The Chant of Savant

Sunday 24 April 2011

Kikwete atamvisha nani hili gamba?




Breaking news ni kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Jakaya Kikwete imekubali kuwalipa matapeli wa kihindi wa RITES Dola 20,000,000 sawa na shilingi 30,000,000,000.

Wezi hawa walioingia nchini wakiwa maskini sasa wanaondoka vibopa. Walikuja na mabehewe 50 chakavu ambayo kwa nchi za wenzetu yameishakuwa written off na wanaondoka na mabilioni kutokana na majambazi wa kitanzania kuingia ubia na wale wa kihindi na kusaini mikataba tata.
Pia serikali italipa gharama zote za wezi wa RITES za kuja Tanzania na kwenda India kwa miaka yote minne ya jinai hii!
Je Kikwete anayejidai kujivua gamba atamvisha nani hili gamba? Ama kweli jamaa hafai hata kuwa baba mwenye nyumba kama tutamtendea haki.Maana ukisoma kisa kizima unagundua kuwa kumbe tuna majambazi na mataahira kwenye ofisi zetu hasa zile kuu. Bila kuandamana na kuangusha genge hili la majambazi tutauzwa tunaona. Maana baada ya kumaliza hivi vilivyopo huenda watependa kutuuza sisi kama taifa. Habari hii ya kutia doa ilikuwa itoke kwenye gazeti la Aprili 25 la The Guardian lakini ajabu iliondolewa kwenye mtandao haraka kiasi cha kuibua maswali mengi juu ya seriousness ya IPP kwenye kupambana na ufisadi.

2 comments:

Jaribu said...

Ndio maana siku kila kitu India na China, India na China. Wanaona ni rahisi kuingia nao hii mikataba ya utapeli. Enzi za ujamaa za akina ten percent, watu walikuwa wanakula rushwa, lakini at least miradi walikuwa wanatimiza. Umeme na maji yalikuwapo ingawa almost kila mtu alikuwa maskini. Siku hizi jamaa itikadi yao ni wizi bila kukamilisha chochote. Sina habari kuhusu reli hiyo, lakini sidhani kama inafanya kazi kama ilivyokuwa zamani.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu hujakosea. Tangu tujenge miji yetu kihindi na kuwakumbatia jamaa hao walioletwa na mkoloni kutuhanithi, tumegeuka wahindi. Hii ikichangiwa na kuwa na mtawala asiye na uwezo mkubwa kufikiri ndiyo usiseme. Atasema nini iwapo mikataba namna hii ndiyo iliyozalisha mtaji wa kununulia urais huku ikiendelea kutengeneza kiinua mgongo nyuma ya pazia?