Monday, 9 July 2012

Rais dhaifu, asiyejali na kusikia tunaye!Taarifa zilizopo ni kwamba rais Jakaya Kikwete amekwenda Uingereza kuhudhuria mkutano kimataifa wa Upangaji Uzazi. Kwa jinsi mgomo wa madaktari na kutekwa kwa kiongozi wa madaktari kunakodaiwa kufanywa na serikali ya Kikwete wengi walidhani angetulia nyumbani na kutafuta ufumbuzi. Lakini kama habari hizi ni kweli basi ni ushahidi kuwa Tanzania inaye rais mpenda safari kuliko watu wake. Ni rais wa kwanza kuonyesha kiburi na upofu na upogo wa ajabu ambapo hufanya mambo muhimu kuwa ya hovyo na ya hovyo kuwa ya muhimu. Wengi walikuwa wakidhani Kikwete amepatikana kipindi hiki cha mgomo kutokana na kutokuwepo tukio la kumsaidia kukimbia lawama. Maana mgomo ulipoanza mwezi wa pili alitumia tukio la kifo cha msanii mmoja kukwepa kuwajibika ukiachia mbali kutimkia Brazil kwenye kikao ambacho hakikuwa na umuhimu hivyo. Rais na uzazi wa mpango wapi na wapi wakati waziri wa Afya na waziri wa anayehusika na mambo ya wanawake na watoto wapo? Kweli alijisemea John Mnyika mbunge wa Ubungo (CHADEMA) kuwa Kikwete ni dhaifu sawa na chama chake! Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

No comments: