The Chant of Savant

Monday 1 August 2011

Habel Kifoto hatunaye tena


Kwa wale wapenzi wa zilizopendwa watakuwa wanamfahamu nguli wa muziki wa dansi marehemu Habel Kifoto wa Kenya. Kifoto alikuwa kiongozi wa bendi ya jeshi la Kenya ya Maroon Comandos kwa muda mrefu kabla ya kustaafu jeshini na kurejea kwao Utaitani alikoishi maisha ya kawaida.
Hakika Kifoto alisifika kwa wimbo wake wa Charonyi ni Wasi ambao uliifungulia bendi yake milango ya mafanikio kwa miongo mingi.
Kifoto alifariki juzi jijini Nairobi alikokuwa amekwenda kikazi. Kwa habari zaidi bonyeza hapa.

No comments: