Wednesday, 4 July 2012

Utoroshaji mabilioni ya shilingi Uswisi Mwinyi na Mkapa watanusurika?


Kwa wanaojua jinsi marais Ali Hassan Mwinyi (mzee Ruksa) na Benjamin Mkapa (Mjasiriamali) walivyoendesha Tanzania, hana wasi wasi kuwa kati ya vigogo sita wanaodaiwa kuficha jumla ya Dola za Kimarekani, 196.8 nchini Uswisi watakuwamo. Chini ya dhana ya ruksa, Mwinyi, kwa kuwatumia baadhi ya waarabu na wahindi marafiki zake, alichota pesa nyingi ingawa huwa hatajwi. Nani mara hii kasahau kashfa kama vile IPTL iliyoingizwa nchini na mawaziri wake Profesa Kighoma Malima na Jakaya Kikwete ukiachia mbali wengine? Nani hakumbuki kashfa ya watu waliokuwa karibu na mke wa Mwinyi kupata vimemo vya kununulia madala dala na viwanja na upuuzi mwingi. Kuhusu Mkapa kila mtu anajua jinsi alivyokwapua pesa ya umma kuanzia wizi wa EPA hadi kujimilkisha machimbo ya makaa ya mawe ya Kiwira. Je kwa mtaji huu wawili hawa hata huyu aliyepo madarakani watanusurika na kashfa hii?

No comments: