Monday, 9 July 2012

Waswahili kwa miigizo na ulimbukeni!Wanafunzi wa kike zaidi ya 400 wa shule ya sekondari wasichana ya Rwathia nchini Kenya wametoa mpya. Wamegomea masomo kutokana na kutaka wavae vimini tena vyenye kuvutia. Maskini utakuta hawa ni watoto wa maskini. Maana kwa anayeijua Kenya shule tajwa si mojawapo ya shule za wenye nazo. Wasichana hao wamekwenda hatua zaidi kwa kuzikata sare zao wakidai ni ndefu na haziendani na umri wao. Hii ni ajabu maana hata kwenye nchi zilizoendelea wanakoendekeza haki kama hizi huwa kuna mipaka. Si kila kimini kinaweza kuvaliwa shuleni. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

No comments: