Tuesday, 10 July 2012

Tanesco inapowatangazia kiama dagaa na kuacha mapapa


Kuna taarifa kuwa shirika la umeme la taifa (TANESCO) limetangaza kiama kwa wanaoliibia shirika hilo. Taarifa hizi zilipotoka wengi walidhani zina maana na wanaolengwa ni wezi waliolisababishia shirika kilema kinachojikongoja nacho. Hapa walitegemea kuona  wezi kama wale wa Richmond, IPTL, Dowans na wengine wengi wakishukiwa na kiama hicho. Kumbe kiama chenyewe kinalenga vidagaa na vishoka wakati majambazi wakubwa wanaendelea kuitwa waheshimwa! Wengi walidhani kuwa kiama husika kingeishukia serikali na asasi zake wanaotumia umeme bila kulipa wala kujali! JWTZ, Ikulu na Zanzibar mpo? Ukiachia hawa ni kwamba wezi wa umeme wamo humo humo Tanesco na si kwingine. Hiyo ndiyo Bongo ambapo kila jambazi huiba ofisini mwake. Hii ndiyo Bongo ambapo mtu aweza kulala maskini akaamka milionea na hakuna anayeuliza alivyopata utajiri wake.  Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

No comments: