Tuesday, 17 July 2012

Maskini kwa ulimbukeni!

Busati lote hili la nini na ni bei gani kulinunua? Ajabu wanaowekewa ni watoto wa maskini wa kunuka! Kwanini waafrika hututaki kujikomboa na kuwa huru hadi tunaiga kila upuuzi? Hivi pesa iliyotumika kununua busati hilo na ya kulitunza ingesomesha au kutibu watu wangapi? Sikumbuki kumuona rais Barack Obama akipenda au kuwekewa makandokando kama haya maana yeye na taifa lake wako huru hata wakifanya hivyo ni jadi yao na uchumi wao unaruhusu. Si watumwa wa ukale na miigizo. Tunafanya  israfu yote hii kumkomoa nani kama si mlipa kodi maskini ambaye tumemgeuza punda wetu?Rais Ellen Johnson-Sirleaf wa Liberia na mwenyeji wake Jakaya Kikwete ikulu Dar es Salaam.

1 comment:

Anonymous said...

Barack Obama akipenda au kuwekewa makandokando kama haya maana yeye na taifa lake wako huru hata wakifanya hivyo ni jadi yao na uchumi wao unaruhusu.

Sasa akifanya Obama sawa na Akifanya Kikwete inakuwa insrafu.
What was your point here.