Jose Mujica rais wa Uruguay ni mtu wa kutisha ingawa hana makuu. Nadhani ni rais pekee anayeendesha gari aina ya Gongo la Kobe au Volkswagen Beattle. Mujica haiishi hapo. Wakati marais wengi wakishindana kuiba na kujirundikia mali wao na familia zao, Mujica hutoa aslimia 90 ya mshahara wake kwa maskini. Ni rais ambaye urais wake una usalama zaidi kwa vile wanyonge wanamjua yeye ni nani kwao. Hata hivyo hakosi maadui hasa mafisadi na wapenda mali waliotamalaki dunia nzima. Je ni marais wangapi wanaweza kuvaa viatu vya Mujica?
The Curse of Salvation
Wednesday, 3 October 2012
Mjue rais wa watu
Jose Mujica rais wa Uruguay ni mtu wa kutisha ingawa hana makuu. Nadhani ni rais pekee anayeendesha gari aina ya Gongo la Kobe au Volkswagen Beattle. Mujica haiishi hapo. Wakati marais wengi wakishindana kuiba na kujirundikia mali wao na familia zao, Mujica hutoa aslimia 90 ya mshahara wake kwa maskini. Ni rais ambaye urais wake una usalama zaidi kwa vile wanyonge wanamjua yeye ni nani kwao. Hata hivyo hakosi maadui hasa mafisadi na wapenda mali waliotamalaki dunia nzima. Je ni marais wangapi wanaweza kuvaa viatu vya Mujica?
Tuesday, 2 October 2012
CCM inapogeuzwa kuwa mali ya familia ya Kikwete
- Angalau baadhi ya magazeti ya Tanzania yameanza kuona mwanga kuhusu uroho wa madaraka ambao umeanza kuwa ndiyo mtindo wa maisha nchini. Hili la rais Jakaya Kikwete na familia yake kuanza kujipenyeza kwenye nafasi za juu chamani kiasi cha kugeuka kama mali ya familia lingeandikwa na blog hii huenda lingeonekana kama kumchukia. Taratibu ukweli unaanza kuvuka mipaka. Je nini kitafuatia baada ya wakubwa kuvimilkisha vyama vyao kwa wana familia na marafiki zao bila kusahau waramba viatu wao kama inavyofanya CCM?
Leo utasikia majina ya ndugu kwenye safu za juu chamani hata wake na waume kwenye ubunge wa kuteuliwa hata kuchaguliwa kama ilivyo kwa familia ya Samuel Sitta, Shellukindo kabla ya mume kupigwa chini, Kawawa, Lissu, Nchimbi na wengine wengi.
Subscribe to:
Posts (Atom)