How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Sunday, 17 February 2019

Hatimaye Dhuluma na Kashfa ya UDA yaanza kushughulikiwa-Kudos to Magufuli


Kwa wanaojua namna tapeli ajulikanaye kama Simon Kisena akitumiwa na wakubwa wenye madaraka alivyofanikiwa kuiiba na kuitwaa iliyokuwa Shirika la Usarifiri Dar Es Salaam (UDA), kunyakwa kwake sawa na ilivyokuwa kwa majambazi wa EPA, ESCROW na IPTL, ni  habari njema yenye kuhitaji kusherehekewa. Bado majambazi walioko nyuma ya ya wizi wa Radar na Ndege ya rais bila kusahau majambazi kama vile mzee wa Vijisenti na wenzake. Hapa tunapaswa kuendelea kumuunga mkono rais John Magufuli kwa kuzidi kuonyesha kuwa hana kujuana wala kuhurumiana. Wengi wallisema kuwa Kisena na wenzake wasingeshughulikiwa kwa vile ni wasukuma, kabila moja na rais Magufuli. Kosa, kwenye kupambana na ufisadi, Magufuli hana dini, kabila wala ndugu bali sheria na uadilifu. Tunatumai kuwa Kisena atawataja mabosi zake aliokuwa akisimamia mali na madhambi yao kwa kujitwalia UDA.

No comments: