Leo, tutaongelea baadhi ya mila za ufungaji ndoa katika baadhi ya jamii za sasa na za zamani duniani. Huko Usikochi, marafiki huwapaka rangi nyeusi iliyochanganywa na masizi, manyoya, maziwa yaliyochacha, na unga, hasa bwana harusi na wakati mwingine bibi harusi. Hii huwaandaa kwa ugumu maishani na hii hufanyika hadharani.
Huko Uchina, katika jamii ya Watujia, bi harusi hupaswa kulia kwa saa moja kwa mwezi mzima akiwa kwa wazazi wake. Baadae, bibi na dada zake humsaidia katika kulia kama namna ya shukrani. Nako Kongo, kwa kipindi kizima cha harusi, watarajiwa hawapaswi kucheka bali kununa! Nako nchini India, wanawake waliozaliwa kwenye hali fulani za kinyota waitwao Manglik dosha huolewa na mti, hasa mgomba, ambao baadae hukatwa ili kuondoa laana.
Nako Korea ya Kusini, bwana harusi hufungwa kifundo cha mguu na kuchapwa na samaki makanyagioni kuthibitisha ushupavu wake kitabia. Nchini Ujerumani, kwenye mkesha wa ndoa, vifaa vyote vya udongo huvunjwa na watarajiwa husafisha kila kitu kumaanisha umoja katika kutatua matatizo. Katika tukio hili, ni mwiko kuvunja glasi kwa vile huleta mkosi.
Kwa wamasai, baba humtemea mate bintiye mtarajiwa kwenye kichwa na kifua kama ishara ya baraka. Baada ya hapo, bi harusi huondoka bila kutazama nyuma ili asivuruge bahati yake. Nako Indonesia kwenye jimbo la Java, bi harusi huoshwa na nduguze wazee kwa maji yaliyotiwa maua kama ishara ya kutakaswa. Huko Uswidi, waalikwa hawafichi furaha yao. Bwana harusi akitoka kidogo, wageni wa kiume hupanga mstari kumbusu bi harusi sambamba na bi harusi akitoka wasichana na akina mama huenda kumbusu bwana harusi.
Huko Romania, marafiki wa bi harusi hutekwa na marafiki zake hadi wajadiliane namna ya kumrejesha. Hii hulenga kupima utashi na utayari wa bwana harusi kumrejesha. Nako nchini Ugiriki, rafiki wa bwana harusi hunyoa ndevu siku ya harusi kuonyesha uaminifu baina ya marafiki hawa. Baadae, ndugu wa familia humlisha asali na matunda ya mti wa mlozi. Hii, huashiria ndoa itakayofana.
Turejee tena Kaskazini mwa India. Kuna kitu kiitwacho Joota Chupai, ambapo ndugu wa bi harusi huiba kiatu cha bwana harusi pindi aingiapo nyumbani kuashiria ushindani na inaweza kuisha kwa kutoa dau kubwa.

Kule nchini Mongolia, kabla ya ndoa, lazima achinjwe kuku mchanga na kutolewa ini ili kupata ini lenye afya. Lisipopatikana, utaratibu huu utaendelea hadi lipatikane linalofaa.
Huko Chekoslovakia, ndugu na marafiki huweka kichanga kwenye kitanda cha watarajiwa kabla ya ndoa kuashiria ndoa itakuwa na watoto. Pia, mchele na nafaka husambazwa kitandani kuonyesha wingi wa neema. Kule Japan nako, kuna sherehe ya San-San-Kudo Sake au nilohunshu kinywaji kitokanacho na mchele uliochacha ambapo watarajiwa hawabadilishani pete. Badala yake, hunywa mara tisa, tatu tatu kila mara toka vikombe vitatu vya sake kuashiria kuwaunganisha watarajiwa na familia zao. Na hii huchukuliwa kama ishara iliyobarikiwa kuliko kula viapo.
Huko Afrika Magharibi, baadhi ya jamii ambazo bi harusi huwekwa kwenye vibanda maalumu na kulishwa na kunenepa ili kupata unene unaoridhisha. Kuna imani kuwa bi harusi wanene wanapendeza na wana uwezo wa kuzaa watoto wenye afya! Funga kazi ni kule Spartan huko Ugiriki. Bwana harusi hupigwa kwa fimbo na mawe ili kuonyesha uvimilivu na ustahimilivu katika maisha.
Kwenye mila za Waceltic kule Ulaya uhitaji kitanda cha maharusi kubarikiwa na makasisi wakati waliohudhuria sherehe wakiangalia. Sherehe uhusisha unyunyiziaji maji ya baraka kitandani. Unyunyiziaji maji huu ulidhaniwa kuwa ilikuwa ni alama ya ulinzi na uzazi kwa wanandoa. Warumi nao walikuwa na yao. Mabwana harusi waliwabeba bi harusi na kuwusha vizingiti maalumu kuepuka pepo wabaya kuwaingia kupitia miguuni. Warumi waliamini kuwa pepo wabaya ambao huishi ardhini na wanaweza kuingia kwa wanawake waingiapo kwenye nyumba mpya. Hivyo, kuwabeba kuliepusha wao kukutana na nguvu hiii ya ajabu.
Mwisho, wapo wayahudi. Hawa wangelinganisha watarajiwa na ndoa hufungwa kwa kutema mate ardhini kabla ya kupeana mikono. Wayahudi waliamini kwa mate yana nguvu ya kinga za kuweza kufukuza pepo wabaya.

Chanzo: Mwananchi Jpili 29 Machi, 2026.
No comments:
Post a Comment