How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Friday, 15 August 2014

Kuna uhusiano kati ya CCM na "wana Diaspora?"


Hivi karibuni kuliripotiwa kufanyika kongomano la Wana Diaspora la kwanza nchini Tanzania kwenye hoteli ya Serana jijini Dar. Ni jambo zuri kwa taifa kuanza kuona mchango wa wana Diaspora. Hata hivyo kuna tatizo. Je hao wanaoitwa wana Diaspora wanaowawakilisha wenzao walichaguliwa vipi na lini na kwa utaratibu upi? ukichunguza kwa makini kuna uwezekano kujenga dhana kuwa hao wana Diaspora wanaweza kuwa watu wa CCM. Maana wengine hatujui hata walivyochaguana na kutaarifiana kuhusu hilo kongamano. Hata hivyo, wengine hatujutii kwa vile halina lolote la maana linaloonekana kushughulikia maslahi ya diaspora. CCM ingeacha watu watumie fursa zao badala ya kupenyeza mapandikizi na nyemelezi wao kila kona. Mimi ni mwana diaspora lakini sijui lolote kuhusiana na hilo kongomano na jinsi wanaoitwa viongozi wake walivyopatikana. Nyumba yangu inao wana diaspora nane. Hii si namba ndogo.

5 comments:

Anonymous said...

WANA LAO HAO NA CCM

Anonymous said...

OOPS PASI YA TANZANIA INANUKA DUNIA NZIMA KWA SEMBE URAIA PACHA YANGU MACHO
BONGO KILA KITUN KINAWEZEKANA KWANINI MNATAKA URAIA PACHA BONGO PESA YAKO TUUUUUUUUUUUUUUU

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon mna hoja. Kwanini wasiseme wazi kuwa ni Diaspora ya CCM na si watanzania wote?

Anonymous said...

Diaspora ni nini? Kwa nini mkutano unafanya Tnzania badala ya walipo wahusika!?

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon swali lako ni la msingi sana. Huenda siku hizi diaspora wanaishi Tanzania. Who knows? Yaani kama si zengwe la CCM Kikwete na Pinda wamepata wapi muda wa kuhudhuria? Again, they are fooling themselves.,