The Chant of Savant

Wednesday 10 June 2020

Leo Nimemkumbuka Mwalimu Wangu Rweyemamu RIP

Upumzike kwa amani Mwalimu Chrysostom Rweyemamu | Jambo Leo

Wale waliobahatika kufanya kazi na Marehemu Chrysostom Rweyemamu pale Habari Corporation watakubaliana nasi kuwa huyu jamaa alikuwa mtu mwema. Mtaalamu wa tasnia ya habari, mcheshi, mnyenyekevu na asiyembagua mtu. Mwalimu Rweyemamu kama alivyojulikana, alikuwa mtu wa watu. Isingekuwa rahisi kujua nafasi yake bila kuambiwa. Ukikutana naye, huwezi kuamini kuwa ni yule unayesikia. Leo nimemkumbuka hata kama kimwili hayuko nasi. Pia namkumbuka Marehemu Fransis Semwaiko Mungu ailaze pema mahali pema peponi, kaka yangu na kiongozi wangu Hilal K. Sued, Francis Chirwa na wengine wengi kama vile akina John Bwire jamaa mmoja poa sana, Johnson Mbwambo hakujulikana kama alikuwa ndege au mnyama,  Ansbert Ngurumo ambaye tulipishana akiachishwa mie nikianza, Said Kubenea mwandishi mdogo ambaye hakuwa na weledi wala sifa, Jabir Idris, marehemu Mayage S. Mayage,  dogo Ezekiel Kamwaga, Jostam so and so nimesahau ubin wake, Pendo Mashulano, Marehemu Godfrey Dilunga, Badra Masoud, Mwandosya Mfanga, Marehemu C. Stanley Kamana, Casian Malima,  Brothers Edgar Kasumuni, Iman Mani, Rodney Thadeus, Halima Dendego aliyekuja kuwa mkuu wa mkoa wa Mtwara na wengine wengi ambao nimewasahau. Kwa unyonge nawakumbuka mabosi waliojisifu na kupuuza wadogo kama vile Gideon Shoo ambaye hata udaktari wake sijui kaupataje, Salva Rweyemamu mjivuni wa kunuka. Kwa namna ya pekee namkumbuka Mzee Jenerali Ulimwengu, kiongozi mahiri na asiyejisifu.

No comments: