The Chant of Savant

Monday 2 July 2012

Mgomo wa Madaktari mwanzo wa mwisho wa Kikwete?


Ingawa wengi hawalioni hivyo, kwa wanaokumbuka kilichomkuta imla wa zamani wa Libya Muamar Gaddafi, watakubaliana nasi. Gaddafi hakutegemea kuwa angepinduliwa kirahisi na haraka vile. Tangu Gaddafi aondolewe madarakani kwa aibu ya aina yake, hakuna aliyefuatia. Je nguvu ya umma imeisha au ni suala la muda kushuhudia bazazi mwingine akifurushwa? Kwa wanaofuatilia kinachoendelea Tanzania hasa mgomo wa Madaktari, lolote laweza kutokea. Hii ni kutokana na utawala uliopo madarakani kuwa dhaifu na hovyo kiasi cha kutumia mbinu za mwituni kutaka kuwanyamazisha Madaktari. Rejea kutekwa na kupigwa na kuumizwa vibaya kwa kiongozi wa mgomo Dk Steven Ulimboka kunaokohofiwa kutendwa na serikali.

Ingawa serikali imejitahidi kutumia mahakama zake hata usalama wa taifa, hali inazidi kuwa out of control. Sasa Madaktari bingwa wameamua kuingia moja kwa moja kwenye mgomo na kuupa nguvu na maana zaidi. Je kwa ubabaishaji na usanii huu serikali itaweza kuwanyamazisha au ni mwanzo wa mwisho wa Jakaya Kikwete rais anayesifika kuwa wa hovyo kuliko yeyote aliyewahi kutawala Tanzania? Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

2 comments:

Anonymous said...

Nenda mkwere nenda ukangoje kutupwa lupango au kupigwa hadi mwisho wa kupumua kama Gaddafi. Go to hell JK.

Yasinta Ngonyani said...

kaaaaazi kwelikweli!!!