Tuesday, 31 July 2012

Tumepata kamanda mwingine


Mnamo tarehe 30 Julai hii, familia ya  Mpayukaji ilijaliwa kupata kamanda mwingine Nkwazi Mhango Jr aka Mpayukaji Jr. aliyezaliwa kwenye hospitali ya Boundary Trail MB. Tunachukua fursa hii kuwafahamisheni wasomaji wetu ambao licha ya kuwa marafiki mmekuwa ndugu zetu. Mtoto, mama na baba wanaendelea salama. Tunawakaribisheni kujumuika nasi wakati huu wa furaha ya pekee kwa kumpata kamanda wetu wa pili.

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni furaha ilioje kumpata shangazi wa "pili" HONGERA SANA TENA SANA. Pia ni furaha kusikia wote mnaendelea vema.

NN Mhango said...

Da Yacinta nashukuru sana kwa salam zako. Ubarikiwe na uendelee na moyo huu na karibu sana kwa kuwa mgeni wangu mara kwa mara ukizingatia kuwa kila ukipita huacha unyayo sawa nami nifanyavyo kwenye uga wako.

Jaribu said...

Hongera sana, Nkwazi! Huyu bwana mdogo atakuwa mtetemesha mioyo, "heartthrob!"

NN Mhango said...

Ndugu Jaribu shukrani kwa hongera zako. Tumuombee maneno yako yatimie. Kila la heri na shukrani kwa kuwa mgeni wangu mara kwa mara ukiacha unyayo kila upitapo ugani.