The Curse of Salvation

The Curse of Salvation

Saturday, 18 July 2015

Urahis: Nusu Mlevi kudedi!

 Baada ya kuangukia pua na kutoka patupu kwenye mbio na harakati za kutia nia ya kusaka urahis, Mlevi nimejikuta kwenye matatizo usipime. Kwani wakati nikitia timu nilitegemea kuwa umaarufu wangu na kutembeza njuluku vingenijenga asijue vingenibomoa. Sasa nipo najuta na kuangua kilio kama Kanji baada ya kupata hasara. Ndoto imeyeyuka hata la kushika na kufanya sijui. Nilichodhani kilikuwa ndoto kumbe kilikuwa jinamizi ambalo sasa limegeuka msalaba mwinge shingoni mwangu. Hata Bi Mkubwa anaishia kunipa karata sorry talaka baada ya kuukosa u-First Rider. Alikamia kuunda bonge la NGO ili achange njuluku kama hana akili nzuri. Marafiki zangu walionizunguka zama za kuusaka urahis wote wamenikimbia na kujiunga na mtarajiwa. Ama kweli sikujua kuwa binadamu wakati mwingine ni wajalaana usipime. Bi mkubwa naye usipime. Naye presha imempanda hadi anazimiazimia kama kisimu cha mchina kwa kuukosa u-first-raider ambao licha ya kumtajirisha ungewatajirisha pia ndugu zake hasa usawa huu ambapo urahis umegeuka enterprise ya kutengeneza njuluku haraka na kwa mazabe bila kunyea debe.
Hivi ninavyoandika nimebaki na mshirika mmoja yaani daktari wangu ambaye amenionya nipunguzi mawazo vinginevyo presha inaweza kuninyotoa roho wakati wowote. Kwani daktari wangu ana wasi wasi sana nami. Anasema presha yangu iko juu kuliko wakati wowote.
Hakuna kinachoniuma na kuniumiza kama kuona washikaji na wapambe zangu wakinigeuka. Njuluku wamekula na sasa hawaniabudii tena. Wamenitelekeza huku wakinionyesha wazi watakwenda kuwapa tafu wabaya wangu.
Kwa hasira na uchungu nimeamua kuvunja kambi. Maana haikuwa kambi kitu bali kamba ya kulia njuluku zangu huku wahusika wakiniegeuza juha na hamnazo kwa kunipa ushauri ulilenga kuwanufaisha wao wakati nikijikaanga mwenyewe kwa mafuta yangu kama ngisi.
Hata jamaa zangu wa magazeti ndiyo usiseme. Walizoea kunizonga kila uchao ukiachia mbali kunibeep na kunitoa mshiko ili waniandike vizuri. Sasa nimeangukia pua hawataki hata kusikia habari zangu achilia mbali kuniona. Kila nikiwapigia simu hawapokei. Wananidengulia anajua Mungu mwenyewe. Zama za mchakato nilifanya kosa moja kubwa. Kwani nilijigamba na kuwa karibu nao nikidhani walikuwa marafiki wa kweli kumbe siyo. Wale niliodhani urafiki wetu haukuwa wa barabarani waliishia kunitosa na kuniacha nikihangaika barabarani hata wasione aibu wala kunionea huruma. Ama kweli siasa ni nchezo nchafu kweli kweli. Nani alitegemea kuwa mshirika wangu kama Njaa Kaya angenichunia na kutumika kama kiongozi wa kunishambulia na kuwahimiza wajumbe wasinipe kura za kula? Leo hii namuona akiwa beneti na Joni  Kanywaji Makufuli wakiangusha vicheko wakati mimi nikiangusha kilio. Hanipigii hata simu kunijulia hali pamoja na kujua kuwa presha yangu na ya Bi Mkubwa zimepanda. Ama kweli penye riziki hapakosi hiana!
Sikujua kuwa wengi walinichukia hadi yaliponikuta. Waliokuwa wakiniita rahis mtarajiwa na mheshimiwa wote wametoweka. Kumbe walikuwa wakinisanifu na kuniingiza mkenge ili wale vyangu halafu waniache Solemba!
Huwezi kuamini kuwa umati niliokuwa nikipata wakati nikisaka wadhani ulikuwa ni wa wabaya wangu walionisanifu na kuniingiza mkenge ili wale njuluku zangu. Nani anaweza kuamini kuwa hata yaliponikuta ya kunikuta wa walishindwa hata kuja kuvunja tanga baada ya msiba huu mzito wa kisiasa?
Hata hivyo, nao wana bahati tena ya mtende. Maana nilivyokuwa nimepanga kuwatumia kama daraja kufikia ulaji kama ningetoboa wangekoma waishie kulia na kusaga meno. Hata hivyo, sikujua kuwa tulikuwa tukicheza mchezo wa karata tatu. Kwa lugha nyingine tulikuwa tukitumiana na kutapeliana huku kila mtu akivutia upande wake. Sikujua kuwa siasa wakati mwingine ni kama ukahaba. Hakuna aliyeniongezea presha kama habithi mmoja kati ya waliokula njuluku zangu. Maana, nilipomtwangia simu kuja tupange jinsi ya kutoka alinitolea nyodo kuwa nisihangaike bure kulilia njuluku zangu zilizoliwa kwa vile nilizichuma kifisadi, kirushwa na kiwizi. Nilipomtaka athibitishe kwa kuleta ushahidi alikata simu na kuniacha nikikosa pumzi.
Nawashauri wenzangu wenye ndoto za Alinacha za kuwa marahis kama mimi wafikirie mara mbili. Heri kufanya mambo kimya kimya kama alivyofanya John Kanywaji Makufuli kuliko kujilisha pepo kwa kuwakaribisha wapembe nuksi na walaji ambao watakuacha pakanga unapoangukia pua kama mimi.
Kwa sasa nikiangalia umri ndiyo umenipiga chenga huku udhu ukiota mbawa. Sijui nitafanya nini ili lau nirejeshe nusu ya mshiko niliopoteza kwenye ndoto uchwara za kuula nikaishia kuliwa? Nadhani kwa sasa lazima nami nijigonge kwa Joni Kanywaji Makufuli ili akipata utukufu wake lau anipe kibarua ukiachia mbali kunyamazia mazabe yangu. Maana juhudi zangu za kuusaka urahis, licha ya kutaka kula kwa dezo kwa mikono na miguu huku nikipiga mbizi kwenye sinia, ilikuwa ni kujihakikisha usalama kwa mustakabali wangu hasa ikizingatiwa maskandali ya wizi wa njuluku za walevi unaoninyemelea tangu zama za Nchonga.
Kwa vile nimeishazoea kubwagwa, lazima nirejee kwa walevi wangu lao nigombee uishiwa niendelee kuwa kwenye gem.
Nimalizie kwa kuwaomba wale wote wenye mapenzi nami lau kuja kunijulia hali hasa wakizingatia kuwa hakuna anayeweza kukataa au kutohangaikia ulaji rahis na wa dezo kama urahis. Hivyo, wasinitenge na kuniona kama ukoma wakati walikula vyangu. Nawashauri walevi waache mchezo wa kuwashawishi wanasiasa kutumia njuluku kuwanunulia kila upuuzi kuanzia kanywaji bangi vibandiko na kanga kwani wanawapa wengi motisha kuwaliza japo nao wanaweza kulizwa kama mimi.
Tukutane wiki ijayo. Pombe kwa urahis, pombe kwa walevi makufuli kwa mafisadi. Kanywaji hoyee! Kanywaji na Makufuli hoyeee!
Chanzo: Nipashe Julai 17, 2015.

Friday, 17 July 2015

Kikwete na nembo ya ajabu ajabu

Picha kwa hisani ya ippmedia

Zitto, mabilioni ya Uswisi na Yeremia 5:21: Makala hii imenichanganya

 KUNA wakati, Mwenyezi Mungu ametumia lugha inayoweza kuonekana kali kupitia maandiko yake matakatifu. Kwa mfano, kitabu cha Yeremia 5:21 alisema; “Sikilizeni neno hili, enyi watu wajinga msio na ufahamu, mlio na macho ila hamuoni, mlio na masikio ila hamsikii”. Binadamu hawana ugeni kwa Mungu, anawajua! Unaweza kuwawashia taa na wakalalamika wapo gizani. Ukiwapa chakula, watakula na kusaza lakini baadaye watalalamika wamepunjwa au hawajala kabisa. Wape maji, kiu zikiwaisha watayatoa kasoro maji yako, ama kwa baridi, moto au vyovyote vile! Ndiyo sababu amesema nao kwa ukali. Mwenye macho anaweza kujifanya kipofu asiyeona kuliko mlemavu mwenyewe. Aliye na masikio yake timamu, atajidai hasikii. Akiamua asione wala kusikia, hata utumie picha na sauti gani, atakwambia hasikii wala haoni. Haina tofauti na ule msemo wa Kiswahili “Akutukanaye hakuchagulii tusi”, kwamba lolote linalokuja mbele yake atalitoa ilimradi litamkera au kumvunja moyo anayemkusudia. Kwa kawaida asiyekupenda hana jema na wewe. Utafanya kubwa litakataliwa au kushushwa thamani. Upepo unapokuwa mzuri, kwa wanaokupenda, hata waambiwe lipi baya hawataamini. Watakataa kila ovu utakalotupiwa na litatukuzwa kila zuri ambalo litaelekezwa kwako. Katika Uchaguzi Mkuu wa Liberia mwaka 1997, Waliberia, hususan vijana, walionywa kuhusu Charles Taylor, aliyekuwa anawania Urais wa nchi hiyo, baada ya vita vya kiraia. Wachambuzi wa mambo walionya kuwa Taylor ni mtu hatari, aliyesababisha nchi kuingia vitani na hata vifo. Vijana walikumbushwa kwamba wengi wao walipoteza wazazi wao kwa sababu ya vita iliyochochewa na uroho wa madaraka wa Taylor. Vijana hawakuambiwa kitu, ndiyo kwanza waliimba mitaani kauli mbiu ya “alimuua mama, alimuua baba, lakini nitamchagua…” (he killed my ma, he killed my pa, but I will vote for him). Ni ile ile dhana ya kuwa na macho lakini unajifanya huoni. Umepewa masikio hai lakini kwa makusudi eti husikii. Taylor alishinda urais kwa zaidi ya asilimia 75, ikiwa ni ushindi wenye upinzani dhaifu. Hata hivyo, yaliyotokea baadaye kila Mliberia alijuta. Walipopigana vita ya pili ya wenyewe kwa wenyewe, walijutia uamuzi wa kutoona na kutosikia kila baya lililosemwa kuhusu Taylor. Julai 4, mwaka huu, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, alifanya mkutano mkubwa wa hadhara kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, kwa ajili ya kukitambulisha chama chake kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam. Katika mkutano huo, alitoa majina 99 ya Watanzania wenye akaunti kwenye Benki ya HSBC, Uswisi. Kwa mujibu wa Zitto, orodha hiyo imepatikana kwenye tawi moja tu katika benki hiyo. Maana yake ni kwamba pengine matawi mengine ya benki hiyo kuna majina mengine ya Watanzania ambao wameficha fedha zao. Kwanza; alichokisema Zitto hakikuwa hukumu kwamba majina yale 99 ndiyo hasa walioficha fedha haramu Uswisi. Alichosema ni kuwa kuyaweka kwake wazi majina hayo ni njia mojawapo ya kuichokoza serikali ili iweke mkazo wa uchunguzi. Pili; hotuba ya Zitto ilikuwa wazi kuwa Watanzania walioficha fedha nje ya nchi ni wengi na mataifa yanayohusika na ufichwaji wa fedha za Watanzania ni mengi. Kama uchunguzi utafanyika yapo mengi yenye faida yanaweza kujulikana. Kwa vyovyote vile, uhifadhi wa fedha nje ya nchi, hata kama ni halali, una madhara kiuchumi kwa nchi. Mfanyabiashara anayeweka fedha zake nje, maana yake zinaingia kwenye mzunguko wa kibiashara kwa benki ya nchi husika ambayo inanufaika kwa kukata kodi na makato mengine. Hivyo, kama fedha hizo zingehifadhiwa Tanzania, taifa lingefaidika kibiashara na kikodi. Kwa msingi ulio wazi ni kwamba yeyote ambaye anaishi Tanzania na kufanya shughuli zake ndani ya nchi kisha kutunza fedha zake nje, huyo ni msaliti kwa nchi. Hili lingeweza kuonwa haraka kisha Zitto angepewa pongezi zake. Kilichotokea badala yake ni Zitto kushambuliwa. Hoja kubwa ikihusu asili ya majina yaliyomo kwenye orodha iliyotolewa na Zitto. Kwamba mbona wote ni kama wana asili ya Bara la Asia? Wanasahau kuwa upo uhuni wa kutumia majina ya watu, kwamba mtu fulani kwa kutambua kuwa ikigundulika amehifadhi fedha kwenye akaunti ya nje ya nchi lazima atiliwe shaka, ataamua kutumia akaunti ya mtu mwingine ili kupata kivuli cha uchafu wake. Hapahapa nchini, inajulikana kuna watu wanaoitwa vigogo serikalini, wanamiliki makampuni ambayo majina ya wamiliki ni ya wengine kabisa. Mkurugenzi wa shirika la umma anaidhinisha zabuni kwa kampuni ambayo yeye ndiye mmiliki lakini ukienda kukagua majina yanayotambulika kama wamiliki huwezi kumkuta. Kama hayo yangetazamwa, Zitto asingezodolewa. Ingeshtua mjadala mkubwa sana wa kitaifa. Jina moja baada ya lingine lingepitiwa kujua anafanyaje biashara zake nchini, analipaje kodi na washirika wake wa kibiashara ni akina nani. Hatuwezi kufika huko kwa sababu kuna tabaka la watu ambao walishaamua kuwa ‘anti-Zitto’, yaani wapinga Zitto kwa jema kwa baya. Hao ndiyo wale ambao inyeshe mvua, liwake jua hawakubaliani na Zitto, imekuwa rahisi zaidi kwao kupaza sauti na kutamka, “alitafuta kiki.” Huyo anayesemwa anatafuta umaarufu, alishakuwa nao kitaifa, tena kwa kiwango kizuri, yapata miaka 10 sasa. Akutukanaye hakuchagulii tusi! Ilivyo ni kuwa Zitto angetaja majina ya wabantu, waliozoeleka kwa kashfa za ufisadi, bado angezodolewa. Yangetajwa majina ya wawania Urais 2015, angeambiwa amenunuliwa na ametumwa na makundi ya wagombea Urais. Ni yaleyale ya Yeremia 5:21, kuwa wana macho yao lakini hawaoni, na masikio wanayo ila wanagoma tu kusikia. Wataalam wa kupinga wanapokuwa kazini, thawabu wataita dhambi na dhambi itapambwa na kutukuzwa kwamba ni thawabu. Kama hatukukubali, baya lako tutalishangilia na uzuri wako tutaukataa. Hii ndiyo vita ambayo Zitto anakabiliana nayo. Bahati mbaya ni kuwa Zitto pengine hajui kwamba hawezi kuwa na jema la kuwafurahisha wanaompinga. Na ndiyo maana wakati mwingine anajaribu kuwalazimisha wamuelewe kwamba yeye ni mzuri kuliko wale waliotengeneza mpango wa kumpachika jina la msaliti au Yuda. Anawaambia “kwenye ilani ya kilichokuwa chama chetu, tulikubaliana tusichukue posho za vikao maana ni kuwanyonya wananchi, mimi peke yangu sikuchukua, wenzangu wote walisaliti na kuchukua posho, nani msaliti hapo?” Kwa sababu hawaoni wala kusikia kwa makusudi, jibu lao linabaki lilelile, msaliti ni Zitto. Anawaambia Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni anatumia gari la kifahari kinyume na matakwa ya ilani ya chama chake katika Uchaguzi 2010. Mwanzoni alilikataa kisha akazunguka nyuma ya pazia na kulichukua. Hapo ni nani msaliti? Wanamjibu msaliti ni Zitto! Unadhani ni kweli hawasikii na hawaoni? La hasha! Isipokuwa ni ule msemo wa “kipendacho roho hula nyama mbichi.” Yeye anayewaambia hayo hayo maneno hawampendi, wanaamini katika njia walizopitishwa kwamba ni msaliti, kwa hiyo hata aseme maneno yenye rangi gani za kupendeza hawatamkubali. Zaidi, huyo anayewashawishi wamuone ndiye msaliti, wao wanampenda sana. Ni mvurugano tu hapo, ni ile lugha gongana. Sikitiko langu siku hizi hata waandishi tunakuwa wacheza karata kama mawakili mahakamani. Mteja wake ameua na hilo analijua lakini anaamua kutengeneza njia za kumfanya mteja wake aponyoke na aonekane hana hatia ya kuua. Ni michezo tu, waandishi nasi tunaamua kuangalia habari, kuichekecha na kuiwasilisha katika sura inayompendeza na kambi yake. Kama mhusika ni kipenzi chake na habari ni mbaya, anaigeuza ionekane nzuri na kuiwasilisha. Na ikiwa ni nzuri kwa asiyempenda, anaichezea ili iwe na ladha mbaya kwa mhusika. Ni uleule mtindo wa wakili na mteja! Ni suala la muda tu, muhimu ni kwa Zitto kuendelea kufanya kazi nzuri, wakati ukifika watu watageuka. Kwa kawaida huhitaji muda na uvumilivu wa kutosha kumbadilisha aliye amini. Upo msemo wa Kiingereza; Who love too much, hate in the like extreme, kwamba anayependa sana ndiye huchukia kupita kiasi. Tuvute subira, muda utafika! Mwandishi wa makala haya, Luqman Maloto ni mwandishi wa habari na vitabu. Anapatikana kwa simu namba 0683 35 57 17 
Chanzo: Raia Mwema  Julai 15, 2015

Thursday, 16 July 2015

Heko Butiku na Warioba japo mnampigia mbuzi gitaa

Image result for photos of warioba and butiku
 Baada ya kung’atuka na hatimaye kuaga dunia kwa Mwl Julius Nyerere, walibaki viongozi wenye udhu wachache sana. Ni bahati mbaya hata wale aliowaamini akawabeba hadi kubezwa amebeba nyago la mpapure walimgeuka wakageuka mafisadi wa kunuka.
Hata hivyo, bado Tanzania ina watu wa kupigiwa mfano. Hawa si wengine bali wanafunzi wa kweli wa mwalimu Nyerere. Mmoja wa watu hawa ni Joseph Butiku ambaye pia ana uhusiano wa damu na Nyerere. Mzee huyu, licha ya kuwa muwazi na muadilifu, si mwoga na anapokuwa au kukerwa na jambo huwa hasiti kulisema.
Hivi kariubuni Butiku alikaririwa akisema, “Sasa tunatoka kwenye utaratibu wetu wa vyama tunashiriki katika kufanya uovu. Kama haki inauzwa, hatuwezi kupata amani. Viongozi wanatoa rushwa hata kabla ya kupewa nchi. Je, wakipewa nchi itakuwaje?”  Tofauti na wakongwe kama vile Kingunge Ngombale Mwiru, Butiku na wengine wachache kama vile Joseph Warioba ni wazee wachache unaoweza kuamini dhati na yale wayasemayo.
Wazee hawa wameshinda vishawishi na kuonyesha uzalendo wao wakati huu ambapo chama chao kinatafuta mtu wa kupeperusha bendera yake. Wamejitenga na ukuwadi uchwara na unepi ambao umewashinda wengi waliopwakia hongo hadi wazee wazima wakajivua nguo hadharani. Kwa lugha nyepesi ni kwamba Butiku analionya taifa kuwa kama halitajirekebisha likaendelea na ugunia wa kumeza kila kiingiacho litajikuta pabaya huko tuendako.
Butiku bila woga wala kumung’unya maneno alionyesha chanzo cha matatizo tunayoshuhudia ambapo watia nia wanatembeza hongo mchana kweupe bila kuchelea lolote. Alisema, “Mtandao huo iliamua kufanya kazi nje ya CCM kwa sababu itikadi zao na sisi zilitofautiana. Eti wanasema CCM ni chama cha mizengwe kinawachelewesha kutajirika. Sasa hao watu ndiyo wameendelea kuwapo na kusababisha haya matatizo yaendelee.” Butiku alikuwa akielezea uchafu ulioasisiwa na wasaka tonge hapo mwaka 1995 kiasi cha kuendelea kuitafuna CCM.
Butiku hakuwa peke yake kukemea uhovyo na uhalifu vinavyoanza kuonekana kama vitu halali na vya kawaida ndani ya CCM na serikali zake. Mzee Warioba naye aliongeza kwa akionyesha chanzo kingine kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani nchini. Alisema, “Tunakwenda katika uchaguzi lakini huku tukiwa na viashiria vya uvunjifu wa amani. Hivi nani hajui kuwa kuna rushwa kubwa katika uchaguzi.” Kwa mujibu wa Warioba ni kwamba kinachoendelea kwenye kutafuta atakayepeperusha bendera ya CCM ni rushwa tupu. Hii maana yake ni kwamba watanzania kama hawatajifanya kuwa mataahira wanapaswa kutomchagua mgombea wa chama kinachopata mgombea wake kwa rushwa na kuvunja kanuni walizojiwekea. Kama wanaweza kuwa wazembe kiasi cha kuvunja hata kanuni walizojiwekea, wakipata madaraka si watavunja sheria za nchi kama walivyofanya kwenye kuua katiba ya wananchi? Je watanzania wanataka washikwe wapi au watukanwe matusi gani au kuonyeshwa dalili gani wachukie na kuchukua hatua mujarabu? Je itakapotokea nchi ikaingia kwenye machafuko watamlaumu nani kama si kujilaumu wenyewe?
Watanzania wanapaswa kuzingatia wosia na maneno ya wakongwe hawa wa CCM. Kwani wanachosema ni ukweli ambao hauna shaka. Sasa kama wana CCM tena wakongwe wameishaona hatari na uhovo wa CCM kunaja gani ya wapiga kura kuendelea kuipa hadhi ya kupeleka nchi kuzimu? Nadhani ufisadi ambao CCM imeuasisi, kuusimamia na kuutekeleza vinatosha kuwafanya watanzania wachukie na kutoa hukumu yako ya haki.
Najua baada ya CCM kushikwa pabaya na wanachama wake wenyewe na kuishiwa, kwa sasa watakuja na mzengwe wa kusema fulani tuliyempitisha ni mtu safi. Well, well, mnaweza kuwa na mtu safi je chama ni safi?  Huko nyuma tuliwahi kuonya kuwa hata kama CCM wangemsimamisha malaika, mwisho wa siku watamchafua naye awe kama wao. Watambadili lakini yeye hatawabadili kwa vile chama kina mamlaka makubwa kuliko mtu kitakayemfadhili kugombea ili kulinda maslahi yake hata kama ni maslahi haramu.
Wanaotilia shaka ukweli huu wajiulize Mr. Clean aliishia wapi? Si aliaminiwa na Mwl Julius Nyerere akambeba na kumpatia ushindi lakini akageuka kuwa Mr. Dirty? Je huyu ni nani atakayedhaminiwa na chama kichafu asichafuke au atakayeweza kutumia usafi binafsi kusafisha chama kisichoweza kusafishika. Sijui kama kipande cha sabuni kinaweza kuisafisha bahari. Sana sana kitayeyushwa na kumezwa na kugeuka maji ya bahari basi. Hivyo, wanaoitakia nchi mema wanapaswa kutohadaiwa na yeyote atakayeteuliwa na chama ambacho hata waanzilishi na wakongwe wake wameishakichoka na kukiona hakifai tena kuaminiwa madaraka.
Chama kilichoanzishwa kupambana na uonevu na dhuruma kinapoyatenda haya kinakoma kuwa kile kile. Kwa sasa CCM iliyopo ni chama kingine tofauti na CCM aliyoanzisha Mwl Nyerere ambaye alipokufa na CCM yake ikafa ikabakia ya mafisadi, wala na watoa rushwa kama wanavyobainisha Bujiku na Warioba. Je tusipowasikiliza na kuwaamini hawa wakongwe tunataka tupate ukweli toka kwa akina Kingunge Ngombale Mwiru au Paskari Ndejembi?
Tumalizie kwa kuwapa heko Butiku na Warioba hata kama wanawapigia mbuzi gitaa. Maana, hatujui kama CCM au watanzania watawasikiliza na kujiepusha zahama wanayotaka kuipa ridhaa tena.
Chanzo; Dira Julai 16, 2015.

Sijui hapa mbwa ni yupi?


Sitaki waswahili wapenda kuigiza waigize uumbwa huu hata kama unatendwa na wazungu. Jamani nisaidieni. Nashindwa kujua hapa mbwa wa kweli ni yupi.

Tuesday, 14 July 2015

Kijiwe chapokea matokeo kwa hisia tofauti


          Baada ya bata kuwika kule Idodomya ambapo wale ambao hukutegemea wamepitishwa, Kijiwe kimepokea mzengwe huko kwa hisia tofauti. Kwa ujumla Kijiwe kilishangilia kuona baadhi ya manyangumi fisadi wakimwagwa maji mchana kweupe.
Mpemba ndiye anaanzisha mada. Anasema, “Mie kweli nimeamini kuwa kama watu wetu wataamua waweza kuondoa kaya kwenye makucha ya mafisadi. Maana ukiangalia jinsi walivogawanyika na mitandao yao, wapingaji wapaswa kukaa mkao wakula wallahi. Hata hivo, sikutegemea kama huyu Aminia Salimia Ali angeweza kupenyezwa. Ana nini zaidi ya kutuhadaa wazenjmbari tujione kama nasi tumepenyeza ntu?”
“Heri ya huyu manzi. Maana hujui anakula na nani. Hakuna aliyeniacha hoi kama Jan Makamabaye nadhani anawakilisha watoto wa vigogo,” anakamua Mijjinga huku akibwia kahawa yake.
Kapende anaamua kumchomekea, “Unashangaa hiki kitegemezi ambacho kimepitishwa ili kuwazuga vijana? Nadhani hapa kiama kimeamua kujijenga kwa ndani kwa kuwazuga wanachama wake.” Anabwia kahawa na kuendelea, “Hata huyu manzi mwingine Migiriro naye sioni kitu hapo zaidi ya ujinsia jinsia.”
Mipawa naye anakwanyua mic, “Hawa jamaa watakuwa wehu kweli kama watategemea kuwa jinsia inaweza kuwapatia rahis. Kama Marekani pamoja na kuwa huru kwa maelfu ya miaka haijawahi kuwa na rais atokanayo na ujinsia, tunaharakisha nini? Naungana na wanaodhani kuwa manzi na vitegemezi wamepitishwa ili kuzuga makundi ya akina mama na vijana. Hata hivyo, kwa Janiwari wamenoa. Maana hawakillishi vijana bali vitegemezi vya vigogo.”
Msomi anapoka mic, “Kimsingi, mie naona wote walioletwa hawana lolote hata kama wapo wenye nafuu. Huwezi kuvaa kanzu chafu ukaswalisha ati. Mfano chinga kama Maembe ana nini zaidi ya ukaribu wake na Njaa Kaya na uhasama wa taifa? Angalau  Makufuli si haba ni mchapakazi japo ni shehe mwenye udhu lakini mwenye kanzu lililojaa najisi.”
Mheshimiwa Bwege anatia buti, “Mimi nilikuwa naomba wampitishe fisadi wao Eddy Luwasha ili wapingaji wazoe urahis kirahisi rahisi au siyo.”
Msomi anakwanyua mic tena, “Mzee ulikuwa umekosea. Suppose ungefanyika uchakachuaji akapita si wengi tungehama kaya?”
Kabla ya Msomi kuendelea, Mchunguliaji anaamua kutia timu, “Mie kama angepitishwa ningejinyotoa roho au kuhama kaya. Heri angepitishwa jaji Agus.”
Mzee Maneno anaamua kukatua mic, “Unakumbuka nilisema kuwa jaji Agus wasingempa hata kama ni mja safi. Nani anataka mlevi safi jaji na mwanajeshi ili awafanyie kitu mbaya?”
Mpemba anarejea tena na kuronga, “Hakuna kitu kilichonifurahisha wallahi kama Suhanna kupiga mafisadi laana hadi wakatembeza nshiko wasijue wengi wajaisha kwa presha.”
Mijjinga anadakia, “Ami umenikumbusha mzee Kimdunge Mwehu. Sijua ataiweka wapi sura yake. Mimi natabiri kifo cha Luwasha hasa baada ya kumwaga njuluku asiambulie hata tano bora.”
Msomi anarejea, “Mimi nina wasi wasi na mfumo wetu wa elimu. Inakuwaje kihiyo kama Joseph Makamba aweze kujipenyeza kwenye kigwena na kupitisha kitegemezi chake wakati wasomi waliokubuhu wakiishia kutoona mbali au ni kwa vile kaya hii ni ya vihiyo ukiondoa sisi Kijiwe? Maana unashangaa kuwaacha wabukuzi kama profesa Mark Mwando au nuclear physicist kama Dk Bilar unakumbatia wasanii kama Maembe Makambale na Aminia!”
Mijjinga anajibu haraka, “Ulitegemea nini toka kwa wachovu wanaotegemea kughushi badala ya kupiga mabuku?”
Sofia Lion aka Kanungaembe anakula mic, “Kwanza sikubaliani na uamuzi wa kumtupa mheshimiwa Luwasha kipenzi cha wengi. Hata kama mheshimiwa hakufanikiwa bado mshikamano wa chama uko pale pale. Asiyekubali kushindwa si mshindani. Nampongeza sana.”
“Nenda kampongeze nyumbani kwake uone kama mkewe hatakutia ngeu,” anachomekea Mbwamwitu.
Kanji naye kapata upenyo, “Sasa fedha yote namwaga na vatu nakula narudisha wipi? Ile bana iko roho juli sana. Nasaidia chovu sana. Kama nakuwa rahis kaye veza piga hatua na kuwa tajir kama nasema yeye Edi.”
Kapende anachomekea haraka haraka, “Hakuna cha roho nzuri wala kusaidia wachovu. Baada ya kumwagwa maji utaona kama ataendelea na huo ukarimu wa msimu. Kwa vile amekosa alichokuwa akikisaka, kama siyo kurejesha namba kwa shinikizo la roho na moyo atawachukia walaji na kuwaogopa kama ukoma. Kwani alidhani atawatumia asijue walimtumia na kumlia vyake.”
Mipawa anajibu kwa hasira, “Hafi ngurumbili hasa ikizingatiwa kuwa njuluku aliyokuwa akimwaga hakuitolea jasho. Hivyo, Bwana ametoa Bwana ametwaa.”
Mgosi Machungi ambaye leo alichelewa anaamua kutia buti, “Shikubai huu mchezo tinaofanyiwa. Kama wapiga kua watakuwa makini hata hawa jamaa wangeeta maaika angeshindwa kiahisi na wapingaji kama watajipanga vizui.”
Mijjinga anakamua mic tena, “Kama Eddy angesikiliza ushauri wa akina mzee Mpayukaji angeokoa lau njuluku zake. Badala yake alipuuzia alipoambiwa hatoboi. Akawa anawachukia wajumbe badala ya kuangalia uzito wa ujumbe.”
“Kidume Mpayukaji ni mtume aliyesalia hasa kwa wachovu,” anachomekea Mchunguliaji huku akichukua gazeti toka mezani kwangu.
Kijiwe kikiwa kinanoga si ukaja msafara wa wasanii wakienda kumuaga msanii mwenzao. Watakula mafi yao acha Makufuri muone kama lango la ikulu hamjawekewa kufuli msiende kumsanii rahis. Punde si punde ulifuatia msafara wa Luwasha ukienda zake kuomboleza kumegwa na kufishwa kwa ndoto zake za kuilangua kaya kwa washitiri wake.
Chanzo: Tanzania Daima Julai 15, 2015.

Monday, 13 July 2015

Warioba, CCM na sikio la kufa



          
Image result for photos of joseph warioba

 Baada ya kung’atuka madarakani na baadaye chamani kwa muanzilishi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) marehemu Mwl Julius Nyerere kilipata pigo ambalo pengo lake limeshindwa kuzibika. Maana, tangia wakati ule –karibu kila mwaka –CCM imekuwa ikiendelea kuporomoka hadi kuishi kwa matumaini na ubangaizaji utokanao na mchezo wa rafu kama vile kuchakachua uchaguzi na kufadhiliwa na mafisadi.Hivi karibuni mkongwe mwingine –kati ya wachache waliobakia na waliowashinda makuwadi na wasaka urais –mzee Joseph Warioba alikiasa chama chake ingawa sijui kama kitamsikiliza hasa ikizingatiwa uhuni aliokwishafanyiwa na wakubwa wa chama na serikali.

Warioba alikaririwa akisema, “CCM inakabiliwa na wakati mgumu wa kupitisha jina la mgombea urais kutokana na waliojitokeza kuwania nafasi hiyo kufikia 38, na mpaka sasa imekuwa ni vigumu kutabiri atakayepitishwa, jambo ambalo halikujitokeza wakati wa upitishwaji wa mgombea urais wa chama hicho mwaka 1995 na 2005.” Anachobainisha jaji Warioba hapa ni kwamba demokrasia lazima iwe na mipaka. Wote tunajua kuwa uhuru bila mipaka ni wendawazimu. Kimsingi, sasa kinachoitwa demokrasia ndani ya chama kisicho na historia ya demokrasia zaidi ya kuipinga si demokrasia kitu bali wendawazimu na uroho wa madaraka wa kawaida. Haiwezekani watu wastaarabu wenye kukubaliana na kuelewana wakaruhusu kila mmoja autake ukuu. Je kama mwili wote ungekuwa sikio kichwa kingekuwa wapi? Mbona vyama vya upinzani ambavyo viliteseka na kuhakikisha taifa linaingia kwenye demokrasia ya vyama vingi havina utitiri wa wagombea?

Wahenga walisema: Sikio la kufa halisikii dawa. Warioba kwa mapenzi na uzalendo wake vilivyotukuka amejitahidi kuwasaidia wenzake. Je watamsikiliza wakati walishamdhalilisha hasa baada ya kuwapa ukweli ambao hawakutaka kuusikia? Nani amsikilize mzee aliyepitwa wakati kama Warioba ambaye badala ya kuchangamkia madili anahagaishwa na maadili? Warioba ni sawa na mtu aliyeko nyikani. Warioba amejitahidi kufanya kile ambacho kimewashinda wengi. Amejitofautisha na akina Kingunge Ngombale Mwiru na Paskari Ndejembi wanaoweza kukodiwa na watia nia kama bodaboda. Amewashinda akina Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Salmin Amour na Amani Karume wanaoonyesha kuvizia upepo. Warioba amefanya kile ambacho waingereza huita to stand up and be counted au kuwa tayari kufanya maamuzi magumu hata yakimaanisha kulaumiwa. Hakika wamebakia wachache wa namna hii. Laiti CCM ingewasikiliza.

Warioba aliongeza, “Waliotangaza nia wamekuwa wakieleza sera zao na ukiwasikiliza unaona kama walikuwa wagombea binafsi hivi kwa sababu CCM ina sera, wanayo ilani ambayo ipo tayari na yeyote atakayepeperusha bendera ya CCM lazima ajikite kwenye ilani ya chama.” Kama siyo sikio la kufa au tuseme kuchanganyikiwa na kuparaganyikiwa ni nini kwa chama ambacho kilitumia kila hila kupinga mgombea binafsi kujikuta kikiwa na wagombea wenye kila sifa za mgombea binafsi? Je ni laana au historia kutaka kurekebisha mambo? Je CCM watauvuka huu mtihani unaolenga kupima na kuonyesha unafiki na upogo wao salama bila kuwasikiliza akina Warioba? Je kama hali ni hii CCM inayokutana hivi karibuni kuteua na kupitisha mgombea wake itampata wapi wakati waliojitokeza wote hawafai na wala hawana mpango na sera zake? Laiti akina Abdulramahan Kinana katibu mkuu wa CCM wasingekuwa wamejiingiza kwenye siasa za usanii walipaswa kuwa na kibarua kigumu cha kuueleza umma mantiki ya kupambanisha wagombea binafsi kumpata mgombea wa chama.

Je kwa CCM kutekwa na wagombea binafsi hadi ikawahalalisha kama wagombea wa chama siyo kuishiwa na kugeuka chama tegemezi ambacho hakina mtaji zaidi ya kutegemea ubabe wa watia nia? Je CCM hii kipofu itashidwa kumpitisha fisadi kama alivyowahi kutahadharisha mmojawapo wa wagombea ambaye pia ni mtoto wa wa mwanzilishi wa CCM, Makongoro Nyerere aliyekaririwa akisema, “Mojawapo ya matatizo ya chama chetu ambayo ni lazima Rais ajaye apambane nayo ni ukweli kwamba kuna majimbo ya uchaguzi hapa Tanzania ambayo kama mtu hutoi rushwa huwezi kupita.” Maneno ya Makongoro ambaye amejizolea umaarufu kwa kusema ukweli ni ushahidi tosha kuwa bila kuwa fisadi au tajiri CCM hupenyi. Je CCM itavuka kikwazo hiki wakati imekaa kimya wakati fedha zikimwagwa hata kabla ya kipenga cha mwisho kupigwa?

Je nini wana CCM na watanzania wengine wategemee? Jaji Warioba ana jibu, “Hawa ndio watakwenda kuchuja, sasa hapa itakuwa kazi ngumu na inawezekana kukawa na mgongano wa maslahi na hilo lisipoangaliwa linaweza kufanya mchujo ukaonekana kuwa haukuwa wa haki. Jambo hili linatakiwa kuangaliwa na hasa kwa kuwa kuna makundi.” Kwa lugha rahisi ni kwamba kuna uwezekano mkubwa wa CCM kuanguka kwenye mtego ikaamua kutokana na msukumo wa mtu na si sera. Hali inazidi kuwa mbaya hasa ikizingatiwa kuwa CCM ina gonjwa kubwa sana la mitandao ya kimaslahi ambapo karibu kila kiongozi ana mtandao wake kuanzia watangaza nia hata wale watakaowachuja.

Tumalize kwa kusema kuwa CCM sasa ni sikio la kufa ambalo halisikii dawa. Je CCM watamsikiliza au kumpuuzia mzee Warioba?
Chanzo: Dira Julai 13, 2015.

Poor Kimdunge Ngumbalu Mwehu

Sunday, 12 July 2015

Wasanii wanapokuwa bora kuliko waandishi!






















 Kifo mwandishi chipukizi lakini mwenye athari kubwa katika tasnia ya uandishi wa habari marehemu Edson Kamukara kimetufundisha jambo moja kubwa. Kifo cha ghafla cha Kamukara licha ya kusababishwa na ajali ya kimaskini kimetuachia somo kuwa kumbe mbele ya serikali yetu wasanii ni bora kuliko waandishi wa habari!
Nani alitegemea kuwa mwandishi kama huyu aliyeanza kujijengea umaarufu kwa ithibati na taaluma angeagwa bila kupokea lau rambirambi toka Ikulu? Sina sababu ya kuilaumu ikulu hasa ikizingatiwa kuwa huwa ni utashi wake juu ya nani imepende au kumchukia. Nasema –kama mwana taaluma na mwandishi –kuwa kitendo cha ikulu kukaa kimya kwenye msiba huu kinaacha maswali mengi kuliko majibu. Tulizoea kusoma salamu za rambirambi toka ikulu na wakati mwingine kumuona rais Jakaya Kikwete akishiriki ima kuaga au mazishi ya watu mbali mbali wengi wakiwamo wasanii. Tulimuona kwenye misiba ya Kanumba, mzee Small na wengine. Sasa tunajiuliza: Mbona hatukumuona rais wetu kwenye msiba wa mwenzetu kunani? Je inaweza kuwa ukweli kuwa waandishi wa habari hufunga ndoa na wanasiasa wanapokuwa wakisaka ulaji na kuivunja wanapopata ulaji?
Kwa wanaojua thamani ya taaluma ya habari, wameshangaa na kusikitika hasa ikizingatiwa kuwa katika jamii yetu –hata hivyo –mambo ni tofauti. Msanii anapewa umuhimu zaidi ya mwandishi kwa vile watu wetu wengi hawana muda wa kufikiri. Unashangaa mwandishi –kwa mfano wa vitabu –kazi zake haziuzi wakati za wasanii zinauza. Je hii maana yake ni nini kama siyo kujenga taifa la kidaku na kijinga lisilopenda maarifa na badala yake likapenda mambo rahisi rahisi na mengine ya hovyo?
Jambo ambalo nimejifunza ni kwamba waandishi wamewekwa kwenye matabaka ya wanaokubalika na watawala na wasiokubalika. Maana haiingii akilini ikulu itoe salamu za rambirambi ulipotokea msiba wa mtangazaji wa zamani wa radio Tanzania Mshindo Mkeyenge hapo Mei 25, 2015 na kwenye msiba wa mama wa Mwaibale ukiachia mbali ule wa Florence Dyauli lakini ishindwe kufanya hivyo kwenye msiba wa Kamukara uliotokea mwenzi mmoja baadaye. Je ni kwa sababu Kamukara hakuwa anaandikia magazeti ya chama na serikali au ni kutokana msimamo wake wa kutopenda kutumiwa kama nepi? Je huu si ubaguzi wa kiitikadi? Je kama wote tungekuwa nepi kofia ingekuwa wapi?
Ukiachana na kukosekana kwa rais kwenye msiba wa Kamukara, unaweza kujikumbusha utitiri wa magazeti ya udaku tena yakiuza kama keki huku magazeti yasiyo na udaku yakiozea kwenye mbao. Tunaandika hili si kumtetea mwenzetu aliyetangulia mbele ya haki bali kutumia mwitikio wa baadhi ya taasisi za umma kuonyesha uoza wa kimfumo ambao unalikabili taifa letu.
Baada ya watawala kuua elimu na kuendekeza mambo ya hovyo kama vile kufanya siasa karibu katika kila kitu, kuna hatari ya vizazi vijavyo vikatawaliwa na wageni ndani ya nchi yao kutokana na kutokuwa na utamaduni wa kujisomea, kutunga vitabu na kudurusu mambo.
Zamani nakumbuka nilimtembelea rafiki yangu maeneo ya Masaki. Nilipoingia sebuleni kwake nililakiwa na kabati kubwa la vyombo vya kulia. Nilipata mstuko. Baada ya kuamkuana na kukaa kitambo nilimuuliza kama ana maktaba yake binafsi. Alisema kuwa ana vitabu vichache lakini viko kwenye maboksi. Nilishangaa zaidi. Ilibidi nimuulize kwanini asivinunulie shelf na kuviweka. Naye aliniuliza: Nikinunua shelf nitaiweka wapi? Nilimjibu kwanini umepata nafasi ya kupamba vyombo vya kulia ambavyo kimsingi vilipaswa vikae jikoni lakini unakosa nafasi ya kuweka vitabu ambavyo kimsingi ndivyo vimekuwezesha kupata kazi nzuri ya kuishi Masaki na kuweza hata kununua vyombo vya thamani vya kulia?
Rafiki yangu alipigwa na butwaa na akaniahidi angerekebisha kasoro ile. Je ni nyumba ngapi zimejaza upuuzi kama vyombo vya kulia kwenye sebule wakati vitabu vikiozea kwenye maboksi?
Tukirejea kwenye kifo cha Kamukara na jinsi ambavyo mwitikio wa baadhi ya wenzetu tena wanaowategemea waandishi wa habari umekuwa haba, mara nyingi inategemea mhusika alikuwa nani katika jamii. Kama angekuwa kanjanja huenda angeenziwa na wale wanaoweza kumtumia kama nepi. Tofauti na hapo anachoweza kuambulia ni kile kilichowahi kuwakumba akina Absalom Kibanda walipokataa kuwa kitanda kimoja na mafisadi au Stan Katabaro aliyeuawa kwa kushupalia kashfa ya Loliondo zama za ruksa.
Ila ni aibu kwa watu wanaojulikana kuwa sauti ya wasio na sauti,  the voice of the voiceless kuchukiwa kiasi hiki. Hatuna sababu ya kuwalazimisha wahusika watupende, lakini tuna haki ya kuwaambia kuwa wanajenga jamii ya kijinga na kitwahuti inayochukia maarifa na kupenda upuuzi. Ukienda nchi jirani kama Kenya Rwanda na Uganda hata Burundi pamoja na mitafaruko yake, hawana magazeti ya udaku kama Tanzania. Je kuwa na wingi wa magazeti ya udaku ni sifa nzuri au ni kielelezo kuwa sisi ni wadaku tofauti na wenzetu ambao siyo?
Tunaomba tumalizie kwa kuitaka jamii ibadilike ianze kuthamini michango ya watu na ijenge utamaduni wa kuthamini maarifa kuliko upuuzi kama vile burdani. Japo binadamu hawezi kuishi kwa kusoma tu, anahitaji burdani lakini ahitaji kwa kiasi kikubwa kuliko taarifa na maarifa. Ni aibu tunaposhabikia upuuzi na kupuuza mambo ya maana.
Chanzo: Dira Julai 12, 2015.

Je huyu staili yake ya kutawala itakuwa ipi?


Saturday, 11 July 2015

Bravo Eddy Luwasha however

  • LOWASSA CAN YET STEP TO CANAAN: BY NOVA KAMBOTA.
 
     Dear Eddy Luwasha,
 Though I don’t support your bid seeking to become next president, I envy your evasive and organizational skills. If being supported by many Chama Cha Mapandikizi (CCM) bigwigs––especially regional chairs would have been the only means of appointing its flagbearer ––you’d have already clinched the ticket to faceoff with the opposition candidate. Again, things are just beginning. Bro, how did you manage to corner them so as to back you unseeingly and perilously?
I like the way you came forth asking boozers to ignore all those who say you are corrupt. Like a learned friend, you wanted them to adduce evidence vis-à-vis when, where, from whom and how much dosh you solicited. By the way, taking bribes or robbing public coffers don’t need all such legal braggadocios.  For, the political court is different from the court of law. Guess what. Even Jimmy Rugemalayer and Singasinga of escrow will say the same shall one confront them. The state of denial is a Homo sapiens’ nature. Jumping a smoking gun is a normal thing for any cornered person.
I, for one, thought you’d have shed some light on what you know about Richmonduli that’s hunted and haunted you so as to make your bid an impossible thing. The other day little bird told me that for you to get to Magogoni is as good as the camel to go through the eye of the need.
Another thing that left me in stitches is your assertion that you don’t have much dosh to soften the party regional chairs. Really? Why don’t we see paupers like that earthling from Kigoma being backed or supported by any of the same? Penye rupia kaka. You know what I mean. I don’t think that geezers like Kimdunge Ngumbaru Mwehu or Paskari Ndiyejembe could dress down on the agora without being given some mshiko. I thus, don’t think such ancient Homo sapiens are just supporting you out of true altruistic love. If you didn’t give them some dosh, there’s something they expect from you if you become prezzo. There must be something to exchange hand either by the way of promise or just stimulus. It isn’t easy for such bigwigs to dress themselves down without any motivation.
Bro, let be serious a wee bit. When are you going to shed light on Richmonduli that saw you pack and jump into water? Do you think –if there’s no way you’re implicated–would it be easy–for you–to relinquish the dear power that you’re now seeking? The other day one boozer successfully convinced me. He gave me an English adage saying that show me your friends I will tell you who you’re. Guess what. When you showered Ni Ziro Kadamage saying you’d like to have as many as of him as possible, the folk said those are your friends. So, he concluded that with such a venal and thuggish company you can’t deliver the hunk from where your pal thrust it after enacting vending politics. For him, Kadamage, Roast Tamu, Rugemalayer, Singasinga, Endelea Chenga and others are just spineless and pathetic thugs that should never be mentioned by the lips of a clean person. Whoever is bed with them is surely like them.
By the way, is your daughter still working with Bunch of Tembo aka BoT? How did you manage to get your son a job in the embassy in Bondeni sir? I just want to know so that I can send my kitegemezi abroad to the embassy. This will help me to get where to go whenever I am bored with what will be going on Bongolalaland.
Regarding your appeal that people should stop calling you fisadi, I think it very difficult given that you are the one going to them seeking urahis.  You know what. Lisemwalo kaka. You can deny as many times as possible, you can swear by land and heaven. The taint doesn’t go away so easily. If it were me, I would either pulled out from the race or divulge whatever I know about Richmonduli that seems to be the cross on your neck my dear bro. English proverb has it, “Honesty is the best policy.” You better open up. Maybe, you can salvage your tainted image. Again, shall people press on, worry not. As English proverb says, you can't always get what you want. Sometimes, we need to throw towel in when we find that things don’t work the way we expected.

Importantly, I salute your resilience save that I don’t endorse it. Sometimes we need to let go especially those things that prove to be unreachable. He who does not admit defeat is not a sportsman.
Source: Thisday July 12, 2015.