Baada ya kufyautua kanywaji nako kakanifyatua nimefyatuka na kuja na uhalalishaji na urasmishaji sera mpya bab kubwa ya kuombaomba. Kwanza, nilishangaa kugundua kuwa vyura wanaweza kuomba maji ya kunywa ilhali wanaishi kisimani. Pili, kama haitoshi, nashangaa kuona Mafyatu wakiishi kwa kuombaomba karibu kila kitu na kila mtu. Wanamuomba Mungu usiku na mchana, hawatosheki! Wanawaomba wenzao hata kaya nyingine hawatosheki! Ajabu ya maajabu, ombaomba wakubwa wanawafyatua kwa kuwafukuza ombaomba wa vikopo ilhali wao wanaomba kwa mapipa! Ni ajabu haswa.
Ukienda kijijini kujulia hali Mafyatu, kila Fyatu anakuomba kitu au mkopo asipanga kurejesha. Mara, mchango wa birthday, harusi, kipaimara, ubarikio, wanene kuongeza misafara ya ndinga, , semina, upigaji, ziara za kilimbukeni, na upuuzi mwingine mwingi. Nikuchangie kuoa, kwani waniolea au ulinichangia nilipooa? Kwani, lazima kila kitu kisherehekewe ilhali majirani zenu wanafyatuliwa na ukapuku? Ni roho mbaya na ukumbaff kiasi gani?
Najua. Wengi watajifyatua ufahamu na kunishangaa hata kunilaumu wakati nami nawashangaa. Watanishangaa kwanini uombaomba iwe sera tena rasmi. Nifanye nini sasa iwapo naona maajabu Mafyatu kuomba wakati uchumi wanao ila wanaukalia na kujifyatua? Mie siyo mnafiki wala msanii. Nafyatua ukweli kama ulivyo. Ajabu ya maajabu, utakuta ombaomba mkubwa akimbeza, kumkebehi, kumkoga hata kumfukuza ombaomba mdogo!
Tukiacha ufyatu uchwara wa kutofyatuka kikamilifu, hivi, ombaomba wa kopo na ombaomba wa rushwa hata ya ngono, nani mbaya? Utashangaa zaidi ya kutamani ufyatuke na kufyatua unaposhuhudia mijizi mikubwa na mila rushwa ikijifyatua na kupokoma ikiwakoromea ombaomba wadogo iliyowatengeza walipogoma kufyatuka na kuwafyatua waache kuwafyatua kifala na kijambazi.
Heri ombaomba wa vijisenti kuliko wa mabilioni. Kwani, hatuwaoni wala kuwajua ombaomba wanene wanaoingia mikataba ya kijambazi hadi kuuza kaya yetu kwa wachukuaji wawaitao wawekaji ili kutufyatua? Ajabu nyingine, unakuta ombaomba akifuja na kufyatua njuluku za mafyatu tena kwa kujiamini na maringo. Ukifyatuka na kumkemea, anadai unatishia amani. Amani gani ya kufyatuana na kudhulumiana?
Tukifyatuka na kuwa wakweli, nani mbaya kati ya mla rushwa na ombaomba anayefyatuliwa na dhiki hadi aibu inamtoka hadi anaomba? Nani mbaya kati ya mafisi na mafisadi tena wanaoturingia mitaani wakati wanaishi kwa kufyatua jasho letu? Nyinyi Mafyatu wakumbaff, nani aliwaroga hadi mkadoma na kuogopa kufyatuka na kuwafyatua wanaowafyatua? Sasa mjue. Hata mmuombe Sir God vipi, bila kufyatuka mkawafyatua wanaowafyatua, mtafyatuliwa tu hadi mkome kama mkiendelea kugoma kufyatua au kujifyatua kwa kutofyatuka na kuwafyatua wawafyatuao mchana kweupe.
Kaya inachoma mabilioni kujenga bwandari halafu ombaomba na mafisadi wachache wanaigawa eti kukuza Uchumi! Uchumi gani huu ukuao kwa kugawa mali ambazo zingeukuza au ni kwa vile wengi wa wanaofanya hivyo hawakusomea uchumi zaidi ya uchumia tumbo na uombaomba? Kweli, mmejua kutufyatua na kututenza kama mataahira au vipofu wasioweza kufyatuka na kufikiri au kuona makufuru mfyatuayo tena kwa kujisifu eti mnaleta maendeleo. Maendeleo au ni maendeleo katika kutoendelea?
Uombaomba umegeuza Mafyatu chawa na funza walao wasichopanda wala kupanda chochote zaidi ya maangamizi yake na wenzao.

Heri hayawani chawa kwani, hayo ndiyo majaliwa na maumbile yao. Mafyatu wana akili, mikono, nguvu, na ubongo lakini hawavitumii vilivyo. Mie kama doktari wa uchumi na utawala, lazima nifyatuke na kuzoza bila aibu wala woga. Tunakera sana sana. Tunaudhi hadi kuudhika inakuwa sehemu ya maisha. Si tufyatuke na kubadilika japo kidogo. Ili kutenda haki na kutoa fursa kwa wote, kuanzia leo, katika Fyatuland, kuomba, kupiga, na kufyatua Mafyatu waliogoma kufyatuka wakawafyatua wawafyatuao ruksa. Rasmi, Fyatu nahalalisha na kurasmisha haya mambo ili tuache kufungana kamba kuwa tunatendeana haki wakati wachache wanakula na kushiba migongoni nwa walio wengi wanaofyatuliwa na maradhi, shida, umaskini na uzwazwa tena vya kujitakia. Sina haja ya kuwafyatua kwa kuwataka wakaze mikanda wakati wangu nimefungua ili kufyatua zaidi na zaidi. Umeona?
Naona yule anajifyatua na kutikisa kichwa kwa hasira. Huna haja ya kufanya hivyo. Natania tu. Nimesemaje? Kula pini basi Fyatu wangu unayenisoma. I’m just jokin’ kwa Kisambaa kkk!

Juzi, nilipita zangu town nikiwa kwenye mihangaiko na mihanjo yangu. Michuma niliyoona sikuamini kama Fyatuland ni kaya kapuku inayoweza kufurahia, kuridhika, na kutegemea kuomba ili kuishi. Unaombaje wakati ulichona unakigawa au kuruhusu wadudu wadogo wadogo wakinyevue? Waone wafyatuaji walivyonona kama nuni. Nani anauliza walivyonona wakati Mafyatu wanaondeana kwa kufyatuliwa na hawa wanonao kama nune?
Ajabu ya maajabu, utawaona wakiingia kwenye nyumba za Sir God. Humo namo, wenye magwanda wanawafyatua waumini makapuku kwa kisingizio cha kumtolea Sir God! Nani kawadanganya kuwa Sir God ni kapuku hadi ategemee madafu ya makapuku kama siyo uzwazwa na ukosefu wa ufyatu wa kufyatua japo hoja na maswali? Si mmaaminshwa kuwa Sir God ana uwezo wa kila kitu? Kwanini wale wanaojifanya watumikiaji wake wawategemee nyinyi ilhali Sir God yupo na ukwasi wake? Nani anautumia huo ukwasi tuaminishwao anao kama kweli ni kweli?
Chanzo: Mwananchi J'tano leo.
No comments:
Post a Comment