The Chant of Savant

Sunday 10 April 2011

CCM: Nyoka hata ajivue gamba anabakia kuwa nyoka


Heri CCM wangeweka kichwa na mkia wa nyoka kwenye nembo badala ya jembe na nyundo

Kwa wanaojua tabia ya nyoka, watakubaliana nasi kuwa nyoka ni kiumbe pekee anayeaminika kuwa alilaanika kiasi cha kunyimwa miguu na sura nzuri. Pia, ukiondoa mijusi na baadhi ya wadudu, nyoka ndiye ana tabia ya kujivua gamba ikiwa kama njia ya kuchusha na kujihadaa kuwa ametakata. Hivi karibuni Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilisika kikisema kuwa kinajivua gamba. Hii maana yake ni kwamba CCM inajiona kama nyoka. Je CCM kwa kuja na staili ya kujivua gamba wanataka kutuaminisha kuwa tumetawaliwa na nyoka kwa miongo yote? Kwanini CCM ilichagua kujivua gamba badala ya kujisafisha (kuoga)? Kama ni busara iliyotumika kubuni usemi huu si busara kitu bali kujinanga.

Leo utasoma na kusikia kila vyombo vya habari vikisema eti CCM imeamua kujivua gamba kama alivyosema mwenyekiti wake Jakaya Kikwete. Je CCM ni joka kama wengi wanavyohoji?
Kwanini kujivua gamba na si vinginevyo? Kwanini si kujipanga upya? Joka hili li kati yenu. Je mtaendelea kutawaliwa na joka wakati kuna binadamu? Je kama CCM ni joka kichwa chake si Kikwete wakati kiwili wili ni Edward Lowassa, Rostam Aziz, Andrew Chenge na mafisadi wengine? Wakati umefika wa kumkata kichwa joka na kumzika ili binadamu aendelee na maisha yake mwanana. Je nyoka akijivua gamba anaacha kuwa nyoka? Nyoka ni nyoka hata ajivue gamba mara milioni.

No comments: