How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Thursday, 22 May 2014

Ujenzi kweli au usanii

Hapa anaonekana akila na mafisadi

Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahaman Kinana ni mtu asiyeishiwa vituko. Kwa nje ni mtu anayejionyesha kama mpenda maendeleo hasa ya watu maskini. Kwa ndani ni mtu wa kuogopwa kama ukoma. Ni Kinana huyu huyu aliyetuhumiwa kutumia kampuni yake kusafirisha nyara za taifa nje anayejifanya kuwajali hawa anaotuhumiwa kuwahujumu. Wapo wanaosema kuwa anautupia jicho urais japo wanaomjua wanaona kama urais umeishiwa maana. 
Hapa anajionyesha kama mtu wa kawaida ila akishaukwaa humuoni
Rais wa Tanzania anapaswa  kutumiza sharti moja kuu kati ya mengi. Awe amezaliwa Tanzania na mtanzania ambaye wazazi wake walizaliwa Tanzania. Wenye kujua historia ya Kinana watupe ili tutafute jinsi ya kumdurusu kuona kama ana sifa za kuwa rais ingawa hili la kujihusisha na ujangili linamtoa nje ya ulingo. Siku hizi ametokea kuwa mtu wa kuikosoa serikali ya Kikwete hasa baadhi ya mawaziri na kujionyesha kama mpenda kusaidia watu wa vijiji na mtu wa watu wakati si kweli. Je anachofanya kwanini anakifanya leo na siyo miaka mingi iliyopita?

5 comments:

Anonymous said...

Hiyo inaitwa kula na kipofu pasipo kumshika mkono ndicho kinachofanywa na CCM, na pia wakifahamua fika hao wapiga kura wao akili zimeganda!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon umesema vyema. Ila nina shaka. Hawa vipofu wasiostuka watastuka lini au ni vipofu na mataahira?

Anonymous said...

Watastuka wakiwa wamezikwa Kaburini!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Wow! Wastuke ilhali wameishafukiwa kweli!

Anonymous said...

Usha ni wa CCM huo
Wanajua Watanzania kuwadanganya
Kweli nitashangaa Watanzania kuichagua CCM 2015