- Tanzania ni mojawapo ya nchi yenye uongozi usio na kumbukumbu na mgumu kujifunza. Ilipozama meli ya MV Bukoba na kuua mamia ya watu mwaka 1995 wengi walidhani wangejifunza. Haikuwa. Mwaka jana meli ya MV Spice Islander ilizama mwaka jana na kuua mamia kama kawaida. Mwaka huu tena meli ya MV Skagit imezama mwaka huu na kuua watu wengi huku wengine wengi wakiwa hawajulikani walipo. Kinachokera ni kuona upogo wa viongozi wetu wanaokimbilia kwenye maeneo ya ajali eti kutoa mkono wa pole badala ya kushughulikia vyanzo vya mauaji haya ya kizembe. Je wafe wangapi ili watu watie akilini? Je ni kutokana na ukweli kuwa viongozi wetu hawasafirii hii mikangafu kwa vile wana usafiri wa anga ambao ni wa uhakika?
How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Friday, 20 July 2012
Kuzama meli: Wafe wangapi tustuke?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment