The Chant of Savant

Thursday 14 April 2011

kumbe wake za watawala wetu ni vipofu!


Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) mama Salma Kikwete akipokewa na viongozi mkoa wa Lindi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mkoani Lindi jana. Mama Salma Kikwete yuko mkoani humo kushiriki na kuhimiza shughuli za maendeleo ya wananchi. Picha: Aaron Msigwa, MAELEZO



Mjumbe wa Halmashauri ya baraza la umoja wa vijana wa CCM Ridhiwani Kikwete aliyevaa skafu) akikagua gwaride la viaja wa CCM, baada ya kulakiwa eneo la eneo la Ngunichile akitokea kufanya kampeni za ndani Liwale kwenda Nachingwea mkoani Lindi juzi, ambapo katika mkoa huo amefanya mikutano ya kuweka mikakati ya
ushindi wa chama hicho. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

Miraji Kikwete akiwa amepozi na mmojawapo wa waramba viatu wa baba yake mbunge na waziri wa zamani, Lawrence Masha
Rahma Kharoos Kasiga akitoa zawadi


Kwa walioshuhudia yaliyompata imla wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, mkewe Simmone na mtoto wake Michel, angeamini kuwa watawala wetu wangetia akilini.
Kwa aliyetafakari yaliyomkuta imla wa zamani wa Misri Hosni Mubarak, mkewe Suzana, watoto wao Gamal na Alaa na wake zao angedhani hili lingekuwa somo kwa watawala wetu na wake zao makupe wadandiao migongoni mwa madaraka ya waume zao. Lakini wapi? La kufa halisikii.
Kama mnavyoona hapo juu, Salma Kikwete mke wa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete mpenda safari na dezo amerejea ulingoni kwa upya baada ya kujizuia kwa muda kutokana na mashambulizi ya vyombo vya habari.
Wengi wanajiuliza; anapokelewa kisiasa kama nani? Ufisadi wa kimfumo upogo na upofu wa kutosoma alama za nyakati.
Tunachukua fursa hii kumshauri Salma agombee nafasi ya uongozi badala ya kuishi kama kupe mgongoni mwa rais. Huu ni ufisadi anaoendelae kutenda wakati CCM ikijitapa kuwa imejivua gamba. Kwanini haijivui gamba la ukupe uliotamalaki nyumbani kwa rais?
Leo utamuona Salma akilakiwa kama rais. Kesho utamuona Ridhiwani akipokelewa kama rais. Kesho kutwa utamuona Miraji naye akihojiwa kama rais. Mambo hayaishii hapo. Mtondo utamuona Rahma Kharoos Kasiga naye akilakiwa kama rais.
Tanzania ina marais wengi kuanzia Kikwete, mkewe, watoto wake hata nyumba yake ndogo. Mwe! Hawa watajifunza lini?

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hii kali kweli yaani familia nzima wapo kwenye shirika moja. Si ajabu nzhi yetu hakuna kinachoendelea isipokuwa familia za viongozi ndizo zinazoendelea ... Sijui ni lini WATANZANIA TUTAFUNGUKA?

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Kama waarabu wamefunguka iko siku na watu wetu watafunguka na kufanya kweli. Kama si wananchi basi wanasiasa watafanyia wao kwa wao kama ilivyotokea huko Ivory Coast ambako mke wa rais alikuwa rais wa rais wa nchi.
Tuombe matatizo kama migao ufisadi na upuuzi mwingine viongeze makali. Hawa makupe watatimuliwa kama mbwa koko umma ukiamua. Ni suala la wakati.