The Chant of Savant

Thursday 19 December 2013

Miaka zaidi ya 50 ya uhuru bado watawala bado wanatibiwa nje!


Ni hivi majuzi Tanzania na Kenya zimesherehekea zaidi ya miaka 50 ya uhuru wake. Siku chache baadaye taarifa zinakuja kuwa rais Jakaya Kikwete anakwenda Marekani "kuchekiwa" afya yake. Hii maana yake ni kwamba miaka yote zaidi ya 50 ya uhuru haijatupatia hospitali ya kuweza kuwachunguza watawala wetu. Pia miaka hii yote haijatupatia viongozi wanaoweza kujiamini na kuamini katika huduma zinazotolewa na serikali zao. Hii imenikumbusha kisa cha mama ntilie aliyekuwa akiagiza chakuka hotelini kila ikifika saa ya chakula huku akiwauzia wateja wasiojua uchafu na hatari ya chakula chake. Rais anakwenda nje kuombaomba na kuchekiwa afya yake. Ajabu huyo rais asiyeamini usalama wa huduma zinazotolewa na hospitali zinazosimamiwa na serikali yake anawadanganya wananchi kuwa wako sawa na anaipenda nchi yake. Ni unafiki na uhovyo kiasi gani? Mandela alitawala miaka mitano si hamsini. Alihakikisha kila kitu walichoacha makaburu kinaendelezwa kiasi cha kufia nchini mwake bila kwenda kujiaibisha ughaibuni kama hawa. Marais wetu wataendelea kutibiwa, kuchekiwa afya na kufia nje hadi lini? Je hii ni laana kwao kwa kuendekeza ubinafsi,wizi, ufisi, ufisadi na uzururaji hadi afya zao wanaziweka rehani ughaibuni? Je nini yatakuwa matokeo ya uchunguzi huu? Tutegemee yale ya Jangwani au zaidi?Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

2 comments:

Anonymous said...

hayo ndiyo maendeleo kwa viongozi waafrika tena wanaona ni fahari kufanya hivyo wakati.

walalahoi wanatibiwa zahanati zile za Manzese kwa mfuga umbwa na Uwanja wa fisi bila kusahau,

Mgonjwa mhuhimbili hospitali kulazwa chini sakafuni ni sehemu ya adhabu ya kuugua.

Kule kwetu Mbagala ndiyo husiseme zhanati zetu ni hatari kwa afya maana kila kitu feki kuanzia jengo,daktari anayekutibu, dawa unazotumia.

Hii ndiyo sababu sisi(NN nawe unatokea huku??) kule kwetu mbagala tunatumia zaidi miti shamba na kupiga ramli.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon usemayo ni ukweli ila yanauma na kusikitisha. Bahati mbaya zaidi ni hawa hawa wasaliti na matepeli wanaotuaminisha kuwa wako madarakani kwa maslahi yetu wakati ni wizi na ujambazi mtupu. Hivi akifia mtu huko nje watu wakasherehekea waambiwe weanga siyo? May they perish.