Wednesday, 18 July 2012

Tanzania aimegeuka nchi ya vidogoki na vibaka!


Hakuna ubishi kuwa taifa la Tanzania liko msambweni. Kila unaposoma ni ufisadi, wizi, rushwa, uzembe na matumizi mabaya ya pesa ya umma. Kikundi kidogo cha watu kimeamua kuiteka nchi nyara na kuwageuza wananchi wa kawaida wabangaizaji kiasi cha kuanza kushabikia jinai. Leo tunatoa mfano mmoja. Baada ya serikali na taasisi zake kuwa wanatumia umeme maji na simu bila kulipia, wananchi  nao wamegundua njia nyingine ya kujipatia huduma bila kulipia. Cha mno kwa sasa ni ile hali ya kugundulika mitandao ya kuiba umeme. Hebu jiulize hali ni mbaya kiasi gani iwapo hata wakala wa Tanesco analiibia shirika analowakilisha umeme? Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

No comments: