

Baada ya bunge kupitisha bajeti ya wizara ya Nishati bila kupingwa, wenye akili wamejiuliza swali moja kuu: Je ni kweli zile pesa alizokuwa akitaka kuchangisha katibu mkuu wa wizara aliyesimamishwa kazi David Jairo kweli zililenga kuwahonga? Kama ni vinginevyo, inakuwaje wapitishe bajeti ya wizara iliyotoka kuwahonga bila hata kuhoji shutuma hizi?
Wengi wanajiuliza ni kwanini wabunge, kama kweli siyo kutaka kufunika kombe mwanaharamu apite, hawakutaka waziri mhusika William Ngeleja na naibu wake Adam Malima wawajibishwe?
Je hii haiwezi kuchukuliwa au kutafsiriwa kuwa lao ni moja? Picha hiyo hapo juu inaweza kukupa picha halisi ya ndoa hii ambayo wakosoaji wanaiona kama ya wala rushwa wakubwa wa nchi yetu. Inakuwaje wampongeze? Wanampongeza Ngeleja na naibu wake kwa lipi kama wizara yake ilitaka kuwasingizia kuwa ni wala rushwa? Je wabunge wetu si wala rushwa wanaopitisha bajeti za hovyo baada ya kupewa chochote kitu? Wapo wanaoona kama hali ni hii tumekwisha na bunge hatuna bali klabu ya wala rushwa. Wako wapi wabunge wa upinzani?
No comments:
Post a Comment