Wednesday, 18 July 2012

Syria mambo yaanza kumgeuka Bashar


Taarifa za kuuawa kwa maafisa watu (Pichani)  wa karibu na wasaidizi wa Rais Bashar Asaad wa Syria ni ushahidi kuwa mambo yanazidi kuwa magumu kwake. Kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza BBC, maafisa watatu wa karibu wa Bashar akiwamo shemeji yake wameuawa na waasi wa nchi hiyo. Bahati mbaya zaidi waliouawa ni maafisa wa juu wa usalama wa serikali ya Bashar ambayo kwa muda sasa imekuwa kwenye mchuano mkali baina yake na wapinzani wanaotaka aachie ngazi. Wengi walidhani Jumuia ya Kimataifa ingefanya kile ilichofanya nchini Libya ili kuepusha umwagikaji mkubwa wa damu. Lakini wapi? Mamia ya watu wameuawa huku Jumuia ya Kimataifa ikiangalia pamoja na kupeleka waangalizi. Sasa Wasyria wameamua kumung'ao imla wao wenyewe baada ya kuona wamesalitiwa na Jumuia ya Kimataifa. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

No comments: