How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Saturday, 29 February 2020
KATI YA KABWE NA MAALIM NANI ANAMDANGANYA NANI?
Kwa wanojua historia ya Zitto Kabwe kiongozi wa chama cha ADC na aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharriff Hamad na namna walivyoweza kuibuka na kuzunguka kisiasa kabla ya kufikia walipo, atakuwa anashangaa sana ndoa waliyofunga wawili hawa. Seif anasifika kwa kumnyang'anya chama chake marehemu James Mapalala na kukimilki kabla ya kupokwa na rafiki yake wa muda mrefu aliyegeuka kuwa hasidi wake mkuu Prof Ibrahim Lipumba. Zitto naye anakumbukwa alivyotaka kuja juu kwenye chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Kwa historia na malengo yao, wawili hawa ni wajanja hata schemers. Sina Kiswahili chake. Je umefika wakati wa Kabwe kupokwa chama au Maalim kuonyeshwa mlango kwa mara nyingine? je nani anamdanganya nani? Na nani atamzidi kete mwenzie?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment