Thursday, 26 July 2012

Mwanzo wa mwisho wa Bashar?Kwa mujibu wa shirika la habari la Al Jazeera ni kwamba rais wa Syiria Bashar Asaad na kundi lake wanaweza kukabidhi madaraka wakati wowote. Al Jazeera lilimnukuu waziri mkuu wa Uturuki Recep  Teyyip Erdogan akisema kuwa ni suala la muda kwa Bashar na genge lake kukabidhi madaraka kwa umma. Erdogan alisema kuwa utawala mpya unaweza kuchukua hatamu wakati wowete. Hata Umoja wa Mataifa umeachana na juhudi zilizokuwapo za kujadiliana na wapinzani. Je mwanzo wa mwisho wa imla mwingine Bashar Asaad ndiyo umewadia? Nani atafuatia? Afrika Kusini mwa Sahara watakengeuka na kuzinduka toka usingizini? Time will surely tell.

No comments: