Saturday, 21 July 2012

Mnaotapeliwa na wachunaji wajiitao wachungaji tazama hii

Umejitokeza mtindo wa matapeli kutumia dini kuwaibia watu maskini na wenye matatizo mbali mbali. Mara nyingi wizi huu umefanywa kuwa rahisi kutokana na waathirika kuwa wajinga, wenye tamaa, waliochanganyikiwa au wenye imani haba. Nchini Kenya umetokea wizi wa aina hii ambapo matapeli waliofungua makanisa yao huwatumia hata malaya kuwahadaa waumini eti wanatenda miujiza wakati ni wezi wa kawaida.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mungu wangu, kweli huu sasa ni mwisho wa dunia haswaaa..

Anonymous said...

Siyo mwisho wa dunia. Mbona kina Kakobe, Rwakatare, Gamanywa, Gwajima, Lusekelo na matapeli wengine wamekuwapo kitambo?

Ng'wanaMwamapalala said...

Lubala lutale, dini hizi tuliletewa ili kutapeliwa kifikra na kimawazo. Dini zetu za jadi zilipigwa mizengwe hadi zikatokomea kusikojulikana. Huwa inanishangaza matukio kama haya yakitokea jamii huanza kuweweseka na kupigwa na butwaanwakati haya yote ni muendelezo wa mzizi wa utapeli