Sunday, 15 July 2012

CCM na Dangote wana biashara gani?


Bilionea tajiri kuliko wote barani Afrika Aliko Dangote (Pichani) toka Nigeria akiwa na katibu mkuu wa CCM Wilson Mukama jijini Dar. Dangote yumo nchini Tanzania kwa ziara ya kibiashara. Ajabu ya maajabu jamaa huyu anayetambulishwa kama mwekezaji tunaambiwa ni mgeni wa Chama Cha Mapinduzi. Je CCM ina biashara gani? Wapo wanaodhani kuwa huyu jamaa alitaka kuwekeza nchini lakini CCM ikamnyaka ili kuanza kusaka pesa ya kuchakachua uchaguzi ujao. Wenye kuweza kujua watupe mantiki ya mwekezaji kuwa mgeni wa CCM chama tawala. Je hii haiwezi kuleta mgongano wa kimaslahi hata kama jamaa ataamua kuwekeza nchini? Maana huu ni ushahidi kuwa Dangote ni mtu wa CCM ambaye anaweza kupewa upendeleo ili alipe fadhila baadaye. Je tunamkaribisha Chavda mwingine?

7 comments:

Anonymous said...

Mbona unaanza visingizio kabla hata hatujaanza kampeni ya 2015.
sijuwi kuchakachuwa sijuwi nini.

"tulia funga mkanda"
tuongozwe na mtu hata nyumba hawezi kuongoza hawezi kufanya uadilifu kwa mke na watoto ataongoza TANZANIA.
Bora kuchagua JIWE

Anonymous said...

Anon 1
Bure kabisa. Je nawe ni gamba? Lawama zako za nini iwapo kila kitu kiko wazi?

Anonymous said...

Shetani ndio anakuwa hafanyi jambo zuri hata moja katika maisha

lakini binadamu hutokea akafanya makosa sasa wewe kila siku unaona makosa tuu pekee

hakuna siku Ccm inafanya jambo zuri.?

wewe ni kulaumu mtindo mmmoja
hebu jaribu kuelimisha wananchi
kupitia hapa Mwalimu Mhango.

kosoa halafu toa suluhisho.

PhD holder Mze masharubu

Anonymous said...

Masharubu ya shaba
ano number2 hii ni blog ya makapi ya chadema oiro chafu au hujuwi
hii nepi ya chadema

NN Mhango said...

Nawaashukuru wachangiaji wote waliotoa maoni ya kwenye blog hii ingawa utawala wa blog hii haukubaliana na baadhi ya hoja zisizo na heshima wala mashiko. Hivyo, tunatoa onyo kwa wanaotumia uhuru wa kutoa maoni bila kulazimika kungoja zipitiwe kuwa tutazifuta ikibidi. Pia tunakanusha kuwa blog hii, kwa namna yoyote iwayo ni shabiki wa chama chochote. Kazi yetu ni kuelimisha umma bila kujali nani atafurahi au kuchukia.Kuna haja ya watu kuwa na heshima na kutumia akili badala ya kutukana uhuru wa kutoa comments. Kwani ni vigumu kuweka kipengele cha kuchuja maoni kama wengine wanvyofanya?
Utawala

Anonymous said...

mbana mkali heshima inaanza nyumbani hao walochangia wamechangia kwa mujibu wa lugha ya blog hii
kwani hupiti blog nyengine ukaona.

hao ano wapo sawa kabisa wanatumia lugha ya blog hii sasa wewe unakuwa mkali kwa nini
hoja za matusi zinajibiwa kwa matusi
hoja zisizokua na heshima zitajibiwa bila ya heshima.
blog ya chadema labda?

Anonymous said...

Bure kabisa. Je nawe ni gamba?
sasa wewe unajibu hivi
mtu katowa mawazo yake kwa nini umwite Gamba?

halafu umeandika

Leave your comment
ya nini hii ?