Wednesday, 4 July 2012

Je wajua?


Swala huyu aina ya Okapi hupatikana nchini DRC pekee Duniani. Hata hivyo yuko kwenye kitisho cha kutoweka kutokana na kuaawa hovyo  na wawindaji ambao kimsingi hawajui kuwa hii ni tuzo pekee kwao waliyopewa na Mwenyezi Mungu. Hata hivyo nani wa kulaumiwa iwapo wahusika hawaoni faidi ya kuwa na utajiri kama huu ambao katika nchi nyingi za kiafrika hutumiwa na watawala wezi kujinufaisha badala ya taifa? Rejea kusafirishwa kwa wanyama hai nchini Tanzania hivi karibuni huku serikali ikijifanya haijui wakati ilihusika moja kwa moja. Je tunamkomoa nani kama si vizazi vyetu vijavyo?

No comments: