The Chant of Savant

Saturday 10 November 2012

Kwa hili nampongeza rais Bozize

Rais Francois Bozize wa Afrika ya Kati alifanya kitu ambacho kimewashinda marais wengi wa kiafrika. Hivi karibuni aliamrisha mwanae, Kelvin awekwe ndani baada ya kukataa kulipa deni kwenye hoteli moja ya kifahari mjini  Bangui. Sakata hili lilisababisha meneja wa hoteli husika kuwekwa ndani kabla ya baba mtu kuingilia na kumwachia huru meneja huyo.
Viongozi wengi wa kiafrika wamewaachia watoto hata wake zao kutumia madaraka yao bila hata kuwakaripia achia mbali kuwazuia. Kwa hili rais Bozize ameona mbali kiasi cha kujenga picha ya mtu asiyetaka madaraka yake kuwa mali ya familia marafiki au ukoo. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

No comments: