Magufulification: Concept That Will Define Africa's Future and the Man Who Makes Things Happen

Magufulification: Concept That Will Define Africa's Future and the Man Who Makes Things Happen

Thursday, 23 April 2009

Tambwe Hiza, tunda la ukabila linaloulaani

TAMBWE Hiza, mwanasiasa nyemelezi na kiruka njia wa kisiasa, amejitokeza tena hivi karibuni baada ya kunyamaza kwa muda alipogundua kuwa kumbe ameingia CCM baada ya kushindwa ubunge Temeke.

Hiza inaonekana hajui. Watu wanamjua kuliko anavyodhani. Amevishutumu vyama vya upinzani kuwa ni kama kampuni binafsi. Ameenda mbele zaidi na kudai vyama vya upinzani vina ukabila.Kwanza ni uvivu wa kufikiri kudai vyama vyote vya siasa vina ukabila. Pili, ni kweli Hiza ana udhu wa kuongelea ukabila wakati ni ukabila huo huo uliomsukuma katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, kumpachika kwenye ofisi ndogo ya CCM Lumumba na kumfinyangia Kitengo cha Propaganda ambacho hakipo kwenye katiba ya CCM?Kwa mtu anayemjua Hiza kuwa ni 'mganga njaa' na kizabizabina, kwanza anashangaa alikopata mshipa wa kulaani ukabila wakati yeye ni tunda na matokeo ya ukabila ndani ya CCM.

Hiza anasema vyama vya siasa ni sawa na kampuni za watu binafsi ambazo hata hivyo hakuwataja. Lipi bora, kampuni binafsi halali au kuwa chama cha mafisadi kama chama chake kinavyojulikana?

Kama kuna chama ni kampuni ya watu binafsi si kingine bali CCM ambayo mafisadi kama mkuu wa Kagoda, Rajabu Maranda, Peter Noni na wengine wanaotuhumiwa kukitumia kuliibia taifa fedha kutoka Benki Kuu chini ya ujambazi ujulikanao kama EPA.Hiza alikaririwa akisema; “Sisi kama CCM tumeshuhudia kuwapo kwa migogoro mingi ndani ya vyama vya upinzani, migogoro hiyo inakihakikishia ushindi chama, lakini kikishinda vyama hivyo vinaanzisha minong’ono ya kutokubaliana na ushindi wakati hawako makini”

Hiza anaonekana 'kihiyo' au tuseme 'Chitalila'. Hajui CCM kwa sasa ndiyo chama kilichogawanyika kuliko vyote chini ya ufisadi-ufisi na uroho uitwao mitandao?

Hajui CCM sasa ina wanachama rangi mbili kama dawa ya lisilotajika gazetini - yaani CCM safi na CCM mafisadi au wachafu?

Kama CCM haina migongano, inakuwaje zitoke kauli za kukwaruzana kutoka kwa vigogo wake kama ilivyotokea juzi kwa Anne Kilango-Malecela, alipodai viongozi wa CCM hawapambani na ufisadi kwa sababu wananufaika nao. Hii ilimkera katibu mkuu na bosi na mfadhili wake Hiza, Makamba, kiasi cha kusema atajibu mapigo muda ukiwadia.

Huu ni nini kama si mgongano?Pia aangalie mgongano baina ya Dk. Harrison Mwakyembe akisimamia upande wa CCM safi na Rostam Aziz upande wa pili. Hiza aliongeza kuwa vyama vya upinzani hasa CHADEMA, CUF, TLP na UDP vinaendeshwa kwa fedha za walipa kodi maskini na kwa hiyo migogoro ya ndani inapotokea, inapoteza nia njema ya walipa kodi ya kutaka mabadiliko ya kidemokrasia.

Hiza amesahau hata CCM inaendeshwa kwa pesa ya walipa kodi hao hao maskini lakini inazitumia vibaya kuwafuga mamluki na waganga njaa kama yeye? Vyama vya upinzani visingekuwa vinamdharau Hiza, vingemfungulia mashitaka avitaje vyama vinavyoendeshwa kikabila na vile ambavyo ni makampuni ya mfukoni na wamiliki wa makampuni hayo.

Kwa vile Hiza hawezi kula bila kujikomba na kudanganya, vyama vya upinzani vinamchukulia kama kasuku anayeendeshwa na tumbo badala ya kichwa. Bahati nzuri, hata wananchi wanamfahamu tangu alipokuwa CUF akirusha madongo kwa CCM. Wanajua maneno ya Hiza ni matapishi yake mwenye.

Binadamu hali matapishi yake bali mbwa.Baada ya kuukosa ubunge na kuwa na kisomo kidogo kiasi cha kutoweza kufaa kuajiriwa, alijirejesha CCM kama mnyama fulani afanyavyo baada ya kudokoa kwa aliyemfuga. Siku zote nimekuwa nikitahadharisha kuhusiana na siasa za ukuku, ufisi na uumbwa. Kuku hula asichozalisha na kuzalisha asichokula.

Hiza anazalisha migongano na kula pesa ya walipa kodi.Mbuzi huishi kwa masharti kwenye nyumba ya binadamu akichekwa na swala.

Hiza anafugwa na CCM kwa sharti la kupayuka na kuleta fitina kwa wengine.

Aliwahi kukiri alipokuwa Mbeya kuwa alikuwa ni mtaalamu wa CUF wa uzushi, uchonganishi na fitina. Fisi hula chochote hata watoto wake azidiwapo.

Anachofanya Hiza ni ufisi anapowahadaa Watanzania waendelee kuchagua chama nyemelezi na fisadi kwa ajili ya mateso yao na vizazi vijavyo. Kwa kuazima usemi wa marehemu baba wa taifa, Hiza na kundi lake, hata chama chake ni watu wa kuogopwa kama ukoma na pengine kama ukimwi.

Kwa nini Hiza hamwambii mwenyekiti wake aache kuwaangusha na kuwadhulumu Watanzania?

Ametimiza ahadi gani na ngapi tangu aingie madarakani zaidi ya kutumia muda mwingi kufikiri jinsi ya kuua kashfa zinazomkabili, watu wake, chama na serikali yake?Ziko wapi nyumba za Watanzania zilizoibwa wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa na mkewe, na wote waliokuwa kwenye serikali yake akiwamo mwenyekiti wake?

Yako wapi mapambano dhidi ya ufisadi, kufufua uchumi, kuleta nidhamu ya matumizi ya pesa za umma zinazoharibiwa kwa kuwalipa wapiga debe wachumia tumbo kama Hiza na wenzake?Iko wapi safari ya Kanani?

Iko wapi kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya ambayo badala ya kuendeleza na kutawala nchi imeelekezwa kwenye kuiibia? Kwa vile kisomo na uelewa wa Hiza ni mdogo, hawezi kujua mambo haya. Na kwa vile yeye anaendeshwa na tumbo, mambo yanayohitaji kufikiri hayawezi.

Heri angefunga domo lake kabla ya kuaibika zaidi. Ni kitu kibaya kwa mwanamume mzima kujiingiza kwenye uchangudoa wa kisiasa na usasi ngawira, tena kwa mgogo wa kuwahadaa Watanzania.

Hiza, angekuwa anajua maana ya kampuni za mifukoni za watu binafsi, basi angemwambia bosi wake na chama chake wafunge kampuni zao za Meremeta, Deep Green Finance, Mwananchi Gold, Richmond, Kagoda, WAMA, EOTF, ANBEN, Tanpower, Fosnik na nyingine nyingi. Angewaambia mabosi wake kama Andrew Chenge, Idris Rashid, Maranda, Noni, Mkapa na wengine warejeshe pesa ya umma.

Kwa vile Hiza hana nidhamu na uelewa, atabaki kuropoka mradi wanawe wale. Huu ni udhalili uliovuka mipaka, kwa mtu mzima kutegemea uongo na fitina kuendesha maisha yake.Hata hiyo, ofisi ya propaganda ni kampuni ya Makamba anapoweza kuweka kila takataka aifagiayo kutoka upinzani.

Nasisitiza 'takataka'.
Chanzo: Tanzania Daima Aprili 22, 2009.

Kwa vile baada ya vyama vya upinzani kuwashtukia kuwa wahusika ni makapi huwafagia na Makamba - kama kokoro - huwazoa na kuwajaza Lumumba.Hawa ni wezi wa pesa ya umma watake wasitake.

Hiza acha uhuni na ufisadi, ufikie mahali ukue, uwe mwanamume mwenye tabia za kiume na si vinginevyo kama ulivyo sasa.

Kisiasa na kiakili Hiza unahitaji kufundwa na kupelekwa jandoni.Watanzania mdharauni na kumpuuzia Hiza, kwani mnajua njaa ikipanda kichwani matokeo yake ni kuwa tayari kutumiwa na kila atakaye wa kutumika kama mtumwa Hiza anavyofugwa na CCM.

Kweli nyani haoni kundule.

1 comment:

Anonymous said...

hiza ni shoga,ana maumbile ya kishogo kiakili mpaka kinadharia.waarabu wamuita kama.laarasati nisuani(shaksia).yeye akipewa donge na rostam-aziz..kulonga umbeya atalonga tu huyu ni mwenye njaa ..kama vile shoga akikosa basha basi hata punda atambaka .kwas nyege zake..tanzania ni jalala la wahuni.ma malofa kama huyu msemaji wa chama cha magaidi na majambazi (ccm)time will tell waerevu tupo na media na utandawazi upo karne hii tutapambana nao hata kuwashitaki kwenye mahakama za dunia.kwa kutudhulumu na kutudhalilkisha kwenye nchi yetu..na ole wake mheshimiwa mtawa,ambae yeye ni secretary wa ufisadi wa ikulu..wote tutawafikisha mahakamani kama alivyofikishwa sadam hussein na marekani..bali ummaa wa kitanzania utawahukumu nyinyi na vizazi vyenu mpaka watoto wenu tutawashitaki.ipo siku ya siku