyatu wa mwambao. Hivyo, wanachofanya mafyatu wafyatuliwao na wawafyatuao si kushangilia kwa wanaowafyatua kufyatuana bali kujitahidi kuepuka kupoteza muda na kuwapa wawafyatuao fursa nyingine ya kujipanga upya na uzuri na kuendelea kuwafyatua.
            Kimsingi, mafyatu wawafyatuao mafyatu wakifyatuana na kudhoofishana yapaswa kuwa fursa kwa mafyatu kwa sababu wanatoa fursa kwa mafyatu kufyatuka na kuwafyatua wakati wakifyatukiana na kufyatuana na kusahau kuwa wale wanaowafyatua nao wanaweza kutumia hii fursa kufyatuka na kuwafyatua wawafyatuwao ila kuwanyina fursa ya kuendelea kuwafyatua.
            Kwa vile mfyatuano wa wafyatuaji wa mafyatu wasiofyatuka ndiyo umefyatuka, tutegemee nini? Je, mafyatu watajifyatua au kufyatuliwa wawafyatue hawa mafyatu wawafyatuao wanaofyatuana? Je watapoteza fursa hii ya dhahabu ya kufyatuka na kufyatua wawafyatuao? Je wasiofyatuka na kufyatua, watamlaumu nani iwapo watapoteza hii fursa na kuendelea kufyatuliwa badala ya kutumia hii fursa ya kufyatuana kufyatua?
            Kwa vile huu ufyatuanaji umenifyatua na kuwataka mafyatu wafyatuliwao wafyatuke na kufyatuka, sidaiwi lolote zaidi ya kutumiza wajibu wangu. Hivi kufyatua na kufyatuana ni nini na kwanini mafyatu fyatuliwa hwakufyatuka kujua kuwa kufyatuana kwa kunguru ni neema ya kunguru!
Chanzo: Mwananchi J'tano leo.

 

No comments: