How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Wednesday, 6 August 2014

Kijiwe chapanga kutafuna njuluku ya Luwasha


 
          Mbwamwitu anaingia kijiweni akiwa na furaha si kawaida. Anasalimia na kukaa chini huku akiagiza kahawa. Kabla y ahata kueleza chanzo cha furaha yake Mgosi Machungi anamuuliza, “Mgosi inaoneka leo umeangukia. Maana naona una furaha sina mfano. Kulikoni ndugu yangu?”
“Mwenzenu nimeangukia kweli. Si katika pitapita yangu nikatonywa na rafiki yangu wa intelligence kuwa kuna mpango wa kupiga njuluku kibao toka kwa fisadi mmoja anayetaka kuwania urais,” anajibu Mbwamwitu huku akibwia kahawa yake.
Kabla ya kuendelea, Mpemba anachomekea, “Hilo ndilo lafanya ufurahi kana kwamba ushapata hiyo njuluku?”
“Tuliza bori mshirika. Hii njuluku hata kama sijaidaka ni sawa na nimeidaka,” anajibu Mbwa Mwitu huku akisugua mikono yake pamoja.
“Hebu basi tieezee utakavyopiga hii njuuku nasi tupige au vipi?” anachomekea Mgosi huku akibomu kipisi cha sigara kali toka kwa mzee Maneno.
Mbwamwitu akiwa anatabasamu anasema, “Mna habari kuwa kuna chama kimeanzishwa kinaitwa Alliance of Conmen and Traitors kifupi ACT?”
Mijjinga aliyekuwa anabuku novo yake iitwayo, The Beginning of the End anakwanyua mic, “Mbwamwitu acha utani. Hii ACT siyo ile ya akina Mzito Kabwela na Mfuatamkubo Kitila na Sam Mwigambo inayosemakana kuanzishwa na kudhaminiwa na fisadi Eddie Ewassa Luwassa wa Richmonduli ili kudhoofisha CHAKUDEMA na kushinda urais kwa kutumia tiketi ya Chama Cha Mafisadi (CCM)?”
“Marhabaaaaa. Umepatia sana mshirika.” Anajibu Mbwamwitu.
Kapnde aliyekuwa akitafuta upenyo anachomekea, “Sasa hii ACT ya Conmen na ya Mzito na Ewassa vinahusianaje?”
Mbwamwitu anajibu, “Kwani tumbili na nyani wana tofauti gani zaidi ya majina? Kumbe hamjui! Dili liko hivi. Nina mpango wa kwenda ofisi za CHAKUDEMA leo kukata kadi. Nikishamaliza nakwenda kwa vijana wa Mzito na kuwaonyesha ile kadi kisha wananikatia change nawaacha solemba au vipi?”
“Kweli wewe kichwa ndugu yangu. Nadhani wote hapa lazima tuingie kwenye dili hili la kupiga njuluku ghafla bin vu na kuwaacha mafisadi na makahaba wa kisiasa Solemba au vipi?” anajibu Mipawa huku akigonganisha mkono na Mbwamwitu anayetabasamu kama hana akili nzuri.l
Msomi aliyekuwa akisikiliza kwa mshangao anaamua kutia guu, “Mpango huu unaingia akilini. Hata nami nauunga mkono ikiwa ni njia mojawapo ya kupata mshiko na kuzuia hujuma kwa demokrasia. Hivyo, mpango huu una baraka zangu.”
Bi Sofia Lion aka Kanungaembe aliyekuwa amefura utadhani anapasuka anaamua kukamua mic, “Hata nawe msomi mzima unaunga mkono ujinga na utapeli kama huu! Kweli tunakwenda pabaya.”
Kapende hamkawizi, “Inakuwaje wasomi wa CCM na makahaba wa kisiasa kama Mzito wakisuka misheni za uhujumu kama hizi mnaziunga mkono lakini wasomi tukipanga kuwahujumu au kuwakaanga kwa mafuta yao mnalalamika na kutuona si wasomi Sofi? Umeingiliwa na nini dada yangu mbona huko nyuma hukuwa hivyo?”
Bwege aliyekuwa akisoma gazeti anaamua kutia timu kinamna, “Nadhani ni ubwege wa kutupwa kuwatetea mafisi, mafisadi na vyandoa wa kisiasa wanaotaka kuhumu demokrasia ambayo kimsingi ndiyo ukombozi wetu walalapuu. Hivyo, Profesa Msomi hajakosea kama anavyodhani da Sofi.”
Kanji kuona mshirika wake amebanwa anaamua kuingilia kati, “Somi napaswa fanya vitu ya haki. Kama Somi naunga kono pango hii ya juluku ya Luwassa nakosea sana na hapana itwa somi tena.”
Msomi hamkawizi, “Kanji mbona unaongea bila marejeo. Hivi wale magabacholi waliotupa miili na viungo vya dugu yetu Afrika siyo somi kama mimi?”
Kanji hakubali. Anaamua kujitetea, “Sasa ile hindi natupa ungo na juluku vapi na vapi somi dugu yangu? Ile iko kesi tofauti.”
Msomi anakwanyua mic bila kungoja Kanji amalize, “Kanji umeongelea usomi. Nimekupa mfano wa hivi karibuni wa kibaguzi na kishenzi ambapo wabaguzi wenzio wametudhalilisha tena katika kaya yetu. Wana bahati. Kama siyo kutetewa na vyangudoa wa kisiasa tungetoa mtu roho.”
“Mimi si baguzi Somi omba samaha yeye.”
Mpemba anachomekea, “Ama kweli nyani haoni nonihino lake. Kanji wakanusha wewe si mbaguzi? Kama hii jinai toke Bombay nafanywa na Swahili hindi hapana choma yeye moto hai.”
Kanji anajibu haraka, “Diyo mimi si baguzi. Sisi sote dugu  jamani.”
Mipawa anauliza, “Hivi Kanji unaweza kunionyesha hindi naona Swahili?”
Mbwamwitu anachomekea, “Huenda akina Kanji wanaolea Swahili kizani jumbani yao wanakotumikisha na kubagua kama mbwa.”
Kanji kuona mashambulizi yamezidi anaamua kuondoka kijiweni akisingizia kuwa anakwenda fungua duka.
Kijiwe kinaendelea.
Msomi anakoleza mada, “Tuachane na hawa wabaguzi. Tupange jinsi ya kupiga njuluku na kuzuia hujuma kisiasa. Lazima twende Kinondoni kwenye ofisi za CHAKUDEMA na kuwaeleza mpango wetu na kuchukua kadi ili kuwapiga hawa mafisadi akina Luwassa na Mzito Kabwela wakome.”
Baada ya Msomi kumaliza wanakijiwe wote isipokuwa bi Sofi na Kanji tulikwenda zetu kituoni kupanda ngwala ngwala kwenda kuchukua kadi tayari kuwaliza hawa wapuuzi wanaodhani wanakaya wote ni majuha kama wao.
Chanzo: Tanzania Daima Augosti 6, 2014.

2 comments:

Anonymous said...

Biashara ikulu, ipi hiyo mtujulishe!! Walevi tufungue Bar na Kitchen Party pale ikulu vikao vya harusi kila siku ahu vipi walevi wenzangu tutatoka sana tuu..!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon unauliza biashara gani ikulu wakati ni kuwachuuza nyinyi wenyewe? Sipati picha mafisadi wanaotumia fedha kuwanunua walevi wakiingia kule kama hawatarejesha utumwa kama huu wanaowafanyia twiga na wanyama wengine hai wanakopelekwa Arabuni.