Hivi
karibuni waandishi wa habari walimbana waziri wa fedha Dk. William
Mgimwa kueleza ni kiasi gani cha fedha kimesharejeshwa na majambazi wa
EPA. Mgimwa alijikanyaga na kshindwa
kutoa jibu sahihi na badala yake alikaririwa akisema, “Kwa sasa siwezi
kuwaeleza ni kiasi gani kimerejeshwa hadi nipitie mafaili ndipo ninaweza
kutoa jibu sahihi.” Sitegemei kama kuna siku Mgimwa atawaita tena waandishi wa habari awape hizo taarifa anazodai kwenda kuzihakiki ofisini kwake. Kwa
mtu asiyetafuta kujaza tumbo lake, kwa nafasi yake asingekubali ufuska
huu wa EPA. Ila kwa vile anayetafuta kujaza tumbo lake ni suala jingine.
Hata
hivyo, waandishi wa habari licha ya kumchokonoa na kutaka kumuaibisha
Mgimwa walimuonea. Nani aongelee EPA iwapi mtuhumiwa mkuu aliyedaiwa
kutumia fedha ya wizi wa EPA kutafutia madarakani amekuwa akiogopa
kugusia suala hili na kuliogopa kama ukoma? Mgimwa angekuwa mtu safi
basi angegoma kupokea pesa hiyo na kushauri wahusika wafikishwe mbele
ya vyombo vya sheria. Kwa vile lao ni moja ameamua kunywea na kuwa
msemaji wa uchafu huu.
Kwa
matendo ya watu wanaoitwa wasomi tena wenye shahada za uzamivu kama
Mgimwa kufanya vitu vya namna hii, ni ushahidi kuwa kumbe kusoma si
kuelimika. Inashangaza ni kwanini mtu mwenye hadhi hii kisomi kukumbatia
upuuzi usioweza kukumbatiwa na hata mbwa aliyendaye lindo bila malipo?
Tunazidiwa na hata hayawani wanaujua ukweli kuliko sisi. Wanatuzidi hata
mahesabu raisi kwa kujua kuwa mwizi si mtu wa kushirikiana naye. Siku
moja rafiki yangu aliniacha hoi aliposema eti aliposema kwa kukata
tamaa: Laiti mbwa angejua kusoma na kuandika akaaminiwa benki kuu yetu
kuliko wasomi wa hovyo kama hawa
wanaofanya mambo ambayo hata mnyama hawezi kutenda achia mbali mjinga.”
Hii ilinikumbusha swali la : Nani anaweza kuamini kuwa mjinga aliyeitwa
msomi tena Daktari kama Daudi Balali angeingizwa mkenge na wajinga
wachache akaamua kusaliti kiapo cha kazi yake? Ajabu wajinga hawa hawa
wanaendelea kuwahenyesha wale tunaodhani ni wasomi kumbe bure.
Sikujua
kuwa bado ujambazi wa EPA unaendelea. Yaani nchi inayojisifia utawala
wa sheria bado inaendelea kulala kitanda kimoja na mafisadi kwa kuwataka
warejeshe chumo la wizi badala ya kuwafunga? Je ni kweli pesa hiyo
inarejeshwa au ni danganya toto? Je ni kwanini wezi hawa wanaorejesha
fedha hawawekwi wazi ili umma uwajue hata kama serikali imeamua kulala
nao kitanda kimoja? Je serikali inayowaficha kwa sababu
inazojua inaweza kuwanyang’anya tonge mdomoni au ni kuendelea kutufanya
hamnazo?
Je
hawa ni akina nani wenye uwezo wa kuilazimisha serikali kufanya
wanavyotaka hata kwa kupinda sheria? Je hawa si washirika wa serikali?
Serikali inayoficha majina ya wezi wa fedha za umma inaweza kufichua
majina ya wauza unga kweli?
Je
Mgimwa anaridhishwa na kitendo hiki cha jinai cha wezi kurejesha fedha?
Je kufanya hivyo hakumfanyi Mgimwa kuwa mwizi kama wezi anaowakubalia
kurejesha chumo la wizi? Maana sheria iko wazi kuwa asirikianaye na
mhalifu naye ni mhalifu
na adhabu yao ni ile ile iwe ametenda au kushiriki kwa namna yoyote. Je
hawa si mibaka tunaoalalamikia ambao wana uwezo wa kuiba na kulazimisha
serikali iwalinde? Je namna hii nchi iko salama mikononi mwa majambazi
kama hawa? Ukimuuliza mwanasheria mkuu wa serikali na hata mwendesha
mkuu wa mashtaka wa serikali na TAKUKURU juu ya ujambazi huu utagundua
jinsi huu ulivyo mchezo wa kuigiza. Wanatupotezea muda kupambana na
vidagaa wakati wakifua nepi za majambazi wa kubwa. Kwangu wote naona ni
wezi tu hata kama wana madaraka.
Tukisema
serikali ya Kikwete ni ya ubia kati yake na mafisadi hata majambazi
tunaambiwa tunamchukia. Nani anaweza kueleza mantiki ya Kikwete kutoa
‘amri’ kwa wezi tena wa mabilioni ya umma warejeshe chumo la wizi? Mbona
hawaambii
wezi wa kuku kurejesha kuku? Je tangu lini Kikwete akawa hakimu au jaji
kama si ufisadi wa kunuka? Nani hajui kuwa kwa mfano Kagoda iliishia
mlangoni mwa mshirika na swahiba mkuu wa Kikwete aitwaye Rostam Aziz na
hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi yake? Nani hajui kuwa hata Richmond ni
Rostam Aziz huyu huyu na hakuna anayethubutu kumgusa? Wapo wanaodhani
kuwa kuna ufisadi mwingine unaoishia kwa mtu huyu huyu haujawekwa wazi.
Wapo wanaodhani kuwaRostam si bosi wa Kikwete. Wapo wanaotamani Kikwete
ajitete ili kutua zigo hili ambalo limemng’ang’ania shingoni miaka yote
ya utawala wake. Je Kikwete anaogopa nini kujitetea kama hakuna namna?
Je kuna siri ambazo Kikwete asingetaka ziwekwe hadharani. Wapo wanaoona
kama habari za EPA ni kaa la moto hata kurugenzi yake ya propaganda za
kichovu haiwezi kuligusa bila kumuunguza bosi wao. Natamani waandishi wa
habari wazidi kumchimba Mgimwa ili tuone kama atakuwa na jipya
kuhusiana na kashfa ya
EPA.
Chanzo: Dira Desemba, 2013.
No comments:
Post a Comment