Tuesday, 3 July 2012

Huu ndiyo uzawa aliotetea Idd Simba au ufisi wake?

Ingawa habari za kufikishwa mahakamani kwa waziri wa zamani wa Biashara Idd Simba na wenzake aliohudumu nao kwenye Bodi ya UDA si mpya, nimefadhaishwa na kuhusishwa kwake na kampuni la kimarekani linalotaka kukwapua ardhi nchini. Sina video ya mahojiano aliyofanya Simba na shirika moja la habari la Marekani akisema kuhamishwa au kutohamishwa kwa wananchi waliomilki ardhi inayotaka kutumiwa na kampuni lake halimhusu, nimesikitishwa na mwanasiasa huyu aliyejizolea umaarufu kwa sera yake ya uzawa. Nikikumbuka tulivyozoeana kutaniana naye akiniita paparazi kila nilipoendelea habari kwake, hata nashindwa kuwaamini wanasiasa. Kumbe wanasiasa waweza kuwa chui kwenye ngozi ya kondoo!

No comments: