Friday, 27 July 2012

Viongozi wa namna hii sijui kama wana akili sawa sawa?Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kaja na mpya. Eti ametoa amri kwa mamlaka ya Zanzibar kuhakikisha pesa ya kununulia meli kubwa yenye uwezo wa kubeba abiria 1,000 na tani 100 za mizigo ndani ya wiki moja. Je hii maana yake ni kwamba serikali inafanya kazi kwa nguvu ya soda au inakurupuka? Je huu siyo mwanya wa kwenda kupata mikopo yenye masharti ya kinyonyaji ukiachia mbali wajanja wachache kutumia mwanya huu kujinufaisha? Je huku ni kutatua tatizo au ni kuwa sehemu ya tatizo? Viongozi wa namna hii wana akili sawa sawa au ni miradi yao ya sirini?

1 comment:

Anonymous said...

Pongezi sana tuu Mheshimiwa Rais.
Angalau tupate usafiri wa uhakika.
sisi tunajuwa Serikali ya unguja inazo pesa za kununua cash hiyo meli.
ila alkher fi batini shar
wiki mbili mchuma unaingia bandarini.
usije ukawa dhaifu