How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Monday, 2 September 2013

Hebu angalia MPigs wenu wa viti maalum wanavyousaka ubunge kwa wizi na rushwa

Msomaji hebu angalia madudu haya ya wizi wa mchana unaofanywa na anayeitwa mheshimiwa wakati ni mwizi tu wa kawaida. Mbunge wa viti maalum Catherine Magige anatuhumiwa na kukiri kujipatia pesa kwa ajili ya kuwahonga wapiga kura ili wamchague kwenye uchaguzi ujao. Hii ni EPA ndogo ambapo pesa na dhamana ya umma inatumika kutafutia pesa ya kuusaka ubunge. Mchezo wa wabunge hasa wa kuteuliwa kuunda taasisi umeshika kasi kumbe ni janja na njia ya kuchumia pesa kwa ajili ya malengo machafu ya kisiasa. Kwa mbunge kama huyu anayejiuza kwenye makampuni na taasisi za umma akisaka ngawira anaweza kumwakilisha mlalahoi wa kawaida au kuutumia ubunge wake kujiunza kwa wawekezaji na kuwauza watanzania? Je kwa zao la viongozi kama hawa tutafika kweli? Je nini kifanyike kuepuka balaa hili la kitaifa? Tafakarini kwa makini. Maana nyinyi ndugu zenu hata vizazi vyenu ndiyo waathirika na waadhirika wakuu. Kituko: Hebu angalia hicho kiingereza cha refereed to badala ya referred to na kingine cha kubukanya. Si muende shule badala ya kujifanya mnapenda elimu wakati mnaikwepa? Kama unawapenda sana wanafunzi si usomee ualimu badala ya kutuibia kodi yetu huko bungeni ambako nako huna kazi zaidi ya kufukuzia posho ya makalio dada.


4 comments:

Anonymous said...

Mwl. Mhango, kwani hawa wahuni wa "vigoda maalum" huwa wanapigiwa kura na wananchi au inakuwaje? Ni nini zaidi "u-maalum" wao? Hiyo ni mosi.

Pili, mbona mambo yote haya yaliyoorodheshwa kama madhumuni ya NGO / NPO hii yana wizara husika? Au ndiyo mwendelezo wa WAMA huu nao?

Iwapo hiyo inaruhusiwa, basi nami nitajiandaa kuunda NGO itakayoshughulikia ulinzi au Usalama wa Taifa. Ikiwezekana, ishughulike na mambo ya Ikulu kabisa.

Huu ni uhuni kabisa. Huyu kama ni mbunge kweli, angeeleweka sana iwapo mambo anayoyaendesha kwenye NGO hii angeyapigia chapuo zaidi kule Dodoma ili mawaziri wanaohusika nayo wachukue hatua kwa kuwa wanalipwa kodi za waTanzania kwa majukumu haya.

Na ifike siku nchi yetu iachane na mambo ya hovyo hovyo hivi. Huu uhuni uhuni wa NGO umeanza lini? Mbona zamani tulisoma tu na nyenzo tulizokuwa nazo bila huu ujanja ujanja. Yaani utadhani hizi NGO ni "dini" au "mungu" mpya aliyeibuka kuwaletea "maendeleo" waTanzania.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon usinivunje mbavu. Eti ayashuhgulikie haya mambo ale polisi siyo? Kimsingi, hii ina aina mpya ya ufisadi kwa vihiyo walioko bungeni na hata nje. Ni aina mpya ya wizi uchwara wanayopeana wakubwa kutumaliza. Hukusikia yule mwanasheria mwizi aliyesaidia Richmonduli aitwaye Mwanaid Maajar akianzisha Maajar Foundation baada ya kuupata ubalozi ili imsaidie mumewe lau kupata pa kugangia njaa? Kama mke wa bosi wao anatumia WAMA kuwaibia wafadhili akijidai anawasidia akina mama wakati wanamsaidia kutengeneza fedha haraka unadhani hawa wadogo wataacha? Namlaumu Anna Tamaa Mkapa aliyeanzisha ujambazi huu huko ikulu. Inachekesha mtu anayeomba misaada eti naye kutoa msaada. Mfugwaji hafugi mbwa. Kwa ufupi hii ni aina nyingine ya ufisadi wa kimfumo. Hapa utakuta kuna kigogo mmoja kavuliwa chupi na kulazimisha mamlaka hiyo imlipie hongo yake kwa ngono aliyopewa.

Anonymous said...

Ndo sitaki wala sipendi wabunge wa viti maalum
Wengi wao ni nyumba ndogo na wanakera kwa umalaya kuiba waume za watu. Kila mtu ana NGO yake . Lakini yote haya Kwani Tanzania haiwezi bila misaada ya mafisadi

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon 18:20 umenena vyema. Naamini walengwa watakusoma na kufikiri na kuamua kuondokana na aibu na shutuma hizo toka kwa jamii. Je watakoma ushankupe na tamaa ya fedha hata kwa kujifedhehesha? Siku hizi wanasema ujanja kupata hata kama mhusika anashikishwa ukuta. Uchangu wa kisiasa unalipa au siyo? Hata hivyo ni aibu hata kama watajiona wajanja kwa vile wanapata mifweza.