How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Wednesday, 14 May 2014

Kijiwe chastukia na kulaani mfumo wa kikaburu

BAADA ya kunyaka stori kuwa magabacholi wauza bwimbwi wawili waliachia kiasi cha mahabusu kugoma na kuvua nguo, Mbwa Mwitu anaingia kijiweni kwa nyodo akishangilia kuumbuka kwa waongo na matapeli wanaodanganya wachovu kuwa wanapambana na bwimbwi wakati ni washirika wakuu na mawakala wao toka ugabacholini.
“Halo halo! Wanazidi kuvuliwa nguo kila uchao!” Anaingia Mbwa Mwitu akizomea.
Kabla ya kuendelea Mgosi anauliza, “Nini tena na nani hao wanavuana nguo ii iweje?” Anauliza Mgosi Machungi baada ya kumkaripia dereva wa dala dala aliyeturushia tope pale kijiweni kwetu.
Mbwa Mwitu hajibu. Anampa gazeti la Danganyika Always kwenye sehemu isemayo, “Mahabusu wavua nguo kupinga kuachiwa kwa wauza bwibwi.”
Mgosi anachukua gazeti na kusoma haraka haraka na kusema, “Kwei hapa wamevuana nguo hasa mfumo huu wa kikabuuu unaoanza kuzoeeka hapa kayani.”
Mpemba aliyekuwa akishangaa nini kinajadiliwa anauliza, “Yakhe mbona mwafumba kana kwamba hantaki sie tujue mnichoongelea?”
“Ami hatifumbi. Hebu chukua gazeti uone kaya hii iivyogeuzwa ya kikabuu.” Mgosi anampa Mpemba gazeti na kuendelea. “Hawa magabachoi wamezidi kupendeewa keibu katika kila kitu.”
Kabla ya kuendelea Kanji anapoka mic na kusema, “Sasa gabacholi nini na uza bwimbwi? Veve baguzi kama kaburu dugu yangu.”
Mgosi anapaaza sauti na kuuliza, “Hii nini kuachia Dhaan na Nivan Patel tena waliokamatwa na bwimbwi kama si ubaguzi? Wapi Shemtwashua, Shekiango, Shekwavi na wengine wanaooza mageezani kwa kesi za wizi wa kuku tena kubambikiziwa na ndata? Nikimbuka Chavda alivyoiba mabiioni ya shiingi akishiikiana na wezi wakubwa natamani kupiga mtu zongo.”
Kanji hajibu. Badala yake anatoa mimacho kama kunguru aliyenaswa ulimboni.
Mgosi kampata Kanji. Anamchokoza, “Osie bado iko vasi vasi na na ile sema mimi? Kama iko basi jua hii iko ukabuu nafanywa na kabuu veusi ikipendeea kaburu wa gabacholi kama Chawda naondoeewa kwa siri kama hii Kamuan Ahmed natoosha wanyama wetu hivi keibuni.”
Kanji anajibu, “Sasa kama nakamata na kuachia hindi mbili ndiyo hindi yote husika dugu yangu?”
Msomi aliyekuwa kimya akitabasamu na kufurahia mnyukano wa Mgosi na Kanji anaamua kuingilia kati. Anakohoa kidogo na kusema, “Kanji hebu uwe mkweli. Suala la kupendelewa kwa hawa anaosema Mgosi si siri tena. Ukienda kwenye Asjili Mwaijumba maeneo yote ya mjini ni wao.
Biashara zote nono wanamiliki na kuendesha wao. Ufisadi mkubwa kama vile dege lenye mafua la mkuu na mkangafu wa rada, Chavda ambaye nasikia alisharejea na anatanua mitaani, RITES, IPTL, kusafirisha wanyama nje ni wao. Sasa tuite hii nini bwana Kanji? Hata mitaa yetu ina jina ile ile wakati Bombay hapana taa moja naitwa jina ya kimakonde. Au siyo dugu yangu Kanji?”
“Du! Hii ngoma kweli imepiga vitabu! Yaani anachambua mambo kiasi cha hata kunguru kutingisha vichwa!” Anasema Mijjinga aliyekuwa ndiyo anaweza chini gazeti la Danganyika Always.
Msomi anatabasamu kwa kumwagiwa ujiko. Anaendelea, “Hili liko wazi kuwa kuna tatizo ambalo wakubwa wanajifanya kutoliona. They ignore all warnings and go on with their monkey biz as usual.
Hebu fikiria jinsi Matching guys aka Machinga wanavyosumbuliwa na migambo ya miji na majiji inayowaibia kila uchao wakati hawa ndugu zetu anaowatetea Kanji wakiendelea kufaidi ulinzi huu wa kibiashara.
Hebu fikiria ni kiasi gani cha misamaha ya kodi wanayopewa wafanyabiashara na wawekezaji waitwao wachukuaji ambao wengi ni wao na wageni. Je huu tuuiteje kama si ukaburu anaosema Mgosi?” Anakunywa kahawa yake na kumtazama Kanji kama anayemtaka ajibu hoja zake.
Mipawa aliyekuwa kimya anaamua kutia guu, “Mimi sizungishi. Kinachoendelea ni zaidi ya ukaburu na unazi. Makaburu na manazi walibagua watu ili kulinda watu wao na si hawa wanaobagua wachovu kulinda wageni ambao wengi waliletwa na wakoloni au kuingia kinyume cha sheria.
Msomi umesahau jamaa wa EPA aliyeachiwa na kirahisi rahisi hivi karibuni. La bwimbwi ni kwamba wanakamata na kuchukua unga na kuachia wauza kwa mlango wa nyuma. Ngoma droo mnaingizwa mjini na unga unapigwa bei au siyo?”
Sofia Lion aka Kanungaembe aliyekuwa akinong’onezea jambo Kanji anaamua kukatua mic, “Hii kaya ni ya Amani na mshikamano. Mistake kutuletea siasa zenu za kibaguzi. Nina hakika hamtafanikiwa hata mfanyeje. Hii kaya ina wenyewe na wenyewe ni sisi. Halo halo.” Anamkazia macho Mbwa Mwitu.
“Sofi unaujua ubaguzi au unausikia? Hebu nieleze. Unataka hiki walichoeleza Msomi na Mgosi tukiiteje? Hapa hakuna cha mshikamano na Amani bali mshikwamano na Imani ya Amani. 
Hata hivyo, sikushangai. Nikikumbuka ulivyokuwa unatetea ubaguzi wa kijinsia kupitia viti vya chupi sorry upendeleo na alipopendelewa na kusimikwa Anna Makidamakida baada ya kumbwaga mzee wa Viwango sina hamu. Ila ukweli unabaki pale pale kuwa huu ni mfumo wa kijambazi na kibaguzi.”
Mpemba aliyekuwa anamalizia kusoma gazeti anaamua kutia guu, “Wallahi naona hawa mahabusu mashujaa. Kama wachovu wote wangeona mambo kama hawa mahabusu bila shaka ubaguzi na ukaburu huu ungetokomezwa ati. Tushachoka na huu usanii wa kukamata na kutangaza halafu waachia wahusika toka magerezani kwa mlango wa nyuma.”
Msomi anaamua kuchomekea, “Usemacho Ami ni ukweli mtupu. Nani mara hii kasahau alichowahi kusema Idd Lion alipokuwa waziri wa biashara kuwa uchumi wa kaya unamilkiwa na jamaa kumi tu anaowatetea Kanji? Ajabu alipofichua ukweli huu hakuna aliyekereka wala kuhoji ni kwanini?”
“Nani ahaoji wakati wahusika wanalala kitanda kimoja na kunywa toka kwenye kikombe kimoja wakicheza muziki ule ule wa divide and rule au gawanya utawale? Ajabu wakati haya yakiendelea, kuna wamakonde waitwao Jarawa kule ugabacholini wanaobaguliwa na kutenzwa kama wanyama na hakuna anayejali!”
Kijiwe kikiwa kinanoga si likapita shumbwengu la Mwendesha mashitaki wa Sirikali anayeachia wauza bwibwi! Wacha tulirushie mitusi na mawe hadi likatokomea mitaa ya India na Indira Ghandhi.
Chanzo: Tanzania Daima Mei 14, 2014.

No comments: