The Chant of Savant

Monday 8 August 2011

Wajua nchi ambako wananawake wanasifika kuwabaka wanaume?

Taarifa zilizokaririwa na vyombo mbali mbali vya habari zinadai kuwa kuna jinai ya kubaka wanaume iliyoibuka nchini Zimbabwe hivi karibuni. Kawaida hata kisheria ni kwamba mwanamke huwa habaki. Lakini kadri siku zinavyokwenda ni kwamba tunapaswa kubadili sheria na imani hii. Maana nchini Zimbabwe kumeripotiwa wanawake kuwabaka wanaume tena si kwa kuwategeshea vishawishi bali mtutu wa bunduki.
Kwa wenzangu wanasheria watasema mwanamke hawezi kubaka kwa vile hana uwezo wa kusababisha erection. Kwa ufupi tunarejeshwa kwenye kuchunguza tena uwezo wa ubongo wa binadamu hasa anaposhikiwa mtutu wa bunduki. Hata hivyo, wengi wataendelea kuhoji inawezekanaje kusimama wakati umeonyeshwa mtutu wa bunduki? Au ni yale yale ya kumsukuma mlevi?
Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA

No comments: