Tuesday, 31 July 2012

'Kufuturisha' ni aina mpya udini au ufisadi?

Rais Jakaya Kikwete akiongea na wananchi wakati alipowafuturisha huko mkoani Lindi alikokwenda kwa ajili ya mazishi ya shemeji yake.


Wabunge 'wakifuturu' pamoja  mjini Dodoma akiwamo 'shehe'Samuel Sitta.

Miaka ya karibuni baada ya madaraka kuwekwa maji na kuchakachuliwa, umezuka mtindo wa viongozi wa serikali walio waislam na wasio waislam,makampuni ya biashara na wenye nazo kufuturisha ima wananchi hata viongozi wao. Kfuuturisha huku ni kwa ajabu kidogo. Maana hakujali dini. Kidini, wanaopaswa kufuturu ni waislam tena waliofunga. Lakini siku hizi utasikia rais akifuturisha mawaziri bila kujali kama wamefunga ni waislam au la. Utasikia shirika fulani au kampuni hasa ya biashara yakifuturisha wananchi. Je huu ni udini au aina mpya ya ufisadi au tuseme ufisadi wa kiimani? Je watanzania wanahitaji futari au haki zao na huduma stahiki yao? Je watanzania wana njaa kiasi cha kuonekana kama wenye kuhitaji futari tu na si haki zao?Je wale ambao si waislam wanafuturu nini na kwa dini gani iwapo hawafungi wala kuamini katika imani husika? Je nani hapa anamdanganya au kumtumia nani? Je pesa inayotumika kununua na kuandaa futari hasa zile zinazotelewa na viongozi kama wa rais zinatoka mifukoni mwao au kwenye kodi ya watanzania ambao nchi yao haina dini ingawa wao wana dini?

3 comments:

Anonymous said...

Aliyekwambia kuwa lazima wanaofuturishwa wawe Waislamu ni nani?
au lazima wawe wamefunga.
Huo ni mwaliko umefunga hujafunga hilo si tatizo la mwalikaji
hata wewe kama una nja njoo ufuturu mwezi bado haujesha

Anonymous said...

Hata mimi nashanga kwani hakumwona Mkuu wa Mkoa mhe ludovik na wa chungaji kibao waliohudhuria sasa
hapa tatizo lipo wapi?
punguza bangi a.k.a.unga

Anonymous said...

Aende na Pemba Akaone.