Monday, 23 July 2012

Kujiuzulu Masoud nakupongeza


Alyekuwa waziri wa Mawasiliano na Miundo mbinu  wa Zanzibar, Hamad Masoud akiwa na waziri wa Uchukuzi wa Muungano Dk Harrison Mwakyembe (Pichani) ameweka rekodi ya kuwa afisa wa serikali kuwajibika tokana na kuonekana uzembe kwenye wizara yake. Masoud alifikia uamuzi huu baada ya kutokea kwa ajali ya meli ya MV Skagit hivi karibuni ikiwa ni ajali ya pili ndani ya miezi minane. Je ni wangapi wamepata funzo kuwa kuwajibika siyo jambo baya bali njia ya kutatua matatizo? Tunampongeza Masoud kwa uamuzi huu utokanao na ukomavu na kuona ukweli.

No comments: