How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Wednesday, 5 February 2014
Iwe Rwiyemaaamu unafwikiri tutaacha kujadili mizigo?
BAADA ya juzi kujadili CV ya Saaada Mkuuuya Saalimu, kijiwe kilipata salamu toka kwa mtu wake wa karibu akiomba tumhifadhi. Nasi tuliwatuma wamwambie kuwa kazi yetu si nepi wala gagulo kumhifadhi mtu.
Tutamfichua yoyote atakayetaka kutuhujumu kama jamii. Ndiyo maana wanakijiwe huwa hatuna simile na yeyote.
Leo hii kijiwe kimeamua kumshukia fisadi mmoja wa kimawazo aitwaye Silva Rwiyependekezamu. Ambaye kwa ufupi huitwa Rwiye.
Naona mgosi Machungi anaingia akiwa na ndita usoni. Si bure lazima kuna jambo, tena kubwa limemuudhi.
Anatuamkua: “Asaaam aikum wagosi.” Tunaitikia: “Wa leykum ssalaam.”
Mbwamwitu anachokoza kwa kujibu: “Alaina wa Alaikum.” Mgosi anamdharau wala hampuyukii.
Msomi Mkatatamaa anauliza: “Mgosi mbona umekunja ndita kunani ndugu yangu?”
Mgosi anajibu: “Leo nina hasia ya kuua mtu. Hivi ukumisikia yue kanjanja Saiva Rwiyemaaaamu akisema eti tisiongee mizigo ya bosi wake aiyotutwisha kana kwamba hatiumii!”
“Alaa kumbe unaongelea huyu msaliti na mchumia tumbo anayefanya kazi ya unepi kwa jamaa! Huyo nshamdharau miaka mingi. Tangu lini mtu anayefikiri kwa utumbo akawa na mantiki Mgosi?”
Mpemba anakwangua Mic: “Yakhe huyu jamaa nshenzi sana. Hajui kuwa kulalamika ni haki yetu kikatiba? Basi aambwe na afahamu kuwa hatutaomba ruhusa mtu wala nani.”
Kapende anaidaka mic hata kabla ya Mpemba kuitua na kuzoza: “Huyu jamaa mpuuzi kweli kweli. Yaani hata kama mizigo inaendelea kutuelemea na kutunukia tusilalamike? Au hawa ni kwa vile nao ni mizigo ndiyo maana wanatetea mizigo kwa vile hawajui ilivyo mizito? Akome na akomae hata kama amekataa kukua.”
Mijjinga naye hajivungi. Anakatua mic: “Beng’we hili li Rweyependekezamu lingenyamazaga kabla hatujalitia makofi. Jitu limeishiwa God knows. Huwa nadharau jitu linalosaliti taaluma yake na kwenda kuendekeza njaa hadi linageuzwaga nepi.”
Mzee Kidevu anamnong’oneza mzee Maneno kuhusu Mijjinga anavyobukanya Kikameruni.
Naye Mijjinga kagundua na kuendelea: “I swear to God. One day I will nyonga somebody.”
Kijiwe hakina mbavu jinsi Mijjinga anavyochanganya Kikameruni na Kiswahili.
Mbwamwitu anaamua kuingilia kwa utani. “Mzee Mijjinga naona ng’eng’e lako la mama haswa.”
“Ulikuwa hujuagi kuwa mimi naongea Queen English! Basi nimeamua kuchanganyaga ili wote wajue. Kama huyu mzushi aliyetaka kututisha aliongea Ukameruni kwanini sisi tusimjibu akajua tunajua kuliko anavyojua?” Anajibu Mijjinga huku akijifagilia.
Kanji anajitia urweyependekezamu naye. Anasema: “Mimi jua ili bana iko soma Britain na naongea good English.”
Mzee Maneno anaamua kukwanyua mic: “Tushazoea mawazo yenu mgando. Mbona Wachina hawaongei hiyo guudu ingilishi na bado wanaendelea?”
Kanji hajivungi, anakwanyua mic na kuchonga: “Veve iko compare Chinese na Danganyika. Acha tani bwana. Chinese iko viumbe ya juu sana.”
“Kanji acha ubaguzi wa kipumbavu. Baada ya kusema China iko viumbe ya juu utasema gabacholi iko viumbe ya juu pia kwa sababu iko kuja hapa honga mizi kuba yetu pata tenda hata pesa ya EPA.”
“My friend hapana mimi pumbaf wala shiriki iba pesa ya EPA. Hata ile Hindi naachiwa na tukufu juzi siyo dugu yangu. Dugu yangu nyinyi hapa.”
Kijiwe hakina mbavu Kanji anavyotaka kutuhadaa kuwa sote ni dugu wakati dugu yake ni fisadi yenye daraka.
Bi. Sofi Kanungaemba lazima ampe tafu mshikaji wake Kanji. Anakwanyua mic na kuzoza: “Kanji wapashe wapashike. Wanaosema kuwa mheshimiwa Silva hajui kimombo wana vichaa. Angekuwa hakijui angepewa usemaji wa Kurungezi?”
“Sofi umeingiliwaga na nini dada yangu? Mimi nilimsikia akibukanya na kuchanganya kiswangilish akisema eti kaya inapaswa ku-move forward. Hii ina maana gani? Bosi wake mwenyewe hakimanyi kama Nchonga itakuwa yeye?”
Msomi anagundua kuwa maongezi yanaanza kuhama toka kwenye mada kwenda kwenye kujadili watu. Anakunywa kahawa yake na kunyoosha vidole vyake na kusema: “Waingereza husema, healthy minds discuss philosophy. Sick minds discuss personalities. Yaani akili zenye afya huongelea falsafa na masuala. Akili zilizougua hujadili watu. Nasi tusijadili huyu Rwiyemaaamu bali alichosema ambacho ni kutaka kutunyamazisha.”
Kabla ya kuendelea Mpemba anadakia: “Yakhe hapo nimekupata uzuri. Ndiyo, twapaswa ongelea masaala badala ya huyu kidhabu ati.”
Mgosi Machungi anakwanyua mic na kulonga: “Tikubaiane. Huyu Weyependekeza azima ajipendekeze ndipo mkono uende kinywani. Muhimu timwambie hata bosi wake aliyetitwisha mizigo yake kuwa hatinyamazishwi na hatiogopi mtu. Kwani mbwai mbwai bwana?”
Kapende anadandia: “Hakuna huyu mpuuzi aliniacha hoi kusema eti tuache mjadala ili kuwapa nafasi mizigo kuchapa kazi. Wachape kazi gani wakati waliishaivuruga miaka mingi? Mie nawaonea huruma akina Kinamna na Mapepe Ninaye waliotaka kutumia mizigo kuimarisha chama wasijue bosi wao atakifumua.”
“Mie naona Rweyependekezamu hajakosea ati. kama yeye yu nzigo twambeba kwanini asitake tubebe na wenzake kama yeye? Bila shaka haya ndiyo mantwiki alotumia bosi wake kurejesha mizigo ili tubebe. Kwani tukishabeba mizigo hatuwezi jikomboa hata kidogo kwa vile yatuelemea na kutuumiza ati.”
“Ami hujakosea. Hukusikia akisema eti kama rahisi ameona wanafaa basi nasi tuwaone hivyo. Kwani sisi hatuna akili hadi tuamuliwe na mtu ambaye naye ni mzigo kama hao anaowatetea? Maana Waingereza, samahani leo nitatumia maneno ya Kiingereza, husema, show me your friends I will tell you who you are. Au tuseme Waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba. Hivyo, huyu mchumia tumbo ni wa kudharauliwa na kuendeleza mjadala. Kwani kaya hii ni ya rahisi na mizigo yake au wachovu?”
“Msomi nakuunga mkono sana. Sisi ndiyo tinaipa kodi wanayotumia kutanua. Hii kaya ni yetu wala si ya mkuu wala mizigo. Tina haki ya kumijadii yeyote hata kama ni mkubwa.”
Kijiwe kikiwa ndiyo kinachangamka si likakatiza gari la Rweyependekeza. Kila mtu alizoa mitope na kulimwagia huku tukimzomea hadi akatimka huku akiwa anatetemeka kama aliyevamiwa na homa ya ghafla. Ole wake! Siku tukimpata tutamfanya kitu mbaya.
Chanzo: Tanzania Daima Feb 5, 2014.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment