Sunday, 8 July 2012

Madai ya CHADEMA ni mazitoChama cha Demokrasia na Maendeleo kimefyatua shutuma juu ya uwepo wa mpango wa kuua viongozi wake waandamizi. Waliotajwa katika njama hii chafu ni Usalama wa Taifa ambao kimsingi umegeuka Uhasama wa Taifa. Genge hili nyemelezi limekuwa likitumiwa na viongozi wahuni kuwadhuru watu wasio na hatia. Ni genge hili linalodaiwa kumteka na kumtesa hata kujaribu kumuua kingozi wa mgomo wa Madaktari Dk Steven Ulimboka. Wanaofuatiliwa kwa karibu ili wauawe ni Mbunge wa Ubungo John Mnyika ambaye hivi karibuni alilichachafya bunge kwa kudai kuwa rais Jakaya Kikwete ni dhaifu. Mwingine ni katibu mkuu  Dk Wilbrod Slaa. Wengi wanajiuliza mantiki ya kuwa na genge la kijambazi linalotafuna kodi yetu na kutumiwa kama nepi. Kwa habari zaidi kuhusiana na tuhuma hizi BONYEZA hapa.

3 comments:

Anonymous said...

UZUSHI.Abrakadabra mazingaobwe.
vibaraka wa chadema wala matapishi ya SABADO

Anonymous said...

Mr. Umesikia madai ya upande mmoja tayari unaanza kutumia lugha chafu against these guys!

My take! CDM walikuwa na mipango michafu SANA against humanity kwa kuwezeshwa na wajomba zao (...names reserved..) baada ya kuona wanakwamishwa na taasisi hiyo ( ndiyo wajibu wao, kuzuia mbinu zozote chafu against Tanzanian public) wameamua kuzusha tuhuma hizo. Ni aibu kwa viongozi wa chama hicho cha siasa.

Watsonnejg said...

Mr. Umesikia madai ya upande mmoja tayari unaanza kutumia lugha chafu against these guys! My take! CDM walikuwa na mipango michafu SANA against humanity kwa kuwezeshwa na wajomba zao (...names reserved..) baada ya kuona wanakwamishwa na taasisi hiyo ( ndiyo wajibu wao, kuzuia mbinu zozote chafu against Tanzanian public) wameamua kuzusha tuhuma hizo. Ni aibu kwa viongozi wa chama hicho cha siasa.