How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Tuesday, 18 February 2014

Kijiwe: Landani uwe mji mkuu wa Bongo


BAADA ya kijiwe kugundua kuwa mkuu anapata sana taabu kukesha kwenye pipa akienda kueleza na kupokea sera kule Landani, kimependekeza Landani uwe mji mkuu wa Bongo.
Leo hakuna maroroso wala ronga ronga. Tiende ku nchito, Mijjinga anaingia akiwa amebeba makabrasha yake kama kawa. Anaamkia na kukaa. Akiwa anabofya bofya kisimu chake analianzisha: “Waheshimiwa wanajikiwe, mlisikia kuwa mkuu amekwenda Ulondon kushiriki kampeni ya kutokomeza ujangili?”
Msomi anajibu bila hata kumtazama Mijjinga usoni: “Wadude wauawe Afrika kampeni Ulondon siyo? Tutaacha lini visingizio na uzembe jamani?”
Mpemba anakatua mic: “Huenda kule ndiko wanakouza hayo meno na pembe.”
Mgosi Machungi anakwanyua mic: “Ami tiambizane ukwei tieewe. Hii kitu inauzwa China na India kama hatikosei.

“Basi hizo kampeni zingefanyika kule yakhe. Je, inakuwaje nkuu ende Ulondon badala ya kwenda lau mbugani?” Anajitetea Mpemba.
Mbwa Mwitu anaingilia kwa utani: “Hujui siyo! Matanuzi baba. Makamuzi baba.”
Kanji anaamua kukwanyua mic: “Nyinyi Swahili vipi? Kuu kwenda London soma juu ya tunza nyama. Maana koloni natawala nyinyi naleta sisi  natunza wanyama nyinyi tawala na kula nyama yote dugu yangu!”
Mgosi Machungi kaguswa pabaya. Anakwanyua mic: “Tiseme ukwei Kanji amesema ukwei. Sisi tinakulana na kula wanyama bado titakula nyasi.” Kanji anakenua na kusema: “Mwagia yeye.”
Kabla ya kuendelea Mgosi anamshika begani, na kusema: “Chonde chonde Kanji angaia unakwenda pabaya. Yaani wewe ni wa kumwambia kijana huyu animwagie? Hujui kahawa inaweza kuniunguza vibaya?”
Kapende anaokoa jahazi kwa kuchomekea akisema, “Tule nyasi mgosi? Hukuona juzi kwenye runinga tapeli mmoja huko Sauzi akiwalisha watu nyasi kama mbuzi akidai ndiyo neno la Mungu?”
“Hebu tuwe serious jamani,” anasema Msomi huku akibwia kahawa yake na kuendelea: “Huwezi kuondosha ujangili kwa kukutana na wakoloni huko Ulondon. Sana sana wanakucheka na kukuona hamnazo.
Leo tutaelekeza mapambano ya kuteketeza ujangili huko Ulondon wakati wanyama wenyewe wanapitishwa kwenye viwanja vyetu vya ndege tena wakiwa hai. Are we serious really?”
“Yakhe usinkumbushe hili. Mie naona hata mikakati ya kupambana na bwimbwi tutafanyia huko Ulondon.”
Kijiwe hakina mbavu jinsi Ami anavyotamka Ulondon.

Msomi ameamua kutoa shule leo. Anakwanyua mic na kudema tena, “Nadhani watawala wetu siku watakayokuwa serious tutajikomboa. Mwaka jana tu mkuu alikwenda London mara mia kidogo. Alikwenda kwenye mkutano wa uwazi, uzazi wa mpango na sasa wa kupanga ujangili.”
Kabla ya kuendelea Kanji anaamua kujivua nguo kwa kusema: “Kwanini nyinyi penda kosoa kuu? When he goes there hupewa saada nyingi na saada nasaidia nyinyi lakini bado lalamika tu dugu yangu.”
“Unaongelea Saada Mkuyati au Saada yupi?” Anachomekea Mbwa Mwitu.

Sofia Lion Kaungaembe anaamua kumhami mshirika wake Kanji kwa kusema: “Nawe umezidi.” Anaongea akiwa amemkazia macho Mbwa Mwitu anayejibu haraka, “Njoo unipunguze au unipunguzie.”
Kanunga anaendelea: “Kuna ubaya gani kwa mtukufu kwenda kuomba misaada au kujadili kupanga uzazi?”
Kapende anaingilia haraka: “Sofi kawambie wajinga wenzako huo utumbo. Nani ahudhurie mkutano wa uwazi au kupanga uzazi wakati yeye mwenyewe hapangi wala hayuko wazi?”
“We Kapende we Kapende. Yaani unatakaga mkuu awege wazi na apangege uzazi?”
“Ndiyo. Si hilo tu. Apange uzazi pia. Maana kwa umri wake sikutegemea awe na vitegemezi vinanyea nepi au kusoma vidudu wakati anapaswa kutukuu achilia mbali kujukuu,” Anajibu Kapende huku akimpa sigara kali Mgosi Machungi.

Mchunguliaji anaamua kukwanyua mic: “Hebu tuwe serious,” anamkata jicho la furaha Msomi na kuendelea: “Hivi jamaa ana vitegemezi vingapi?”
“Kwa nani?” Anauliza mzee Maneno.

