Friday, 6 July 2012

UN yapendekeza kodi ya mabilionea kusaidia nchi maskini


(Goodshoot)

Umoja wa mataifa (UN) umekuja na mkakati wa kuzisaidia nchi maskini kwa kutaka mabilionea duniani watozwe kodi ili kuweza kupata jumla ya Dola  400,000,000,000 kusaidia nchi maskini. Kwa juu ni mkakati mzuri ingawa kisheria ni vigumu hasa ikizingatiwa kuwa sheria za kibepari haziruhusu mtu kuweka shuruti isiyo ya lazima kwenye mali au mapato ya mtu binafsi. Kitu kingine kinachofanya mkakati huu kuona kama hauna maana ni ukweli kuwa kuna pesa nyingi toka nchi maskini imefichwa kwenye mabenki ya Ulaya hasa kule Uswisi. Kwa mfano kama nchi kapuku kama Nigeria ina watu binafsi walioliibia taifa na kuweza kuficha kiasi cha Dola 130,000,000,000. Kwanini nchi hii ichangiwe badala ya kuwezeshwa kurejesha pesa hii toka Uswisi? Je hii cha kuwatoza kodi mabilionea ni mbinu ya nchi tajiri kuzifumba macho nchi maskini kama Nigeria kuachana na kushughulikia kurejesha pesa yake toka nje? Je hili ni jibu? Kwanini nchi tajiri zisifikirie kufanya biashara kwa ulinganifu na nchi maskini badala ya kuhangaika na vitu visivyoingia akilini? Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

No comments: