Tuesday, 10 July 2012

Tumshauri Salma KikweteRais Jakaya Kikwete na mkewe salama wakisalimiana na watanzania  kwenye hotel ya Regency Hyatt Churchil jijini London,

Wengi wanadhani muda mwingi anaoutumia kuzurura na mumewe, mke wa rais Salma Kikwete angeutumia kujisomea na angalau kupata hata elimu ya msingi wa kawaida. Hii licha ya kumsaidia kwenda na wakati ingeokoa hata pesa ya umma wanayotumia hovyo hovyo na mumewe. Kwa vile watanzania wanaonekana kuwa na vipaumbele tofauti, per diem inaonekana kuwa na thamani kuliko elimu. Ni aibu kuwa na first lady asiyeweza hata kuandika na kusoma hotuba zaidi ya kuonekana ubavuni mwa mumewe kila aendako.

2 comments:

Miss K. said...

Hawa wanafanya kama kumbikumbi badala ya kufikiria maendeleo wao ni kuzurura tu. Kaka Mhango hawa walitia nadhiri kuwa wakipata "kula" watatembea nchi zote duniani. Wanahakikisha pesa ya mlala hoi yote inafujwa...

NN Mhango said...

Miss K nakushukuru kwa kunitembelea na kutoa nasaha safi hivi. Ila kumbuka hata kama waliweka nadhiri zina mwisho na unaweza kuwa mbaya kwao amini dada yangu.