“Si kwa bi mkubwa wa Ma-ngo,” anajibu Mchunguliaji.
Mzee Mdomo aliyekuwa akiangalia anaamua kujibu: “Hiyo ni top secret tena ya usalama wa taifa.”
Mgosi Machungi anaamua kutia guu tena. “Weee done mgosi, I didn’t know that you know ingiishi this way!”
‘Du Mgosi unatema ung’eng’e kwa Kisambaa. hawasemi wee done wanasema wello dani. Pia hawasemi ingiish wanasema inglishi.” Anachomekea Mchunguliaji.

Machungi anajibu mapigo: “Kwai hujui Kisambaa na Kiingeeza ni mapacha!”
Baada ya Msomi kuona utani unaanza kuingilia kati anaamua kurejesha mada kwenye mstari. Anasema: “Nimependa sana wazo la kufanya Ulondon kuwa mji mkuu wa Bongo ili kumuondolea usumbufu mkuu. Pia ningependekeza Davos uwe mji wa kibiashara au vipi?”
“Yakhe usiniambie mambo ya Davos. Jamaa wenda kila mwaka kutumia na kutanua waja wakituongopea eti wenda kutafuta jinsi ya kuondoa umaskini. Maskini wakubwa. Wawezaje ondoa umaskini wakati watumia hata bila kufikiri?”
“Seriously, huenda tukifanya hiyo miji kuwa makao makuu yetu rasmi tutaokoa pesa nyingi inayotumika kwenda huko na kutufanya maskini,” Anazidi kutetea hoja yake Msomi.

Kapende ambaye anaonekana kuna dili analifuatilia kwenye simu anaamua kukwanyua mic: “Nakubaliana nawe Msomi mwenzangu.” Kabla ya kuendelea anaangalia huku na kule na kukuta kina mzee Maneno wakikonyezana kwa kujiita msomi. Hajali anaendelea, “Mie napenda makao makuu ya Takokuru yawe Washington ili FBI itumike kupambana na magamba, ufisadi na hata ujangili.”
“Mie naona hata makao makuu ya Benki Kuu yaani BoT yaani Belly Of Tembo yawe Uswizi ili kutuepusha na mapresha yatokanayo na kujua mauza uza na ujambazi kama EPA au vipi?” anauliza Mijjinga huku akiangalia saa yake.

“Basi na makao makuu ya TRA yawege Jersey na mkuu wake awe Anderea Chenge huku Rostamia Azizi akiwa waziri wa njuluku ili tuzalishe mabilionea wengine wengi.”
“Loo! Mijjinga umesahau. Pia tungefanyaga mpango makao makuu ya Wizara ya Afya yawe Bombhai na waziri wa afya awe Rama Murder-bidder au vipi beng’we?” Anachomekea Mipawa.

Kijiwe kikiwa kinanoga si mdege wenye mafua wa mkuu ukapita juu yetu ukielekea Ulondon. Acha tuurushie mitusi na mimawe. Huku huku tunaona ndata wanakaa mkao wa kumwangosi mtu. Tunaamua kujikata kislesi taratibu.
Chanzo: Tanzania Daima Feb. 19, 2014.

6 comments:

Jaribu said...

Natamani kjiwe kitamke rasmi kuwa JK ni kifupi cha Jamaa Kachemsha au Juha Kalulu!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

We Jaribu! Kijiwe kinamheshimu Njaa Kaya hata kama hajiheshimu. Kikitamka hivyo kitampa ujiko wa kutangaza kuWa uvumilivu sasa mwisho.

Jaribu said...

Au vipi? Maana kwa visingizio ndiyo hajambo.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Kumbe unamjua vizuri! Tusimnasue kwenye mtego alikojitundika kwa irresponsible utterance.

Jaribu said...

Labda na wakati mwingine huwa tunatemea sana uwezo wa hawa viongozi wetu, high expectations kama wanavyosema wenzetu. Kwa mfano juzi nilikuwa naangalia kipindi kimoja cha wana historia ambao walikuwa wanampigia kura raisi uozo katika wote Marekani. Waliokuwa kwenye list walikuwa Andrew Jackson, mbaguzi wa rangi na muuaji wa Wahindi Wekundu, Herbert Hoover aliyekuwa madarakani wakati wa Great Depression, Nixon wa kashfa ya Watergate, George Bush na wengineo. George Bush alichaguliwa kuwa kutokuwa na uwezo wa uongozi, kuanzisha vita, kuwapa misamaha ya kodi marafiki wenzio na last but not least, upeo mdogo.

Na wakati wa utawala wake waliokuwa wakimwita George Bush mjinga walikuwa wanaonekana si wazalendo, lakini leo kila mtu anakubali kuwa Bush kazi hakuiweza. Siyo kila mtu ana kipaji cha uongozi. Ndio maana mimi sihamaniki nikisikia Don Giacchia amepayuka tena, kwa sababu sitegemei chochote kingine. Swali langu daima linakuwa, "What else is new?"

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Methinks what's new is to unearth new and hidden characteristics of our quacks that we wrongly call leaders. Don can jabber as many time as he likes. Our mongrel can't be touched. Don't refer to him as a goon of dunderhead. After he vacated all stones will be turned and those who used to worship and lick his rump will be the first ones to call him names believe ye me.